Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  17 Dhu al-Hijjah 1444 Na: 1444 / 44
M.  Jumatano, 05 Julai 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Utoaji wa Marekani wa Silaha za Kisasa kwa India ili Kukabiliana na China, ni Tishio la Moja kwa moja kwa Usalama wa Pakistan. Je! Uongozi wa Kisiasa na Kijeshi wa Pakistan utaendelea hadi lini Kuamiliana na Marekani kama Mshirika, Wakati ni Adui wa wazi wa Uislamu na Waislamu?

(Imetafsiriwa)

Baada ya mkutano kati ya Joe Biden na Narendra Modi mnamo tarehe 22 Juni 2023, taarifa ya pamoja ilitolewa na Marekani na India, ambayo imezua wasiwasi ndani ya jumuiya ya kimkakati ya Pakistan. Tangazo hili linathibitisha tena ushirikiano wa kina katika mahusiano ya Marekani na India. Linawakilisha hatari ya wazi iliyoko kwa usalama wa Pakistan. Tangazo lenye vipengele 58 lenyewe linakubali kwamba, "Hakuna sehemu ya biashara ya binadamu ambayo haijaguswa na ushirikiano kati ya nchi zetu mbili tukufu, ambazo zinaenea baharini hadi kwenye nyota." Mbali na ushirikiano katika silsila za usambazaji viwandani, na ushirikiano wa majini na usalama kuhusu Indo-Pasifiki, Burma, Pakistan, Taliban na Ukraine, Marekani itaisaidia India kuunda droni na injini za ndege, miongoni mwa teknolojia nyingine za juu za kijeshi.

Ingawa makubaliano haya yanalenga kuongeza uwezo wa kiuchumi na kiulinzi wa India, ili India iweze kukabiliana na China kijeshi na kiuchumi, kuongezeka kwa uwezo wa India pia ni tishio la moja kwa moja kwa Pakistan na Waislamu wa eneo hilo. India inatawaliwa na serikali ya Baniani, serikali yenye chuki dhidi ya Uislamu ambayo imejitolea kutekeleza sera dhidi ya Uislamu. Inaleta uharibifu kwa idadi ya Waislamu ndani ya India na Kashmir Iliyokaliwa kimabavu. Ni kwa sababu ya uadui wake mkubwa dhidi ya Pakistan, kwamba New Delhi iliisisitiza Washington kujumuisha sera za kuipinga Pakistan katika tangazo la Marekani-India.

Ni lazima izingatiwe hapa kwamba Marekani inaweza tu kuishindisha India dhidi ya China, ikiwa India haitapingwa na Pakistan. India lazima ihakikishiwe kuwa Pakistan sio tishio kwa usalama wa India na malengo ya kikanda. Hakika, New Delhi tayari ina uhakikisho thabiti kutoka Islamabad kwamba Jeshi la Pakistan halitachukua hatua za kijeshi juu ya Kashmir. Uongozi wa sasa wa kijeshi na kisiasa wa Pakistan umeelezea hamu yake ya kusawazishwa mahusiano na India. Umelipatia Jeshi la India afueni kupitia makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye Mstari wa Udhibiti. Utabanni zaidi sera ya kujizuia, ukikataa kuchukua hatua za kijeshi juu ya Kashmir Iliyokaliwa kimabavu. Kwa hivyo, uongozi wa Pakistan ndio ulioisahilishia Marekani katika jaribio lake la kupambanisha India na China.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Je, wazee wetu hawakuanzisha nchi katika Bara Hindi Dogo, ambayo kwayo mamlaka yawe kwa Waislamu, ili kuhakikisha usalama wao? Je, hawakuapa kwamba kamwe hawatakubali utawala wa Washirikina wa Kibaniani na utawala wao wa ukafiri? Vipi basi muko tayari kumkubali Raj mkoloni wa Kibaniani katika eneo hili hivi leo? Je, hamushuhudii, kwa macho yenu wenyewe, uovu wa Raj huyu Baniani dhidi ya Uislamu? Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاء مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ]

“Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi.” [Surah Aali-Imran 3:118].

Endapo mtabakia bila kuteteleka kwa vitendo vya watawala wenu, India itainyakua Kashmir kabisa. Watawala hawa watapigia debe usawazishaji mahusiano na India, wakiomba kulazimishwa kwa uchumi, baada ya uchaguzi nchini India mnamo 2024. Watakuwekeni kama walinzi wa uwasilishaji wa nishati, kutoka Asia ya Kati na Iran, hadi India. Hadhara ya kuchukiza wa kishirikina ya Kibaniani, tamaduni na desturi ambazo mababu zetu waliasi dhidi yake, zitalazimishwa juu ya kizazi chetu kichanga, kwenye ardhi yetu.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Mna uwezo wa kupindua mipango ya Marekani kwa eneo hili. Ni lazima mukatae kuwa dola kibaraka ya India. Haupaswi kuruhusu Marekani kumpa adui yenu silaha, dhidi yenu. Ikabilini India, tangazeni sera ya kijeshi kwa ajili ya ukombozi wa Kashmir na muzuie uwasilishaji wa mafuta na gesi kutoka Ardhi ya Waislamu hadi India! Mnajua kwamba uongozi muoga na unaoiunga mkono Marekani hauwezi hata kufikiria kufanya hivyo. Kwa hiyo, wang’oeni watawala hawa. Toeni Nusrah yenu kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Khalifa wa Waislamu ataziunganisha ardhi za Waislamu, kupitia uwezo wenu wa kijeshi. Khilafah itawezeshwa na gesi ya Qatar na Azerbaijan, mafuta ya Iran, Saudi Arabia na Imarati, nguvu za kijeshi za Pakistan, Uturuki na Afghanistan, na utajiri wa kilimo wa Pakistan na Asia ya Kati. Itaondoa mara moja uwepo muovu wa Marekani kutoka kwa ardhi za Waislamu na kuikumbusha Dola ya Kibaniani thamani yake halisi.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Waislamu ndio warithi wa halisi wa Bara Hindi Dogo! Waislamu walitawala eneo hili kwa karne nyingi, licha ya idadi yao ndogo. Nguvu zenu haziko katika wingi wa rasilimali. Nguvu zenu ziko katika Imani yenu kwa Mwenyezi Mungu (swt) na ari ya Jihad katika Njia Yake. Jitokezeni na muwashinde maadui zenu kwa kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَلاَ تَهِنُوا وَلاَ تَحْزَنُوا وَأَنتُمُ الأَعْلَوْنَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ]

“Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini.” [Surah Aali-Imran 3:139].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu