Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  25 Dhu al-Qi'dah 1444 Na: 1444 / 41
M.  Jumatano, 14 Juni 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Khilafah Pekee ndiyo Inayoweza Kutatua Mgogoro Unaoendelea wa Uhaba wa Fedha katika Uchumi wa Pakistan

(Imetafsiriwa)

Serikali za Pakistan mtawalia zimekabiliwa na changamoto ya upungufu wa fedha. Inamaanisha kuwa serikali ina uhaba wa rasilimali za kutumia kwa ajili ya watu. Uhaba huu wa rasilimali unaoikabili serikali ni matokeo ya moja kwa moja ya miundo ya utawala wa kiuchumi inayotekelezwa nchini. Kipote cha watawala wa Pakistan kinatabikisha mtindo wa uchumi wa kirasilimali nchini. Urasilimali husherehekea uhuru wa kumiliki. Unaamini kuwa rasilimali za kiuchumi za nchi lazima ziwe mikononi mwa sekta ya kibinafsi. Unaamini kuwa serikali lazima iwe na uingiliaji mdogo zaidi katika uendeshaji wa uchumi, isipokuwa kuwa kama mdhibiti madhubuti wa sekta ya kibinafsi. Mwelekeo huu kuelekea usimamizi wa uchumi unainyima serikali usimamizi wa moja kwa moja wa rasilimali za nchi. Badala yake, zinamilikiwa na sekta ya kibinafsi. Ili kuzalisha mapato kwa matumizi ya serikali, serikali inategemea kuitoza ushuru sekta ya kibinafsi. Kwa kuongeza, inafadhili nakisi ya kifedha kwa mikopo yenye riba, ambayo inaiweka Pakistan katika mtego wa madeni.

Sekta ya kibinafsi kwa kawaida inauona utozaji ushuru kwa mali yake kama serikali kuchukua kutoka kwa rasilimali zake. Inaona juhudi za utozaji ushuru za serikali kama uwindaji. Mvutano huu unaibua siasa pinzani za utozaji ushuru. Serikali na wale inaotaka kuwatoza ushuru inagongana nao kwa mapato makubwa ya kifedha. Mvutano na shinikizo la kisiasa linalotokana na siasa kama hizo mara nyingi huzuia uwezo wa serikali wa kuzalisha ushuru wa kutosha kukidhi mahitaji yake ya mapato. Serikali basi inaamua kuchukua mikopo yenye riba kutoka kwa taasisi za fedha, masoko ya mitaji na umma kwa jumla. Mikopo yenye riba inaburuza uchumi, haswa inapotumika kufadhili matumizi yasiyo ya maendeleo ya serikali. Wakati malipo ya riba yanapoongezeka, serikali haina njia ya kulipa riba hiyo, isipokuwa kwa kuongeza ushuru na kuchukua deni zaidi la riba. Kwa hivyo, serkali inafungika ndani ya mgogoro mkubwa endelevu wa kifedha. Usimamizi wa uchumi wa ubepari unatupa tatizo la nchi maskini na yenye uhaba wa rasilimali na sekta tajiri ya kibinafsi.

Uislamu una mtazamo tofauti kabisa kuelekea usimamizi wa uchumi. Uislamu hautoi udhibiti mkubwa wa rasilimali muhimu za uchumi kwa sekta  ya kibinafsi. Uislamu unagawanya rasilimali za nchi katika miliki tatu tofauti: miliki ya umma, binafsi na dola. Serikali inasimamia rasilimali chini ya miliki ya umma na dola, huku sekta ya kibinafsi ikidhibiti rasilimali chini ya miliki ya kibinafsi. Uislamu pia unaruhusu serikali kutoza ushuru milki ya kibinafsi. Hata hivyo, unauzuia uwezo wa dola wa kutoza ushuru wa mali ya kibinafsi kwa kumruhusu Khalifa kukusanya ushuru ulioidhinishwa na Shariah kutoka kwa sekta ya kibinafsi pekee. Khalifa hana haki ya kutoza ushuru wowote kwa Ummah, kama Shariah haijatoza ushuru huo. Uislamu unakataza aina zote za ufadhili uliojengwa juu ya riba, kwa dola pamoja na sekta ya kibinafsi. Hakuna miamala inayotegemea riba au zana za kifedha zenye riba zinazoruhusiwa katika Uislamu.

Aidha, katika urasilimali, mtaji na uwekezaji hutengwa katika uchumi kupitia nguvu za soko. Hata hivyo, katika Uislamu, mtaji na uwekezaji huingia katika uchumi kupitia mikataba ya ushirika na dola yenyewe. Hakuna mabenki, masoko ya hisa na masoko ya mitaji katika Uislamu. Hivyo, sekta ya kibinafsi haiwezi kuongeza mtaji kupitia mikopo yenye riba, kutoa hisa kwenye soko la hisa na kutoa bondi kupitia masoko ya mitaji. Hii inafanya kuwa vigumu kwa sekta ya kibinafsi kupata kiasi kikubwa cha mtaji. Hivyo basi, katika uchumi wa Kiislamu viwanda vinavyohitaji mtaji mkubwa kama vile mawasiliano ya simu, usafiri wa anga, utengenezaji wa silaha, saruji na sekta ya mbolea vyote vinafadhiliwa na dola. Dola inafanya uwekezaji katika viwanda vinavyohitaji kiwango kikubwa cha mtaji. Mapato kutoka kwa viwanda kama hivyo yanaingia kwenye hazina ya dola. Kwa hivyo dola katika Uislamu ni tajiri.

Utajiri unaotokana na mali ya umma, kama vile mapato yanayotokana na mauzo ya rasilimali za mafuta, gesi na madini, wote uko katika mamlaka ya dola kuutumia kwa mahitaji ya umma. Dola  inamiliki mapato yanayotokana na viwanda vikubwa vinavyohitaji kiasi kikubwa cha mtaji. Inakusanya ushuru ulioidhinishwa na Shariah kama vile Ushr, Kharaj na Zakah kutoka kwa sekta ya kibinafsi. Mapato ya dola hayapotezwi katika malipo makubwa ya riba, ambayo hufanyika kwa mtindo wa ufadhili wa ubepari. Kwa hivyo dola ina rasilimali nyingi za kutumia kwa watu. Khilafah itatabikisha hukmu za Shariah zinazohusiana na uchumi. Itafungua uwezo mkubwa wa kiuchumi wa ardhi za Waislamu. Itakuwa dola tajiri yenye sekta ya kibinafsi inayotozwa kodi ndogo. Italeta ustawi mpana wa kiuchumi, kama ilivyokuwa hali kihistoria. Utabikishaji wa mfumo wa kiuchumi wa Uislamu ulilifanya Bara Dogo la India kuwa mojawapo ya maeneo tajiri zaidi ya dunia.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu