Jumanne, 05 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  30 Rabi' I 1446 Na: 1446 / 12
M.  Alhamisi, 03 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Msimamo Dhaifu wa Watawala wa Pakistan kwa Kashmir Inayokaliwa Kimabavu Wampa Ujasiri Mvamizi India

(Imetafsiriwa)

Baada ya kuisalimisha Kashmir Inayokaliwa kimabavu kwa India mnamo Agosti 2019, watawala wa Pakistan wanadumisha msimamo dhaifu. Mnamo 18 Septemba 2024, wakati akitoa maoni yake juu ya uunganishaji kwa nguvu wa India wa Kashmir Inayokaliwa kimabavu, Waziri wa Ulinzi wa Pakistan, Khawaja Asif, alisema, “Msimamo wetu juu ya Kashmir bado haujabadilika, lakini mtazamo wetu lazima uwe wa kidiplomasia. Ulimwengu unaliona kama suala la ndani la India, na lazima tufanye kazi ndani ya mipaka hiyo.” Aidha alionyesha matumaini yake juu ya matokeo ya uchaguzi wa majimbo katika Kashmir Inayokaliwa kimabavu, kana kwamba uchaguzi wa udanganyifu utamlazimisha Modi kufikiria upya ukandamizaji wake! Msimamo dhaifu wa waziri wa ulinzi unathibitisha hatua duni kabisa ya fikra ya kushindwa ndani ya makundi tawala.

Msimamo huo dhaifu wa watawala wa Pakistan unamshajiisha Modi kubadili daima mistari mekundu kuhusu Kashmir. Baada ya kuimarisha ukaliaji wake kimabavu wa sehemu ya Kashmir, India sasa inadai juu ya eneo lililokombolewa. Jeshi la India na uongozi wa kisiasa unaendelea kuitaka Pakistan iondoke Azad (Iliyokombolewa) Kashmir na Gilgit-Baltistan. Mnamo tarehe 28 Septemba 2024, Waziri wa Mambo ya Nje wa India, S. Jaishankar alisema kwa kiburi kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, “Suala lakutatuliwa kati yetu ni kuondoka kwa Pakistan katika eneo na India inalolikalia kwa njia haramu.” Mrengo tawala wa India pia umetishia kuanzisha vita ili ‘kukomboa’ Gilgit-Baltistan. Hii ni pamoja na India kuibua mzozo kuhusu maji, chini ya bendera ya kujadiliwa upya kwa Mkataba wa Maji wa Indus (IWT).

Msimamo dhaifu wa watawala wa Pakistan ni kwa sababu ya ubaraka wao kwa Amerika. Hata kabla ya kuisalimisha Kashmir kwa India mnamo Agosti 2019, watawala wa Pakistan hawakuwa makini kuhusu ukombozi wa Kashmir Inayokaliwa kimabavu. Watawala wa Pakistan walifuata tu sera ya Amerika ya kutoa shinikizo kwa India, ili iingie kwenye kambi ya Amerika. Baada ya India kuingia katika kambi ya Marekani kupitia kundi tawala la Hindutva, watawala wa Pakistan waliachana na Kashmir Inayokaliwa kimabavu ili kuifurahisha Amerika, na kuwadunga kisu mujahidina mgongoni. Tangu wakati huo, watawala wa Pakistan hawapambani na utawala wa India hata kidogo, wakijiwekea kikomo katika kudhibiti upinzani wa ndani kwa msimamo wao dhaifu. Watawala wa Pakistan hawakuchukua hata fursa ya kushambulia India na kuikomboa Kashmir Inayokaliwa kimabavu, wakati China iliposhambulia India huko Ladakh mnamo Mei 2020. Badala yake, kwa utiifu wa kipofu wa maagizo ya Amerika, watawala wa Pakistan waliipa India zawadi ya makubaliano ya kusitisha mapigano mnamo Februari. 2021.

Kwa utiifu kwa Amerika, watawala wa Pakistan wanadumisha msimamo dhaifu wa kuwezesha utawala wa India wa kanda hii. Mpango mkakati wa Amerika ni kuimarisha Dola ya Kibaniani huko Asia Kusini, kama vile inavyoimarisha umbile la Kiyahudi katika Ulimwengu wa Kiarabu. Huku Amerika inashirikiana na watawala wa Waarabu kukandamiza upinzani wowote dhidi ya umbile la Kiyahudi, Amerika inafanya kazi na watawala wa Pakistan kuzuia vikosi vya jeshi na mujahidina kuikomboa Kashmir Inayokaliwa kimabavu. Huku Amerika ikifanya kazi na India kuongeza uwezo wake wa kijeshi, ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa wakala wa usalama wa kitaifa, inafanya kazi na watawala wa Pakistan ili kupunguza nguvu za kiuchumi na kijeshi za Pakistan.

Enyi Maafisa Wanyoofu wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan! Ni wakati wenu sasa wa kuwang'oa vibaraka wa Amerika, wanaounga mkono na kuwaimarisha maadui zetu. Waislamu wa Asia ya Kusini wanangojea kusonga kwenu kwani nyinyi ndio jeshi lenye nguvu zaidi la Waislamu katika kanda hii. Ummah wote unangoja kusonga kwenu kwani nyinyi ndio jeshi lenye nguvu zaidi ndani ya Ulimwengu wa Kiislamu. Mwenyezi Mungu (swt) amekupeni uwezo wa kuupa Ummah wa Muhammad (saw) uhuru kutoka kwa Amerika, kupitia kusimamishwa kwa Khilafah Rashida nchini Pakistan. Ni Khilafah Rashida ndiyo itakayokusanya uwezo tele wa kiuchumi na kijeshi wa Ummah ndani ya dola moja yenye nguvu. Ni Khilafah ndiyo itakayokataa maagizo ya wakoloni na kupindua mipango yao. Ni Khilafah ndiyo itakayokusanya majeshi kwa ajili ya ukombozi wa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Waislamu.

Enyi Maafisa Wanyoofu wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan! Toeni Nusrah yenu kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Mulikeni macho yenu kwenye Jannah na mutembee kwenye njia ya Answaar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao. Answaar walitoa msaada wao wa Nussrah kwa Mtume (saw) kwa ajili ya kusimamisha utawala wa Uislamu, huku macho yao yakiwa yameelekezwa kwenye Pepo ambayo ni pana mithili ya mbingu na ardhi iliyoandaliwa kwa ajili ya watu wema. Kama ilivyoripotiwa na al-Bayhaqi katika “Dala’il al-Nubuwwah” Amir amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliwaambia Answar katika Kiapo cha Pili cha Utiifu cha Aqabah,

«أَسْأَلُكُمْ لِرَبِّي أَنْ تَعْبُدُوهُ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئاً، وَأَسْأَلُكُمْ لِنَفْسِي وَلِأَصْحَابِي أَنْ تُؤْوُونَا وَتَنْصُرُونَا وَتَمْنَعُونَا مِمَّا مَنَعْتُمْ مِنْهُ أَنْفُسَكُمْ»

Ninakuombeni kwa ajili ya Mola wangu Muabuduni na wala msimshirikishe na chochote. Vile vile nakuomba kwa ajili ya nafsi yangu na Maswahaba zangu mutuunge mkono, mutunusuru, na mutulinde na yale munayojihami kwayo.” Wakauliza, “Tutapata nini tukifanya hivi?” Akajibu,

«لَكُمُ الْجَنَّةُ» “Pepo itakuwa yenu.” Wakasema, “Basi hilo ndilo tutakalofanya.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu