Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  29 Shawwal 1445 Na: 23/1445
M.  Jumatano, 08 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Askari wa Kinana: Mtakutana na Mwenyezi Mungu kwa Namna Gani na Ni fedheha gani Mliyojiwekea juu ya Nafsi zenu?!
(Imetafsiriwa)

Misri imelaani vikali operesheni za kijeshi za uvamizi katika mji wa Rafah wa Palestina. Pia imechukulia, katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje hapo jana, kwamba ongezeko hilo hatari la ghasia linatishia maisha ya Wapalestina zaidi ya milioni moja ambao kimsingi wanategemea kivuko hiki kwani ndio tegemeo kuu la Ukanda wa Gaza, na njia salama kwa waliojeruhiwa na wagonjwa kuondoka ili kupokea matibabu, na kuingia kwa misaada ya kibinadamu kwa kina kaka na dada wa Kipalestina huko Gaza. Misri ilitoa wito kwa umbile la Kiyahudi kutumia viwango vya juu vya kujizidhibti, na kujiepusha na sera ya brinksmanship ambayo ina athari ya muda mrefu, na ambayo inaweza kutishia hatima ya juhudi kubwa zinazofanywa kufikia makubaliano endelevu ndani ya Ukanda wa Gaza. Misri pia ilitoa wito kwa pande zote za kimataifa zenye ushawishi kuingilia kati na kutoa shinikizo linalohitajika ili kutuliza mzozo uliopo na kuruhusu juhudi za kidiplomasia kufikia matokeo wanayotaka. Haya yanajiri saa chache baada ya jeshi la uvamizi kutangaza jana udhibiti wake wa upande wa Palestina wa kivuko cha mpaka cha Rafah na Misri, licha ya harakati ya Hamas kutangaza siku moja kabla ya jioni ya jana kuidhinisha pendekezo lililowasilishwa na Misri na Qatar la kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza. (Al-Ahram, Mei 8, 2024 M).

Huku watu wetu wakiuawa nchini Palestina, masafa ya karibu mno kutoka kwa ndugu zao katika jeshi la Kinana, ambapo wanasikia sauti za wito wao wa kuomba msaada na vilio vya watoto wao, na huku wamezingirwa na ndugu na adui, utawala wa Misri unatoa tamko la kulaani na kushutumu oparesheni za jeshi la Kiyahudi huko Rafah na udhibiti wake wa kivuko, kana kwamba utawala huo hauizingiri Gaza na watu wake na haushiriki na umbile nyakuzi linalowachinja! Kisha anaendelea kuzingatia mipango ya mabwana wake katika Ikulu ya White House, akitoa wito kwa pande zote za kimataifa zenye ushawishi kuingilia kati na kutoa shinikizo muhimu ili kutuliza mgogoro wa sasa, na kuruhusu juhudi za kidiplomasia kufikia matokeo wanayotaka! Diplomasia pekee, wakati Mayahudi wanawaua na kuwachoma moto watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa na kuvunja nyumba zao juu ya vichwa vyao, bila kuzingatia juhudi zinazohitajika za kidiplomasia ambazo serikali inazungumza, ambayo hakuzungumza juu ya juhudi za kidiplomasia nchini Libya, lakini badala yake alimuunga mkono kibaraka wa Marekani huko kwa kila aina ya usaidizi katika kutumikia maslahi ya Marekani na katika jitihada za kupanua ushawishi wake huko. Lakini hapa katika Ardhi Iliyobarikiwa, mipango ya Marekani ni tofauti, na Mayahudi ni wakaidi katika kuikubali na kunyenyekea kwao, na wanaichosha Marekani kwenda nao katika yale wanayoyataka, na Marekani inawafanya vibaraka wake kuwa ngao inayowalinda Mayahudi dhidi ya ghadhabu za watu na majeshi, na kuwalazimisha kuyafunga pingu majeshi hayo ili asitokee yeyote kati ya wakati huo ambaye atakasirika na kulidhuru umbile hilo nyakuzi na utawala wa Misri bila ya shaka ndiye mlinzi wa kwanza wa umbile hilo nyakuzi na silaha muhimu inayolilinda kutokana na taifa na sehemu muhimu zaidi ya kuba lake la kweli la chuma ambalo linajumuisha tawala zinazotawala nchi yetu kwa chuma na moto na kulizuia kunusuru watu wetu katika Ardhi Iliyobarikiwa na kuikomboa ardhi yote ya Uislamu huko.

Kadhia ya Palestina haiko Rafah wala katika kivuko chake, ambacho kimedhibitiwa na Mayahudi. Bali, ni kadhia ya Ummah mzima ambao ardhi yake imenyakuliwa na ambayo watu wake wanadhalilishwa mbele ya macho ya majeshi yake yaliyowekwa kwenye kambi zao, baadhi yake wakiwa masafa mafupi sana. Je, ni fedheha gani inayowapata watu hawa, na ni kwa njia gani watakutana na Mwenyezi Mungu Mtukufu, hali wao wanajukumu mbele yake, kuhusu hilo na faradhi ya kuikomboa na kuwanusuru watu wake kikamilifu?!

Enyi Wanajeshi wa Kinana: Wajibu wenu ni kuikomboa Palestina yote, kuwanusuru watu wake wanaodhulumiwa, na kuwaondolea dhulma, na kung'oa kila kinachowazuia nyinyi kutekeleza wajibu huu, zikiwemo tawala na watawala waovu. Kwa hivyo mtafanya nini?! Wallahi, watawala hawa hawatokufaeni na wala hawatakubebeeni pigo hata moja la Moto wa Jahannam mbele ya Mwenyezi Mungu, basi msiwasikilize wala kuwatii katika kumuasi Mwenyezi Mungu, na ni dhambi gani kubwa kuliko kuwatelekeza ndugu zenu katika Ardhi Iliyobarikiwa! Je, hamjasikia maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

«مَا مِنْ امْرِئٍ يَخْذُلُ امْرَأً مُسْلِماً فِي مَوْضِعٍ تُنْتَهَكُ فِيهِ حُرْمَتُهُ وَيُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ إِلَّا خَذَلَهُ اللهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ فِيهِ نُصْرَتَهُ، وَمَا مِنْ امْرِئٍ يَنْصُرُ مُسْلِماً فِي مَوْضِعٍ يُنْتَقَصُ فِيهِ مِنْ عِرْضِهِ وَيُنْتَهَكُ فِيهِ مِنْ حُرْمَتِهِ إِلَّا نَصَرَهُ اللهُ فِي مَوْطِنٍ يُحِبُّ نُصْرَتَهُ» “Hakuna mtu (Muislamu)  yeyote atakayemtelekeza Muislamu katika sehemu ambayo utukufu wake unakiukwa na heshima yake inavunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamtelekeza katika sehemu ambayo angependa kupata nusra yake; na hakuna mtu (Muislamu)  yeyote atakayemnusuru Muislamu katika sehemu ambayo utukufu wake unakiukwa na heshima yake inavunjwa isipokuwa Mwenyezi Mungu atamnusuru katika sehemu ambayo angependa kupata nusra yake.” Uko wapi mwitikio wenu kwa kilio cha wafiwa, wanawake, na wazee? Uko wapi mwitikio wenu kwa kilio cha wafiwa, wanawake, na wazee? Wako wapi wafuasi wenu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambaye alitangaza mkusanyiko wa jumla na akaelekea kuifungua Makka kwa ushindi wa Khuza’a na akasema: “Umekuwa mshindi, ewe Amr bin Salem.” Na akasema: “Mwenyezi Mungu hatanipa ushindi ikiwa sitawanusuru Banu Ka’b”?! Muko wapi kuhusiana na Al-Muutasim, ambaye mwanamke mmoja alimuomba msaada na akaitikia kumnusuru na kuifungua Amuriya kuipa ushindi?! Basi muko wapi katika maelfu ya wanawake wanaokuombeni msaada na wazee wanaokuombeni msaada na watoto wanaokuiteni nyuma ya uzio na kuta, “kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Ewe Mmisri”?! Mayowe ambayo watu wameamsha fahari kwa watu waadilifu duniani kote, na yakapita karibu nanyi kana kwamba hamkuwasikia, na ni kina kaka na dada zenu na familia yenu! Kwa hivyo hisia yenu ya wajibu iko wapi? Imani yenu na Uislamu uko wapi? Iko wapi hisani yenu mnayoipigia kelele?! Wallahi hamuna udhuru leo, na aibu yenu haitafutika! Hata kwa damu!

Enyi Askari wa al-Kinana, Enyi Askari bora: Wema si nishani, bali ni amana ambayo mtaulizwa, na ni wale tu wanaoibeba bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) wanaoistahiki. Mujahidina kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kuwanusuru waliodhulumiwa, watiifu kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Dini yake. Hakuna utiifu kwao juu ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na hawana utiifu kwa watawala wanaochukua amri kutoka kwa nchi za Magharibi, kutekeleza mifumo yake, kutekeleza miradi yake ya kikoloni, na kuwazuia kuukomboa Ummah na kuwanusuru wanyonge ndani yao. Hawa ndio wanaostahiki wema kweli. Kwa hiyo Je, nyinyi ni miongoni mwao? Jijibuni kabla ya kukuulizeni Mwenyezi Mungu Mtukufu, na simameni kumnusuru Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Dini yake, na muitoe potofu hii kutoka kwenye mizizi yake na kila anayekuja baina yenu nayo na akuzuieni kuing'oa kutoka kwa watawala waovu na usaliti. Ni amana ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), basi ihifadhini na muwe ni watu wake na ngao kwa Umma huu, walinzi wake na wasaidizi wa waliodhulumiwa ndani yake, wakisimamia dini yake na maisha yake ya dunia. Msipofanya hivyo na kukiuka matukufu ya Umma na kuuvunjia utakatifu wake kama inavyotokea sasa, basi hamna kheri kwenu wala hamna heshima kwenu, basi muonyesheni Mwenyezi Mungu yale anayoyapenda kutoka kwenu, na muonyesheni kuwa nyinyi  munastahiki kheri hii kwa kubeba bendera ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa namna bora na kuwanusuru wanyonge kama alivyofanya, kuikomboa ardhi ya Uislamu iliyonyakuliwa na Mayahudi na kuwanusuru watu wa Ardhi Iliyobarikiwa ambao utakatifu wao unakiukwa. Na jueni kwamba wajibu wenu ni kuondosha kila kitu ambacho kinakuzuilieni kufanya yale ambayo Mwenyezi Mungu Amekuamrisheni kwa hoja kwamba “Wajibu wowote ambao hauwezi kukamilika bila ya jambo maalumu jambo hilo pia ni wajibu.” Basi uondoeni utawala huu unaokuleteeni aibu na mnaoshiriki ndani yake na unaomlinda adui wa Mwenyezi Mungu na adui yenu, na msimamishe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama dola inayonyanyua majeshi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya haki na kuwanusuru watu wake; Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Kuweni na hasira, enyi Askari wa Kinana, na hasira zenu ziwe ni dalili inayothibitisha ukweli kwa maneno ya Mwenyezi Mungu na kukata njia ya wahalifu.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu