Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  25 Jumada I 1445 Na: 1445 / 24
M.  Jumamosi, 09 Disemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Inachukulia Uanamgambo kwa ajili ya Kusimamisha Dola ya Kiislamu kuwa ni Haramu Kisharia. Hizb ut Tahrir Inadumu katika Kutafuta Nusrah kwa ajili ya Mabadiliko, kwa Mujibu wa Njia ya Mtume ya Mabadiliko!

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir imekariri mara kwa mara kukataa tuhma za uongo za uanamgambo. Licha ya hayo, ndani ya wiki mbili, kwa mara ya pili, habari zilizotokana na vyombo vya usalama zilijitokeza kwenye vyombo vya habari vya uchapishaji na elektroniki, zikidai kwa uongo kwamba Hizb ut Tahrir amejiunga na vikosi vya mashirika ya wanamgambo. Kwa ajili ya rekodi ya umma, kupitia taarifa hii kwa vyombo vya habari, kwa mara nyingine tena tunaeleza msimamo wetu kwamba Hizb ut Tahrir amejifunga katika mvutano wa kifikra na kisiasa kwa mujibu wa Sharia, katika nchi zaidi ya arubaini, kwa zaidi ya miaka sabiini. Kamwe haijainua silaha na haitafanya hivyo kwa sababu inazingatia kuwa ni Haram Kisharia. Hizb haina uhusiano wowote na shirika au kundi lolote la wanamgambo. Haina uhusiano wowote na uanamgambo.

Katika mwendo wake wa kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, Hizb ut Tahrir inafuata imara njia ya Mtume (saw) katika mapambano yake ya kusimamisha Uislamu mamlakani. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alijifunga mjini Makka kwa Da'wah. Hakutumia nguvu yoyote ya kimwili huko. Pindi watu waliompa Bay’ah ya Pili ya Aqabah, Bay’ah ya Nusrah, walitaka ruhusa yake ya kupigana na watu wa Minah, ambao walikuwa ni Washirikina, yeye (saw) alijibu akisema, «لم نؤمر بذلك» "Hatujaamrishwa hilo (kupigana) bado." Mwenyezi Mungu (swt) alimtaka yeye (saw) kuwa mvumilivu dhidi ya madhara na mateso, kama vile Mitume waliotangulia (as) walivyokuwa wavumilivu. Mwenyezi Mungu (swt) alisema,

[وَلَقَدْ كُذِّبَتْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ فَصَبَرُوا عَلَىٰ مَا كُذِّبُوا وَأُوذُوا حَتَّىٰ أَتَاهُمْ نَصْرُنَا]

“Na hakika walikanushwa Mitume wa kabla yako. Nao wakavumilia kule kukanushwa, na kuudhiwa, mpaka ilipo wafikia nusura yetu.” [Surah Al-An’am 6:34].

Kwa rehma ya Mwenyezi Mungu (swt) na Dini yake, Hizb ut Tahrir inajulikana katika Ummah kwa ushujaa wake, msimamo wake wazi na hoja yake ya kushawishi, ya uelezaji. Kwa hivyo, tunawauliza watawala hawa na mashirika ya kijasusi; Sasa kwa kuwa tumeshawasilisha hoja yetu, muna hoja gani ya kuegemea msimamo wenu, mbele ya Mwenyezi Mungu (swt)? Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ]

“Siku ambayo nyuso zitanawiri na nyuso zitasawijika.” [Surah Aal-i-Imran: 106].

Ama kuhusu waandishi wa habari, wanaweza kupata msimamo wetu wa kina kutoka kwa maudhui yaliyopo kwenye akaunti zetu za mitandao ya kijamii na tovuti. Zaidi ya hayo, njia moja rahisi ya kuwasiliana na Hizb ut Tahrir ni kupitia akaunti zetu za mitandao ya kijamii. Waandishi wa habari pia wanaweza kuwasiliana na Mashababu wetu ambao wanawafahamu. Tunavikumbusha vyombo vya habari kwamba watawala hawa ni wale wasiotawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَآ أَنزَلَ اللَّهُ فَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْكَـفِرُونَ]

“Na wasio hukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” [Surah Al-Ma’idah 5:44]. Abdullah Ibn ‘Abbas (ra) amesherehesha, "من جحد ما أنزل الله فقد كفر ومن أقر به ولم يحكم فهو ظالم فاسق" “Yeyote anayepinga yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, basi amekufuru, na yeyote anayeyakubali lakini asihukumu kwayo, yeye ni dhalimu na fasiki (muovu).” [Imesimuliwa na Ibn Jarir]. Hivyo hebu sote na tuzingatie amri ya Mwenyezi Mungu (swt) ili kuthibitisha habari zozote zinazoletwa na Fasiki! Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن جَاءَكُمْ فَاسِقٌ بِنَبَإٍ فَتَبَيَّنُوا أَن تُصِيبُوا قَوْمًا بِجَهَالَةٍ فَتُصْبِحُوا عَلَىٰ مَا فَعَلْتُمْ نَادِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na khabari yoyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kuto jua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda.” [Surah Al-Hujurat, 49:6]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu