Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  21 Shawwal 1444 Na: 1444 / 37
M.  Alhamisi, 11 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Sio Kumwasilisha Naveed Butt, Mtetezi wa Khilafah, kwenye Mahakama Yoyote, Hata Baada ya Miaka Kumi na Moja, Wala Kumwachilia Huru, Kunathibitisha Uthabiti wa Naveed Butt, na Batili na Uoga wa Watawala

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 11 Mei 2023, imekuwa ni miaka kumi na moja tangu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Pakistan, Naveed Butt, kutekwa nyara na asasi za serikali. Naveed Butt alitekwa nyara na majambazi wa serikali katika jiji la Lahore, mnamo tarehe 11 Mei 2012, alipokuwa karibu kuregea nyumbani, baada ya kuwachukua watoto wake shuleni. Mlango wa kila mahakama ya Pakistan umegongwa, kwa ajili ya kumpata kwa salama Naveed Butt. Hata Tume ya Uchunguzi juu ya Utoweshwaji kwa Nguvu iliziamuru asasi hizo kumleta Naveed Butt. Hata hivyo, uongozi wa kisiasa na kijeshi haufuati katiba yao iliyoundwa na mwanadamu, wala Shariah ya Mwenyezi Mungu (swt).

Kwani Naveed Butt amefanya nini dhidi ya nchi hii, watu na taasisi ambapo hawezi kufikishwa mbele ya mahakama yoyote? Kwa nini badala yake awekwe kwenye magereza ya siri? Je, Naveed Butt aliua mtu yeyote, au alihusika katika ufisadi, au alikuwa akishirikiana na nchi adui? Hapana! Badala yake, Naveed Butt ni mtoto mtiifu wa Ummah huu na mmoja wa walinzi wake waaminifu. Aliendesha mapambano ya amani ya kisiasa na kifikra kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo peke yake ndiyo itaregesha utukufu uliopotea wa Umma huu. Katika nchi iliyoanzishwa kwa jina la Uislamu, je, mapambano yake ni uhalifu wa kutisha, kwamba Naveed Butt lazima abakie kuwa mwathiriwa wa utekaji nyara na kutoeshwa kwa nguvu?

Je, ni uhalifu wa kutisha kudai kukomeshwa kwa Raj wa Kimarekani nchini Pakistan? Je, ni hatia kufichua mapungufu ya mfumo wa uchumi wa kibepari, na mfumo wa kidemokrasia unaotabikishwa? Je, ni hatia kuwasilisha maelezo ya mfumo wa kiuchumi wa Uislamu, na mifumo yake yote mingine ya maisha? Je, ni hatia kulingania mfumo wa utawala wa Uislamu, Khilafah, ambao unatabikisha Uislamu kivitendo? Je, ni hatia kufikisha Uislamu kupitia makala, taarifa kwa vyombo vya habari, hotuba na mawasilisho, kwa wanahabari, waandishi wa makala, wasomi, wanasiasa na umma kwa jumla wa Pakistani? Je, huu ni msimamo wa kutisha hivi kwamba Naveed Butt ametekwa nyara na kutoweshwa kwa miaka kumi na moja? Je, kweli Naveed hataachiliwa, wala kuwasilishwa mbele ya mahakama yoyote kwa hili?

Leo, mkuu wa jeshi ni mtu anayedai kuwa Hafidh wa Qur’an Tukufu. Mkuu wa jeshi hata anajaribu kuwatia moyo watu kwa kusoma aya za Qur’an Tukufu. Ilhali, wakati wa amri yake, Naveed Butt hajaachiliwa, licha ya kuwa aliendesha mapambano ya kisiasa na kifikra ili kuasisi utawala kwa Qur'an Tukufu na Sunnah za Mtume. Hili linathibitisha kwamba, kama wakuu wote wa jeshi waliopita, bwana wa mkuu wa sasa wa jeshi pia ni Marekani. Marekani daima itasisitiza watumishi wake kufanya kazi ili kuzuia kuenea kwa ulinganisi wa kusimamisha Khilafah nchini Pakistan. Hii ndiyo sababu pia, katika kesi kwamba iwapo Naveed Butt ameuawa kishahidi, uongozi wa sasa hauwezi hata kukusanya ujasiri na adabu kuthibitisha kifo chake.

Hebu marafiki na familia ya Naveed Butt, pamoja na wafuasi wake na watu wanaomtakia mema katika Umma wa Kiislamu, na wawe na uhakika kwamba kufungwa kwa Naveed Butt katika jela za vibaraka, sio hasara kwake. Kufungwa kwake, kuachiliwa huru kwake au kuuawa kishahidi, vyote vinachangia katika mafanikio yake katika Aakhira.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُواْ الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَأْتِكُم مَّثَلُ الَّذِينَ خَلَوْاْ مِن قَبْلِكُم مَّسَّتْهُمُ الْبَأْسَآءُ وَالضَّرَّآءُ وَزُلْزِلُواْ حَتَّى يَقُولَ الرَّسُولُ َالَّذِينَ ءَامَنُواْ مَعَهُ مَتَى نَصْرُ اللَّهِ أَلاَ إِنَّ نَصْرَ اللَّهِ قَرِيب]

“Mnadhani kuwa mtaingia Peponi, bila ya kukujieni kama yaliyo wajia wale walio pita kabla yenu? Iliwapata shida na madhara na wakatikiswa hata Mtume na walio amini pamoja naye wakasema: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu itakuja? Jueni kuwa nusura ya Mwenyezi Mungu ipo karibu!” [Surah Al Baqarah 2:214].

Endapo kipote cha watawala wa Pakistan wanadhani kwamba watasitisha kuwasili kwa Khilafah, kupitia kutoa mfano wa Naveed Butt kwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir, wamekosea. Kusonga mbele kuelekea Khilafah, na kuregesha tena Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, kunasonga mbele kwa nguvu na bidii, bila ya kujali. Ukweli huu unajulikana vyema kwa watawala. Mashababu wa Hizb wameinua neno la haki mbele ya madhalimu katika Ulimwengu mzima wa Kiislamu. Wamekumbatia magereza, wamebeba mateso na kuyafanyia biashara maisha yao kwa radhi za Mwenyezi Mungu (swt). Ukatili wa madhalimu unaimarisha tu azma ya wanaume, ambao hawamuogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt).

Hakika, Naveed Butt, na watoto mashujaa wa Ummah kama yeye, ni mifano ya ujasiri na dhamira kwa ajili yetu sote. Ama Naveed Butt na familia yake watalipwa kwa ajili  ya subira yao kesho Akhera. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[جَنَّـتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا وَمَنْ صَلَحَ مِنْ ءَابَائِهِمْ وَأَزْوَجِهِمْ وَذُرِّيَّاتِهِمْ وَالمَلَـئِكَةُ يَدْخُلُونَ عَلَيْهِمْ مِّن كُلِّ بَابٍ]

“Nayo ni Bustani za milele, wataziingia wao na walio wema miongoni mwa baba zao, na wake zao, na vizazi vyao. Na Malaika wanawaingilia katika kila mlango.” [Surah Ar-Ra’d 13: 23].

Ama watawala wa Pakistan, hata hivyo, ni lazima wajiondolee mzigo wa dhambi kubwa la kutekwa nyara kwa Naveed Butt na wengine wengi. Ni lazima wamuombe Mwenyezi Mungu (swt) msamaha wa madhambi yao. Ni lazima wawaachilie huru mara moja wale watu wote wasio na hatia, ambao "uhalifu" wao si chochote isipokuwa kusema: "Mola wetu ni Mwenyezi Mungu (swt)." Tunawatahadharisha watawala hawa kwa adhabu kali ya Mwenyezi Mungu (swt) kesho Aakhira. Ama kuhusu Dunia hii, tunawatahadharisha juu ya uadilifu wa mahakama za Khilafah, ambazo zitawaadhibu wahalifu walioudhulumu Ummah, hivi karibuni, inshaaAllah.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu