Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  20 Rajab 1444 Na: 1444 / 25
M.  Jumamosi, 11 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir ni Chama cha Kimfumo na Kisiasa ambacho Kinaona kuwa ni Haramu Kubeba Silaha kwa ajili ya Kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Kutafuta Nusrah kwa ajili ya Kusimamisha Tena Khilafah ni Faradhi

(Imetafsiriwa)

Watawala wa Pakistan wametikiswa na kufeli kikamilifu kwa mfumo wa sasa na wito unaokua wa Khilafah. Wakifichua kufilisika kwao wenyewe kimfumo na kisiasa, wanajaribu bila mafanikio kukinasibisha chama cha kimataifa, kimfumo, kisiasa, Hizb ut Tahrir, na ugaidi, kupitia ripoti ya habari katika Gazeti la "Daily Aaj" ('Daily Today') la mnamo tarehe 11 Februari 2023. Je! Watawala hawa hata hawakufikiri kwamba kujaribu kuinasibisha Hizb ut Tahrir na ulipuaji wa Msikiti wa Makaazi ya Polisi wa Kiraia wa Peshawar, itaharibu kile kilichobakia katika hadhi yao? Watawala hawa wanajua kwamba Hizb ut Tahrir ndio harakati kubwa zaidi ya kisiasa duniani, ambayo mfumo wake ni Uislamu. Wanajua kwamba imetabanni mapambano yasiyo ya kijeshi ya Mtume (saw), huko Makka, kwa ajili ya kusimamisha utawala wa Uislamu, tangu kuasisiwa kwake mwaka 1953, hadi leo, miaka sabiini baadaye, 2023.

Kwa miaka sabiini, Hizb imekuwa ikifanya kazi kwa uchangamfu kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah, kupitia mvutano wa kisiasa na kifikra, katika nchi za Kiislamu. Imepita miaka 23, tangu Hizb ut Tahrir ijitahidi pakubwa, kifikra pamoja na kisiasa, nchini Pakistan. Tunaona kuwa ni Haramu kubeba silaha ili kusimamisha tena Khilafah, kutokana na kufuata kwa uthabiti sana Sunnah ya Mtume (saw). Katika kipindi hiki, Hizb imekosoa vikali uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan, kwa utumwa wake wa kisiasa kwa Marekani pamoja na uigaji wake wa kiupofu wa kifikra wa hadhara ya Kimagharibi. Hizb inawataka watawala wa Pakistan wasimamishe hukmu kwa msingi wa Wahyi wa Mwenyezi Mungu (swt). Hizb pia inawakumbusha hasa wenye ikhlasi katika vikosi vya jeshi juu ya jukumu lao, ambalo ni faradhi wa Kishariah ya kusimamisha Khilafah, kupitia kutoa Nusrah yao kwa Hizb ut Tahrir.

Watu wa Pakistan kwa jumla, na watu wake wenye ushawishi hasa, wanatambua uwezo wa wenye ufahamu na elimu ya kutosha wa watetezi wa Khilafah, ambao wanawasilisha Da'wah ya Kiislamu kwa njia ya kukinaisha. Hizb imepata uongozi wa kifikra wa wasomi wenye ufahamu katika miji mikubwa ya Pakistan, huku ikiendeleza shughuli zake za kisiasa. Ni ukweli na ujasiri wa Hizb, kupitia sera yake ya kuinua neno la haki mbele ya watawala dhalimu, ndio umewafanya Mashababu wa Hizb kuwa shabaha ya watawala hawa madhalimu. Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan, Mhandisi Naveed Butt, bado hajulikani aliko baada ya kutekwa nyara takriban miaka kumi na mbili iliyopita. Kwa hiyo, tunawauliza watawala hawa, je, ukatili wenu haujawatosha, mpaka sasa mumeanza kutumia uongo, ili kuzuia mapambano ya kusimamisha tena Khilafah?

Pia tunaiomba timu ya wanahabari ya Daily Aaj kuhakiki habari zozote kabla ya kuzisambaza, kwa mujibu wa amri ya Mwenyezi Mungu (swt). Tufafanua mfumo, fikra, siasa na mbinu zetu kwa njia ya kutoa udhuru. Kwa ajili ya rekodi ya umma, tunakanusha vikali habari zilizochapishwa kwenye gazeti lenu. Hizb ut Tahrir haina uhusiano wowote na Daesh (ISIS) au wanamgambo. Uchapishaji wa habari kama hizo hautaleta tofauti yoyote kwa Hizb. Ni uaminifu wenu tu wa  taaluma ya uandishi wa habari ndio mnaouhujumu. Tafadhali rekebisheni makosa yenu kwa kuchapisha maoni yetu kwenye gazeti lenu. Endapo mwahitaji maelezo zaidi kuhusu Hizb ut Tahrir, mwaweza kuwasiliana nasi, kupitia mojawapo ya akaunti zetu nyingi za mitandao ya kijamii.

Kuporomoka kwa demokrasia, na kufeli kwa mfumo wa sasa na uongozi wa kisiasa na kijeshi, kumeelekeza mazingatio ya Ummah kuelekea kusimamisha tena Khilafah. Tunasisitiza azma na dhamira yetu. Hizb ut Tahrir itaendeleza mapambano yake ya kifikra na kisiasa kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah. Hatujali lawama ya mtuhumu yeyote wa kirongo katika suala hili. Kusimamishwa tena kwa Khilafah kumo ndani ya Ahadi ya Mwenyezi Mungu (swt), ambayo ndani yake Hizb imeweka imani kamili.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

#HakikiDeğişimHilafetle

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu