Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  1 Dhu al-Qi'dah 1442 Na: 1442 / 82
M.  Jumamosi, 12 Juni 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Badala ya Kumzika Raj Mkoloni wa Kiamerika katika Makaburi ya Himaya, Afghanistan, Serikali ya Bajwa-Imran Yaipa Nguvu

(Imetafsiriwa)

Kwa kushikilia mila yao ya zamani ya kuudanganya Ummah, waziri wa mambo ya nje, wizara ya mambo ya nje na maafisa wengine wa serikali waliwarusha vumbi machoni mwa Waislamu, wakikanusha kwa nguvu kuwepo kwa kambi ya kijeshi ya Amerika. Lakini ripoti ya New York Times ilifichua udanganyifu wao, ikisisitiza kuwa Pakistan bado iko kwenye mazungumzo na Amerika katika kiwango cha juu kabisa, kuhamisha muundo wa jeshi la Amerika kutoka Afghanistan kwenda Pakistan, na maelezo anuwai yanafanyiwa kazi hivi sasa. Likifafanua ripoti yake ya Juni, gazeti hilo liliweka wazi kwamba Mkurugenzi wa CIA, William J. Burns, alikuwa amefanya ziara ya siri jijini Islamabad hivi karibuni na kukutana na Mkuu wa Jeshi, Jenerali Qamar Javed Bajwa na Mkurugenzi Mkuu ISI, Jenerali Faiz Hameed. Waziri wa Ulinzi wa Amerika, Lloyd J. Austin, pia yuko katika mawasiliano ya kila mara na Jenerali Bajwa. Madhumuni ya kuwa na kambi hii ya kijeshi na muundo wa jeshi nchini Pakistan ni kutekeleza operesheni dhidi ya kile kinachoitwa ugaidi nchini Afghanistan. Lakini, itaunda pia uwezo wa Amerika kufanya shughuli za kigaidi ndani ya Pakistan, na pia ujasusi dhidi ya maeneo yetu ya kinyuklia. Pia itasaidia Amerika kuongeza uwezo wake wa mawasiliano ya simu na kuashiria ujasusi katika eneo letu, kulinda uwepo wa jeshi la Amerika katika eneo hili.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Mujahideen wa Afghanistan hakika wamezika kiburi na fahari ya Bush, Obama, Trump na Biden katika kaburi la himaya, Afghanistan, kupitia jihad, na kulazimisha Amerika kuramba vumbi la kushindwa. Majeshi ya Amerika hayakuweza kuhimili makabila elfu chache ya Waislamu ambao hawana uwezo wa kimsingi wa ulinzi kama vile ulinzi wa anga, wakiwa na silaha ndogo ndogo na hawajapewa mafunzo mazuri. Lakini, bado waliilazimisha Amerika kukimbia, ingawa majeshi vamizi ya NATO ya nchi arubaini na mbili yalikuwa na silaha za kisasa. Kwa hivyo ni sababu gani kwamba uongozi wa jeshi la Pakistan, kutoka Musharraf hadi Bajwa, ambayo inaamuru zaidi ya wanajeshi 600,000 na ina vifaa vya kila aina vya silaha za kisasa, imekuwa ikifanya amali za kijeshi kwa ajili ya Amerika na inabaki kuwa mlinzi wa ALOC na Njia za usambazaji wa GLOC kwa vikosi vya Amerika? Wakati Amerika haijaweza kumaliza upinzani wa Afghanistan, uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan sasa unacheza dori ya msaidizi aliyeajiriwa kwa Amerika kwa njia anuwai, ikiwemo kulazimisha upinzani wa Afghanistan kushiriki katika serikali ya Kabul iliyowekwa na Amerika, huku ikifanya mazungumzo na Amerika kuhamisha muundo wake wa kijeshi kwenda Pakistan. Tutavumilia hadi lini usaliti wa watawala hawa kwa Waislamu? Tutadanganywa hadi lini na ukanushaji wa kirongo wa watawala hawa? Je! Mapenzi yetu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) yanaturuhusu kukabidhi matumizi ya ujasusi wetu na vikosi vya jeshi letu kwa Amerika? Je! Tunawezaje kuwaruhusu watawala hawa kutumia nguvu na rasilimali zetu za kijeshi kulinda maslahi ya Amerika, wakati watawala hao hao wanakataa kirahisi kupeleka jeshi letu kulinda heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na kukomboa Msikiti wa Al-Aqsa, Palestina na Kashmir?

Enyi Waislamu wa Jeshi la Pakistan! Watawala wa Pakistan katika uongozi wa kisiasa na kijeshi hawana ujasiri wa kukataa ombi lolote kuhusiana na nyinyi kutoka Amerika. Rekodi iliyowekwa ya usaliti wao kwa Ummah wetu ni ushahidi wa kutosha wa hilo. Bwana wao katika Ikulu ya White House anawaruhusu kutoa taarifa ambazo zinawapotosha watu wa Pakistan na maafisa wao wa jeshi, ili tu waweze kufanya kila kitu ambacho Amerika inaamuru wafanye. Wanafanya hivyo ingawa Amerika iko vitani na Mwenyezi Mungu (swt) na Waislamu wa Pakistan na kwengineko. Hakika, wao ni vibaraka ambao hawawezi kufikiria kukataa ombi lolote kutoka kwa mabwana wao, au hata kujaribu kufikiria kukataa. Vuteni zulia kutoka chini ya miguu ya watawala hawa wa duni, muipe Nussrah yeni Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itaondoa kwa haraka Fitnah ya Amerika kutoka eneo lot hili. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [وَلَا تَرۡكَنُوۡۤا اِلَى الَّذِيۡنَ ظَلَمُوۡا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُۙ وَمَا لَـكُمۡ مِّنۡ دُوۡنِ اللّٰهِ مِنۡ اَوۡلِيَآءَ ثُمَّ لَا تُنۡصَرُوۡنَ]

“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Surah Hud 11:113]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu