Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  28 Jumada II 1445 Na: 1445/15
M.  Jumatano, 10 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hati ya Serikali Mpya Inaashiria Kuachiliwa zaidi kwa Rasilimali za Misri na Umiliki wa Umma
(Imetafsiriwa)

Serikali ya Misri inakusudia kuunga mkono na kuongeza mafanikio ya ubadilishanaji fedha za kigeni na mapato yanayolengwa ya dolari bilioni 300, ikiwakilisha takriban mara tatu ya viwango vya sasa vilivyopatikana kutoka kwa ubadilishanaji fedha za kigeni. Hii inakusudia kuimarisha mnyumbuko na ukakamavu wa uchumi wa Misri katika mbele ya migogoro, kulingana na hati iliyotolewa na Baraza la Mawaziri kuhusiana na “Mwelekeo wa Kiuchumi wa Kimkakati kwa Uchumi wa Misri wakati wa kipindi cha 2024-2030”. Hati hiyo imepangwa kuwasilishwa kwa mazungumzo ya kijamii kabla ya utekelezaji wake. Hati hiyo inaelezea vyanzo sita rasmi vya kukuza vyanzo vya ubadilishaji fedha za kigeni, na muhimu zaidi na hatari ikiwa ni kuunda kamati ya mawaziri ya kiwango cha juu kujadiliana na nchi na benki kadhaa ambazo ni wakopeshaji kwa Misri kwa kubadilishana deni la umma kwa hisa katika baadhi ya Kampuni zinazomilikiwa na serikali. Hii ni sehemu ya hati ya sera ya serikali, inayolenga kubadilisha 38% ya deni la nje la Misri kuwa uwekezaji. (Jukwaa la Habari la Mazid)

Kile ambacho serikali ya Misri inakusudia ni kuizamisha zaidi nchi katika kinamasi cha ubepari na kuendelea kwenye njia ya kuelekea janga kwa maamuzi ambayo madhara yake hayana tofauti na migogoro ambayo Misri inakabiliwa nayo sasa. Badala yake, wanawakilisha misiba ya ziada na kuondoka kutoka kwa suluhisho lolote. Inaonekana kana kwamba serikali haitafuti kwa dhati tiba kwa matatizo na migogoro ya watu.

Ndio, serikali haijali kuhusu Misri na watu wake, na haiwatazami kwa jicho la kinga. Badala yake, inawaona kama chanzo cha mapato yake, ikiwa sio chanzo msingi. Watu ndio wanaolipia bili za ufisadi na bili za utumiaji ovyo wa utajiri wa nchi hii kupitia ushuru wa ziada chini ya majina anuwai, na kupitia mfumko wa bei ambao humomonyoa akiba zao na hula juhudi zao.

Kwa kweli, kujaribu kupata fedha za kigeni sio suluhisho, haswa katika nchi ambayo huingiza karibu 90% ya matumizi yake, ya kwanza ulimwenguni kote katika uagizaji wa ngano licha ya kuwa taifa la kilimo lenye ardhi kubwa na uwezo wa kibinadamu wenye uwezo wa kulima. La kusikitisha, uwezo huu haujatumiwa ipasavyo. Kwa kuongezea, mbinu zinazotumiwa kupata fedha za kigeni sio tu ni duni lakini pia zenyewe ni uhalifu. Hii inajumuisha kupuuzwa kwa umiliki wa umma na kubadilishwa kwake kuwa umiliki wa kibinafsi, mara nyingi hukabidhiwa kwa wawekezaji wa kigeni, kimsingi ikiruhusu Magharibi kufanya ukiritimba kwa mabaki ya utajiri na rasilimali za nchi hii baada ya kupata udhibiti juu ya mafuta, gesi, dhahabu, na madini mengineyo. Magharibi inaonekana kutoshiba inapokuja katika damu na utajiri wetu. Walakini, lawama msingi iko kwa wale waliowezesha uporaji wa utajiri wetu, kulinda maslahi yao katika nchi yetu bila utunzaji wowote wa kweli kwa Misri na watu wake.

Masuluhisho yanayoibuka kutoka kwa mzunguko wa ubepari na akili za wale wanaofikiria ndani ya mfumo wake sio suluhisho la kweli; Badala yake, huunda migogoro mipya ambayo inaongeza mzigo kwa watu. Ni sawa na mtu anayejaribu kutoroka kutoka kwa wavuti wa buibui kwa kusonga mbele, ila tu kupata wavuti unamsokota, ikipunguza nafasi zao za kutoroka.

Kampuni ambazo serikali inakusudia kuziuza kwa badali ya deni lake hazimilikiwi na serikali, na wala bado hazijamilikiwa na serikali. Ni sehemu ya mzunguko wa umma, mithili ya kila kitu chengine ambacho serikali imekiondoa ovyo. Haiwezekani kwa serikali kuuza, kukodisha, au kupeana umiliki wa mali hizi kwa mtu yeyote kwa aina yoyote. Hatua halali pekee ni kwa serikali kuzisimamia vizuri na kugawa upya utajiri wanaotengeneza miongoni mwa watu. Kuuza au kutoa ni uhalifu dhidi ya Misri na watu wake.

Kutoa pesa sio suluhisho la kizungumkuti; bali, suluhisho liko katika kuwawezesha watu kupitia tasnia na kilimo, kutumia rasilimali za nchi, ardhi, maji, na anga, na kuzalisha utajiri kutoka kwazo. Hili linaweza kupatikana kwa kuchimba rasilimali kutoka kwenye ardhi na utengenezaji bidhaa au kuzitumia kwenye tasnia, na pia kukuza mazao ya kimkakati ambayo yanatufanya tusitegemee uagizaji, kama vile ngano na zingine. Kwa kuongezea, ni muhimu kutabanni kiwango cha dhahabu na fedha kama umbo lenye thamani la sarafu, badala ya kutegemea kakamilifu noti za benki ambazo yanaweza kukosa thamani ya dhati. Kwa njia hii, pesa zinaweza kuwa katika umbo la dhahabu au fedha, au karatasi wakilishi, na hatungeshuhudia mfumko wa bei au utofauti wa bei, kupunguza hitaji la fedha za kigeni zisizo na thamani ya dhati.

Suluhisho la migogoro na matatizo ya Misri sio gumu; Misri inamiliki dili kubwa sana, na inahitaji tu watu wenye kujitolea wenye utashi uhuru na maono ya kweli ya tiba, kama tulivyotaja baadhi yake, ambayo yote yanatoka kwa Uislamu, na hayawezi kutabikishwa kwa kutengwa na mfumo wake. Mfumo huu huyatazama matatizo ya watu kama maswala ya kibinadamu ambayo yana hukmu za kisheria zinazoonyesha jinsi ya kutibu na kushughulika nayo. Masuluhisho haya yanaweza kupatikana tu kupitia utekelezaji Uislamu chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

[وَإِذْ أَخَذَ اللهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ]

“Na pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana na walio pewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtokificha, walikitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwacho thamani duni. Basi ni kiovu hicho walicho nunua.” [Aali-Imran: 187]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu