Ijumaa, 29 Rabi' al-thani 1446 | 2024/11/01
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  20 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 26/1445
M.  Jumanne, 28 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mkataba wa Khiyana Unalinda Umbile la Kiyahudi na Kulifanya Jeshi la Misri kuwa Mshirika katika Uhalifu wake, Kumwaga Damu ya Wanajeshi wa Kinanah
(Imetafsiriwa)

Mwanajeshi mmoja wa Misri aliuawa katika makabiliano ya risasi kati ya wanajeshi wa 'Israel' na Misri kwenye kivuko cha Rafah mnamo siku ya Jumatatu, kama ilivyothibitishwa na Shirika la Utangazaji la 'Israel'. (Sky News Arabia, 27/5/2024).

Uhalifu wa Mayahudi haujaisha na hautaisha maadamu wana umbile na uwepo katika Ardhi yetu Iliyobarikiwa. Wao ni umbile lililowekwa kuwa kisu katika upande wa Ummah wetu, wakidhalilisha utu wake, wakidhalilisha heshima yake, na kuchafua fahari yake katika matope ya unyonge wao. Kama tulivyosema mara kwa mara, wao ni kambi ya hali ya juu ya Magharibi ambayo inapurukusha ukweli kwamba Magharibi ni adui wa mkuu wa Ummah, inalinda maslahi yake, inagawanya Ummah, na inazuia kuanzishwa kwa dola inayounganisha chini ya  Rayah (bendera) ya Uislamu.

Hili la kuuawa kwa askari wa jeshi la Kinanah na umbile hilo nyakuzi si la kwanza na halitakuwa la mwisho. Upande wa Misri unatangaza tu baada ya tangazo la Mayahudi, na serikali inajaribu kuficha na kuziba jinai hizi ili kudhibiti hasira iliyokandamizwa ndani ya jeshi, achilia mbali hasira inayozidi kati ya watu. Mayahudi wanaendelea na dhulma yao, wakijua kwamba kamba za utawala huo zote ziko mikononi mwa Marekani, ambayo inawaunga mkono wao na umbile lao katili. Wanajua kuwa serikali hiyo imekabidhiwa ulinzi wao na hawatasubutu kufanya vyenginevyo, hata ikibidi kuua na kuwatia nguvuni waliokasirishwa wenyewe.

Udhalilishaji huu tunaoushuhudia haungetokea lau Jeshi la Kinana lingesonga na shambulizi la kwanza dhidi ya watu wetu nchini Palestina na kuwajibu Mayahudi kwa nguvu za Harun al-Rashid, hasira za al-Mu'tasim, na ari kwa ajili ya Mwenyezi Mungu kama ile ya Qutuz, akiwatangazia Mayahudi kwamba hakuna mahali pao katika ardhi yetu na hakuna maisha kwao miongoni mwetu. Tunasimama kwa ajili ya Uislamu, ardhi yake, na matukufu yake. Tunalinda hifadhi ya Dini hii, tunaulinda Ummah huu, Dini yake, na wanaodhulumiwa, tunawakusanya wenzetu, na kutembee pamoja nao ili kuling'oa umbile hilo potovu na wale wote wanaolilinda, tukianzia na viti vya watawala wetu ambavyo vimeharibiwa na kuoza kwa kutu.

Enyi Askari wa Kinanah: Kunyamaza kwenu kimya juu ya uhalifu wa Mayahudi kumedumu vya kutosha, na sasa mikono yao imekufikieni. Mtafanya nini sasa? Je, utiifu wenu utabaki hadi lini kwa mapatano ya fedheha na ya khiyana ambayo yanakufungeni pingu, yanalinda umbile la Kiyahudi, na kuliwezesha kutawala shingo za ndugu zenu katika Ardhi Iliyobarikiwa, na shingo zenu pia? Ni wajibu wenu kuwanusuru na kuwamaliza wale wanaowadhulumu. Je, mmekubali vipi msimamo huu wa utelekezaji kwenu wenyewe?!

Makubaliano ya khiyana yanayokufungeni hayana uhalali, na wala hamtakiwi kuyakubali wala kuyaheshimu au kutimiza khiyana zake kwa Mwenyezi Mungu, Mtume wake na Dini yake. Badala yake, lazima muyakane, muyakatae, na wale waliyaotia sahihi na kushikamana nayo au kuyatambua yaliyomo ndani yake hadi leo, basi jueni kwamba nyinyi ni washirika wa Mayahudi katika uhalifu wao dhidi ya Ummah wenu na kuwauwa ndugu zenu. Mtajumuishwa katika hasira ya Mwenyezi Mungu na ghadhabu yake na adhabu yake. Kwa hiyo, jichagulieni sasa, kwa maana jambo hili ni zito, si dogo.

Enyi Wanajeshi wa Kinana, Enyi Wanajeshi Bora: Kheri aliyoizungumzia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) inakutakeni muwe walinzi wa Ummah, kupigana vita dhidi ya maadui zake, kutoutishia Ummah wenu wenyewe huku mkihakikisha usalama wa adui wa Mwenyezi Mungu na adui yake. Hamu yenu haipasei iwe kuhifadhi tawala zinazotawala kwa niaba ya nchi za Magharibi, kulinda maslahi yake, na kuufanya Ummah utiishwe, huku mali na rasilimali zake zikifujwa. Je, haya siyo yanayotokea sasa mbele ya macho yenu na chini ya uangalizi wenu? Je, hii sio serikali inayoweka amani na Mayahudi, kuwazingira, na kuwatiisha watu wa Ardhi Iliyobarikiwa na hata watu wa Kinana? Je, huu sio utawala unaopoteza damu za askari wa Kinana baada ya kuwafanya walinzi wa Mayahudi na kutumia rasilimali zote za Misri kwa ajili ya utumishi na utunzaji wao? Mnawezaje, kwa kiapa cha Mola wenu Mlezi, mnaweza kustahamili utawala wa namna hii? Mnawezaje kukubali udhalilifu kama huu na fedheha kama hii kwenu wenyewe? Mnawezaje kudai kustahiki kheri chini ya utawala huu unaotawala kwa ubepari wa Kimagharibi, unaojali maslahi yake, na kulinda umbile lake lisio halali? Yeyote afanyaye hivi au kukubali haya hana kheri ndani yake.

Kataeni utawala huu kama vile mungeutupilia mbali kwenye shimo la tende, kateni mafungamano nao, na muunganishe mafungamano yenu na ndugu zenu wenye ikhlasi katika Hizb ut Tahrir, ambao wamekuusieni bila kuchoka na kukuiteni kwenye kheri ya dunia hii na Akhera. Nusuruni mradi wa kweli wa Kiislamu kwa nusra ya dhati, mukitekeleza hukmu zake katika dola ambayo hata miti, mawe, na ndege wa angani watastawi chini ya kivuli chake: Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mnusuru wenu na Msaidizi wenu, wala hatayaacha matendo yenu yapite patupu.

[وَلَيَنْصُرَنَّ اللهُ مَنْ يَنْصُرُهُ إِنَّ اللهَ لَقَوِيٌّ عَزِيزٌ * الَّذِينَ إِنْ مَكَّنَّاهُمْ فِي الْأَرْضِ أَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ وَأَمَرُوا بِالْمَعْرُوفِ وَنَهَوْا عَنِ الْمُنْكَرِ وَلِلَّهِ عَاقِبَةُ الْأُمُورِ]

“Na bila ya shaka Mwenyezi Mungu humsaidia yule anaye msaidia Yeye. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Mtukufu. (40) Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Sala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya. Na kwa Mwenyezi Mungu ndio marejeo ya mambo yote.” [Al-Hajj:40-41].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu