Afisi ya Habari
Wilayah Misri
H. 8 Jumada I 1441 | Na: 1441/04 |
M. Jumatatu, 13 Januari 2020 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Makubaliano ndani ya Sanduku!
Enyi Muliokubali, Njooni katika Neno ambalo kwamba ni Sawa kati Yetu na Nyinyi
(Imetafsiriwa)
Masharti ya waraka yaliowasilishwa na Muhammad Ali hayakutofautiana kutokamana na katiba ya Misri katika hatua ya awali, kwa kupuuza kwake imani ya watu wa Misri na hamu yao ya kuishi kwa mujibu wa Uislamu. Kusisitiza usekula wa serikali kwa maandishi ya wazi ambayo hayawezi kutafsiriwa vibaya, yaliyofunikwa na maana pana na kauli mbiu kuhusu uadilifu, usawa na kanuni ya sheria, kana kwamba Sisi na kabla yake Mubarak, awakunyanyua kauli mbiu kama hizo na hawakulingania kanuni ya sheria. Badala yake, Mubarak alikuwa akisema kuwa anatawala kwa demokrasia. Na uhakika wa mambo ni kuwa utekelezaji wa demokrasia ni wazo la kufikiriwa kwanza. Nguvu hazipeanwi kwa watu (katika demokrasia), lakini badala yake inadhibitiwa na wenye mtaji pamoja na zana wanazomiliki kubadilisha maoni ya Ummah kulingana na maono yao na kile kinachoshughulikia maslahi yao. Hili halitekelezwi katika nchi zetu peke yake, lakini hata Ulaya na Amerika, kwa hivyo hakuna mzozo wa kutaka uongozi nchini Amerika, kwa mfano, isipokuwa kwa uteuzi kwa Republicans au Democrats, yaani mtu yeyote atakayechaguliwa wanaoamua mambo kuwa mbele ya nidhamu ya kirasilimali. Hii ndio demokrasia iliyowekwa kwetu katika nchi yetu, nidhamu ya kiuchumi ya kirasilimali pekee ndiyo inayotumika kwa njia ya kweli na kamili kwa sababu hutumikia maslahi ya kampuni kubwa au warasilimali wakubwa.
Kwa hivyo, madai ya kwamba nidhamu ya serikali nchini Misri ni ya kiraia, ya kidemokrasia, ni uhakikisho kwa nchi kuu, kwamba hatutatoka nje ya mfumo na hatuta fikiria nje ya sanduku na kwamba tutadumisha utegemezi wetu kwenu na tutatunza maslahi yenu ndani yake kama ilivyokuzwa na watangulizi wetu.
Ukweli wa mambo ni kwamba kipengee hiki hufuta kila kitu kitakachofuata. Uhifadhi wa serikali ya kiraia na kuponea kwa nidhamu ya uongozi ya kirasilimani ni uhifadhi wa ugonjwa na kudumisha muendelezo wa uporaji wa utajiri wa nchi kwa manufaa ya wamagharibi na kuhalalisha uporaji huu. Kwa hivyo hakuna heshima, uadilifu au usawa kwa kuponea nidhamu ya serikali ya kiraia ya kidemokrasia, bila kujali nyuso zinazotekeleza nidhamu hii kubadilika, na hata ikiwa watatupa kwa watu baadhi ya makombo ya meza, wanaweza kuwavuruga wao kwa muda. Walakini, haki za watu hazina dhamana kwenye demokrasia, kwa sheria zake zinazowawezesha Wamagharibi kupata utajiri wa nchi, na kuhalalisha uporaji huu, na nchi imefungwa na mikopo inayoweka rehani uchumi wake na sera kwa maamuzi ya Wamagharibi.
Wale ambao wanataka kweli kuiokoa Misri lazima wafikirie nje ya mfumo na kuzitoa akili zao nje ya sanduku ambalo Wamagharibi waliliweka, na kuviangalia vitu kutoka upande mwingine tofauti na mtazamo wa Wamagharibi, suluhisho, na tiba. Tiba za Wamagharibi na sheria za kimataifa ambazo Muhammad Ali alizitegemea katika waraka wake hazikuwekwa kwa ajili ya nchi yetu lakini badala yake kwa ajili ya nchi maalumu kuhakikisha maslahi yao tu, na wao wenyewe hawazifuati hizo sheria walizoziweka, ikiwa zinagongana na maslahi yao na kuna mifano mingi ya hili.
Hiyo ndiyo sababu mtu yeyote anayetaka uzuri wa kweli kwa Misri lazima atafute mradi mbadala wa kistaarabu unaokabiliana na nidhamu hii ya kirasilimali na kushindana na ufisadi wake na tiba za kweli kwa matatizo ya watu zilizo juu ya watu. Kung’olewa kwa watu, hata wakiwa muhimu, lazima iambatane na kuing’oa serikali pamoja na sera zake zote, zana, alama, na utamaduni; na inapaswa kubadilishwa na nidhamu halisi katika chanzo chake na matibabu yake ambayo hayatumiki kwa wanadamu na hayatofautishi kati yao. Lakini badala yake inawatizama wao wote kama watawala na watawaliwa, masikini na tajiri, pasina dini, dhehebu au mapendeleo ya kikabila, na hili linapatikana pekee katika mradi wa Kiislamu uliostaarabika pamoja na sheria zake zinahakikisha uadilifu, heshima, ukombozi na usawa kwa watu wote, Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Mradi wa kistaarabu wa Kiislamu ni serikali ya Khilafah ya Uongofu kwa njia ya Utume, ambayo sisi Hizb ut Tahrir tunawaalika kukubaliana nayo.
Mwaliko kama ule ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliwapa wajumbe wa Najrani: Njooni katika neno ambalo kwamba ni sawa kati yetu na nyinyi, kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio maregeo yetu, na kuwa sheria ndio hakimu kati yetu, na kuwa twazingatia yanayofanyakazi kwa Misri na watu wake na Ummah kwa ujumla, ilikuwa namna gani na vipi itakuwa, na kwa uhakika ni kwamba hakuna mageuzi nchini Misri bila ya Uislamu na nidhamu yake, sheria yake, kanuni zake na sheria ambazo zimeitoa Misri kutokamana na dhulma za Warumi na kuwadhamini wao hesima yao na ukombozi na kuwaregeshea utajiri wao ambao uliporwa na Warumi wakati huo. Na hivi sasa Misri haitatoka katika ukandamizaji wa Wamagharibi na urasilimali wake, na haitokombolewa kutokamana na utumwa wa mikopo yake isipokuwa kwa Uislamu. Hili ndilo tunalowalingania nyinyi katika Hizb ut Tahrir, kukubaliana juu yake na ni njia pekee ya wema kwa Misri na watu wake na sio kwa njia nyingine zozote na makubaliano ni juu yake pekee, na kubakia katikati ni njia katika kutofaulu na kujizuia dhidi ya hamu ya watu na mazao ya nidhamu ambayo imewafanya wao kuonja shida.
Muhammad Ali alitangaza waraka wake na akasema kuwa ni sehemu ya mradi wa kuunganisha nyadhifa za upinzani wa Misri au vikosi vya kitaifa. Pia alitaja kuwa alikutana na wawakilishi wa mikondo yote ya kisiasa na muelekeo wa kifikra nchini Misri, na kwamba alifanya kazi na kila mtu kutafuta hatua za kawaida zinazoepuka migogoro na kuanzisha ushirikiano kuiokoa Misri na kurudi kwa uhuru, hadhi na uadilifu kwa watu wa Misri. Kisha akatangaza masharti ya waraka wake ambayo alitaka makubaliano, na wale wanaotaka kuiokoa Misri, na kwa bahati mbaya yote ni kulingana na maono ya Wamagharibi na kutokamana na upande wake na kwa misingi ya itikadi yake inayotawala nchi yetu kwa miongo kadhaa ambayo tumeonja shida, lakini badala yake ndio sababu ya shida zetu zote. Sisi, Mubarak na wengineo, ni mazao ya nidhamu hii, na kulifunga tatizo kwa mtu binafsi kama Sisi ni kuwadanganya watu tena na kuwavutia wao kubadilisha sura badala ya kubadilisha nidhamu na jaribio la kusema kuwa majanga si nidhamu ya kisekula ya kidemokrasia yenyewe bali ni wale wanaoitekeleza, wakati uhakika asili ya ugonjwa ni nidhamu ya demokrasia, inayotengeneza mchanga wenye rutuba kwa aina zote za ufisadi na rushwa.
Yatakikana itambulike kuwa Amerika, inayoidhibiti Misri inajua upendo wa watu wa Misri kwa Uislamu na kuogopa kutokuwa na subra kwao kwa sababu ya sera za vibaraka wake walioko uongozini, inaweza kugeuka kuwa mapinduzi ambayo yataleta watawala ambao watatekeleza Uislamu kiukweli. Na kwa hili inadandia matukio na kujaribu kubadilisha wimbi la mzozo kwa kulifanya liwe na rangi safi ya usekula kwa kuhakikisha maslahi yao, ambayo inajua kwa hakika kuwa haitapata na haitapokea utajiri wowote wa Misri lau serikali itabadilika bila mapenzi yake, Misri itageuka kuwa serikali ambayo inatekeleza Uislamu na ni nukta kianzio kwa serikali ya Khilafah kwa njia ya Utume, kwa sababu mapambano yao ya kweli ni kwa Uislamu ambao unakata mikono yao inayopora utajiri wa nchi yetu, sio Misri peke yake.
Mwisho, uamuzi uko katika mikono ya watu waaminifu wa Jeshi la Kinana (Misri), na wao pekee wanauwezo wa kubadilisha mahesabu ikiwa wataacha kuwaangusha Ummah wao na kuunga mkono dini yao na mradi wa kustaarabika unaotokamana nao na mdhamini pekee wa mazuri ya Misri na watu wake na hata Ummah kwa ujumla na hata ulimwengu wote, ambao umekumbwa na moto wa urasilimali na ukatili wake. Kwa hivyo iungeni mikono yenu, Enyi mukhlisina, pamoja na mikono ya ndugu zenu, ambao wanauwezo wa kutekeleza Uislamu katika serikali yake, Khilafa ya Uongofu kwa njia ya Utume. Nusra (msaada) kama nusra ya Maanswari, ambao inaregesha uadilifu katika ardhi, inasawazisha nguvu, na kufufua Ummah wa Kiislamu kama bwana wa ulimwengu kwani inasambaza wema na uadilifu na kuwatoa watu katika dhulma na kiza cha urasilimali na kuwaweka wao katika uadilifu na huruma ya Uislamu, ambao Mtume wetu (saw) aliweka msingi wake na akafuatwa na maswahaba watukufu. Kwa hivyo fuateni njia yao ili Mwenyezi Mungu (swt) atukusanye pamoja na nyinyi na wao katika hadhi hapa duniani na akhera, Ewe mwenyezi Mungu, ifanye iwe karibu badala ya baadaye.
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ)
“Enyi mulioamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Misri
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Misri |
Address & Website Tel: http://hizb.net/ |
E-Mail: info@hizb.net |