Ijumaa, 03 Rajab 1446 | 2025/01/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  5 Jumada I 1446 Na: 1446 / 15
M.  Alhamisi, 07 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Vikundi Tawala vya Pakistan vinamkaribisha Bwana wao Mpya wa Kikoloni, Trump, na Kumhakikishia Utayari wao wa Kutekeleza Maagizo yake

(Imetafsiriwa)

Mithili ya watawala wengine wa Waislamu, Waziri Mkuu wa Pakistan, Shehbaz Sharif, alimpongeza bwana wake mpya, Trump, kwa kutangazwa ushindi wake katika uchaguzi wa rais wa Marekani. Shehbaz Sharif aliandikwa tweet, “Hongera Rais Mteule Donald Trump kwa ushindi wake wa kihistoria kwa muhula wa pili! Ninatazamia kufanya kazi kwa karibu na Utawala unaokuja ili kuimarisha na kupanua zaidi ushirika kati ya Pakistan na Marekani.” Ama kuhusu kiongozi wa upinzani halisi, Imran Khan, pia alimpongeza Trump na kusema, “Rais Mteule Trump atakuwa mzuri kwa uhusiano wa Pakistana na Marekani unaozingatia heshima ya pande hizo mbili kwa demokrasia na haki za binadamu.” Je, vikundi tawala vya Pakistan vinampongeza nani hasa? Ni Trump yule yule aliyesema mnamo tarehe 28 Juni 2024 kwamba Rais Biden anapaswa kuruhusu umbile la Kiyahudi “limalize kazi.” Hata hivyo, vikundi tawala vya Pakistan vinashughulika na kila mmoja kumpiku mwezake ili kupata fursa ya kufanya kazi na wakoloni.

Je, ni vikundi tawala vya Pakistan viko tayari kufanya kazi na nani, haswa? Ni Trump ambaye kwa amri yake uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan uliisalimisha Kashmir Iliyokaliwa kimabavu kwa Modi mnamo Agosti 2019. Ni Trump ambaye alibwaga “Mama wa Mabomu Yote” nchini Afghanistan. Ni Trump ambaye kwa amri yake uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan ulifanikisha mpango huo kuhusu Afghanistan nchini Qatar, ili jeshi lake oga liweze kuokolewa kutokana na kushindwa kwa kufedheheshwa, mikononi mwa mujahidina. Trump ndiye aliyewashambulia kwa mabomu Waislamu nchini Yemen, Syria, Iraq. Sasa kwa hivyo, ni maslahi gani mengine ya wakoloni ambayo vikundi tawala vya Pakistan viko tayari kuyawezesha kwa Trump?

Wanademokrat na Wanarepublican nchini Amerika wameungana katika sera zao kuu. Wanademokrat wanavaa vazi la unafiki wa kisiasa. Wanamakinisha utawala wa Marekani kwa nguvu kote duniani, huku wakizungumza kuhusu haki za binadamu na demokrasia. Ama kwa wanaRepublican, pia wanamakinisha utawala wa Amerika, lakini kwa mtindo wa nguvu ya kikatili. Bila shaka, Waislamu wamefurahishwa na kushindwa kwa Wanademokrat, ambao utawala wao unalipatia umbile la Kiyahudi fedha na silaha linazohitaji ili kuendeleza mauaji ya halaiki mjini Gaza na Palestina. Walakini, Trump pia anatangaza wazi kumuunga mkono Netanyahu. Basi vipi kunaweza kuwa na furaha yoyote kwa Waislamu katika hili? Mabadiliko pekee ni kwamba usimamizi wa Marekani wa kuchinja Waislamu utajitokeza kwa uwazi zaidi hivi sasa.

Nguvu ya Ummah haitatokana na mabadiliko ya siasa za ndani za dola kandamizi za kikoloni. Itatokana na kung'olewa kwa watawala vibaraka katika miji mikuu ya Waislamu. Ni wakati sasa wa kuanzishwa kwa mapinduzi ya Khilafah Rashida kwenye magofu ya tawala hizi za vibaraka. Kwa nini basi mabadiliko hayo bado hayajatokea jijini Islamabad, Enyi maafisa na askari wa Jeshi la Pakistani?! Je, hadi lini tutaendelea kuelekeza masuala yetu, kama vile Kashmir, Palestina, Burma, Turkestan Mashariki (Xinjiang), Syria, Iraq au Sudan kwa dola za Magharibi na taasisi za kikoloni za kimataifa, pamoja na siasa zao za udanganyifu? Hadi lini, wakati tuna mamilioni ya wanajeshi wanaotamani kuuawa shahidi, na idadi kubwa ya ndege za kivita, vifaru, manuari, nyambizi, makombora ya balestiki na ya masafa? Chukueni mambo mikononi mwenu, enyi wana wa Muhammad bin Qasim. Hivyo, enyi maafisa wa Jeshi la Pakistani! Jitokezeni na mtoe Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida. Mtume (saw) amesema, «إِنَّمَا الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Imam (Khalifa) ni ngao kwa Waislamu. Wanapigana nyuma yake na wanalindwa naye.” [Muslim]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu