Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Vikundi Tawala vya Pakistan vinamkaribisha Bwana wao Mpya wa Kikoloni, Trump, na Kumhakikishia Utayari wao wa Kutekeleza Maagizo yake

Nguvu ya Ummah haitatokana na mabadiliko ya siasa za ndani za dola kandamizi za kikoloni. Itatokana na kung'olewa kwa watawala vibaraka katika miji mikuu ya Waislamu. Ni wakati sasa wa kuanzishwa kwa mapinduzi ya Khilafah Rashida kwenye magofu ya tawala hizi za vibaraka. Kwa nini basi mabadiliko hayo bado hayajatokea jijini Islamabad, Enyi maafisa na askari wa Jeshi la Pakistani?!

Soma zaidi...

Mswada wa Marekebisho ya 26 ya Katiba: Chini ya Khilafah, Madaraka na Mamlaka Vinaamuliwa na Qur'an Tukufu na Sunnah, Wakati Kuna Mivutano ya Kuendelea ya Madaraka Chini ya Demokrasia

Chini ya mfumo tawala wa Demokrasia, mzizi halisi wa ufisadi ni uwezo wa walio wengi waliochaguliwa kubadili kila sheria, kila kifungu cha katiba, kila kanuni na kila agizo. Nguvu ya kutunga sheria inavipa vikundi tawala uwezo wa kubadilisha sheria kulingana na maslahi yao, sio tu kupitia mlango wa nyuma, lakini kupitia mlango wa mbele. Nguvu ya sheria ndiyo inayoliruhusu Bunge kuhalalisha wizi unaofanywa na waporaji na wafujaji kupitia Sheria ya Maridhiano ya Kitaifa, kukubali kunyang'anywa madaraka na madikteta kwa nguvu, kupitisha mipango kadhaa ya msamaha kwa mirengo inayotawala na kutoa kinga ya kikatiba ya kutoshtakiwa kwa wale wanaohusika na mambo muhimu zaidi ya nchi.

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir ni Chama cha Kisiasa Ambacho Mfumo Wake ni Uislamu. Kamwe Hakina Uhusiano wowote na Uanamgambo

Hizb ut Tahrir haina uhusiano wowote na uanamgambo. Hata hivyo, watawala wa Waislamu wanaogopa kazi ya Hizb ut Tahrir kwa sababu mradi wa Khilafah ni badali ya kimfumo na ya kisiasa kwa mfumo wa sasa wa dunia. Watawala wa Waislamu hawawezi kupambana kifikra na misimamo ya kifikra ya Hizb ut Tahrir. Wao, kwa hivyo hukimbilia uongo ili kuichafua kazi ya kisiasa na kifikra ya Hizb. Wanaunda uhalali wa kuwanyima wanachama wa Hizb haki zao za kisiasa.

Soma zaidi...

Imepita Mwaka Mmoja Tangu Mauaji ya Halaiki mjini Gaza Yaanze! Umma wa Kiislamu na Majeshi Yake Lazima Usimamisha Tena Khilafah Rashida na Kuikomboa Palestina

Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Mumeshuhudia kupuuza kwa watawala na makamanda wa kijeshi wa Waislamu kwa mwaka mmoja sasa. Uislamu haukubali fikra kwamba adui akiishambulia Islamabad, munajibu kwa nguvu, lakini adui akiishambulia Al-Masjid Al-Aqsa, si jukumu lenu kujibu. Uislamu haukubali fikra kwamba adui akiikalia kimabavu Lahore, mutamfukuza adui kwa gharama yoyote ile, lakini adui akiikalia kimabavu Al-Quds, si jukumu lenu kumfukuza. Uislamu haukubali kwamba munawajibika kuilinda ardhi ya Pakistan, lakini sio kuilinda Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina.

Soma zaidi...

Msimamo Dhaifu wa Watawala wa Pakistan kwa Kashmir Inayokaliwa Kimabavu Wampa Ujasiri Mvamizi India

Msimamo dhaifu wa watawala wa Pakistan ni kwa sababu ya ubaraka wao kwa Amerika. Hata kabla ya kuisalimisha Kashmir kwa India mnamo Agosti 2019, watawala wa Pakistan hawakuwa makini kuhusu ukombozi wa Kashmir Inayokaliwa kimabavu. Watawala wa Pakistan walifuata tu sera ya Amerika ya kutoa shinikizo kwa India, ili iingie kwenye kambi ya Amerika. Baada ya India kuingia katika kambi ya Marekani kupitia kundi tawala la Hindutva, watawala wa Pakistan waliachana na Kashmir Inayokaliwa kimabavu ili kuifurahisha Amerika.

Soma zaidi...

Umbile la Kiyahudi Lawaua Waislamu nchini Lebanon na Palestina Kwa Sababu ya Mwaka Mzima wa Kutochukua Hatua kwa Watawala wa Waislamu na Makamanda wao wa Jeshi

Imepita mwaka mmoja tangu jeshi la watu waoga zaidi katika uso wa dunia kuanza mauaji ya halaiki huko Gaza. Mnawezaje bado kukubali kudhalilishwa, vifo na uharibifu kama huu uliowekwa juu ya watu wenu, mbele ya macho yenu? Vipi bado mnaweza kubaki tuli, ilhali ni kwa kupitia nguvu za mikono yenu ndipo Ummah unatafuta ulinzi wake? Je, mwanajeshi anaweza kukubali ukuu wa kijeshi wa adui yake, bila kufyatua risasi hata moja? Je, askari anawezaje kukataa kupigana na adui yake, na kudumisha Dini yake, heshima na uanaume wake imara?

Soma zaidi...

India Inafanya Kazi Kutishia Ugavi Wetu wa Maji, Huku Watawala wa Pakistan Wakifanya Kazi Kusawazisha Mahusiano na Mchokozi

Licha ya kupita siku nyingi, watawala wa Pakistan bado hawajajibu ipasavyo hatua hatari ya India kuhusiana na Mkataba wa Maji wa Indus (IWT), makubaliano ya kugawanya maji yaliyosimamiwa na Benki ya Dunia mnamo 1960. Mnamo 18 Septemba 2024, India ilituma notisi rasmi kwa Pakistan, ikitaja masuala mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya idadi ya watu, changamoto za kimazingira, na mambo mengine, ikiomba kutathminiwa upya kwa mkataba huo. India imeripotiwa kutuma barua nne tangu Januari 2023, ikitaka uhakiki.

Soma zaidi...

Marekani Yazipatia India na Umbile la Kiyahudi Silaha za Kisasa, Huku Ikiweka Vikwazo kwa Mpango wa Makombora ya Ballistiki wa Pakistan

Sera ya Marekani kwa Ulimwengu wa Kiislamu ni sera ya kuwatiisha na kuwadhalilisha Waislamu, kwa kuungwa mkono na kuwatia nguvu maadui wa Ummah. Kuhusu Pakistan haswa, Marekani inataka kuidhoofisha Pakistan ili kuruhusu India kuinuka, ili Dola hiyo ya Kibaniani iweze kukabiliana na Waislamu na China kwa niaba yake.

Soma zaidi...

Komesheni Kupigania Vyeo na Marupurupu katika Jeshi la Pakistan. Badala yake, Maafisa wa Jeshi Waislamu Lazima Watoe Nusrah kwa ajili ya Kusimamisha Khilafah Rashida

Katikati ya utakaso wa sasa na kuwekwa kando maafisa ambao wanampinga mkuu wa sasa wa jeshi la Pakistan, ilijiri kutajwa kwa Hizb ut Tahrir. Gazeti maarufu la Kiurdu la “Daily Jang,” liliripoti mnamo tarehe 13 Agosti 2024, katika toleo lake kwa jiji la jeshi la Rawalpindi kwamba, “(2011) Brigedia Ali Khan alifikishwa mahakama ya kijeshi kwa kuwa na uhusiano na shirika lenye itikadi kali la Hizb ut Tahrir. Pia alituhumiwa kwa kueneza uasi ndani ya Jeshi la Pakistan.”

Soma zaidi...

Umbile la Mayahudi wa Kizayuni Linakiuka Matukufu Yetu Lipendavyo, Huku Watawala wa Waislamu Wakiyafungia Majeshi Yetu kwenye Kambi Zao

Mnamo asubuhi ya tarehe 31 Julai 2024, umbile la Kiyahudi lilimuua shahidi kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh katika shambulizi la kombora jijini Tehran, mji mkuu wa Iran. Siku moja kabla, umbile hilo la Kiyahudi lilimuua shahidi kamanda wa Hezbollah kwa kushambulia jengo la makaazi jijini Beirut, Lebanon. Hapo awali, umbile la Kiyahudi lilishambulia vituo mbalimbali katika bandari ya Hodeida nchini Yemen kwa ndege za kivita. Hii ni huku Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina ikiwa imegeuzwa kuwa magofu katika kipindi cha miezi kumi iliyopita.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu