Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  5 Rabi' II 1446 Na: 1446 / 13
M.  Jumanne, 08 Oktoba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Imepita Mwaka Mmoja Tangu Mauaji ya Halaiki mjini Gaza Yaanze! Umma wa Kiislamu na Majeshi Yake Lazima Usimamisha Tena Khilafah Rashida na Kuikomboa Palestina

(Imetafsiriwa)

Hakuna idadi ya Makongamano Yote ya Vyama na Siku za Mshikamano itabadilisha chochote kwa Waislamu wa Palestina. Kwa muda wa mwaka mzima, makundi tawala ya sasa ya Pakistan yameshindwa katika uwajibikaji wao kuelekea Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Waislamu wa Palestina hawahitaji mshikamano pekee. Wanahitaji kuhamasishwa kwa majeshi ya Waislamu. Pakistan ina jeshi la saba kwa ukubwa duniani, na jeshi lenye nguvu kubwa zaidi katika Ulimwengu wa Kiislamu. Ina Waislamu wanaopenda Uislamu na Umma wa Kiislamu. Hata hivyo, Pakistan haina uongozi wa dhati unaotawala kwa Qur'an Tukufu na Sunnah ya Mtume. Badala yake ina watawala wanaochukua misimamo kwa misingi ya fikra za mabwana zao, wakoloni. Hakuna matumaini yaliyosalia kwa watawala wa sasa wa Waislamu. Watawala wa Pakistan wanalitazama shambulizi la ardhi ya Israa’ na Miraj kutokana na mtazamo wa utaifa, na wanazitaka dola za Magharibi kutatua masuala hayo. Watawala hawa wanafuata Taghut (mamlaka yasiyo ya Kiislamu) kwa manufaa ya dunia ya muda mfupi. Wamepuuza amri za Mwenyezi Mungu (swt) zilizoteremshwa kuhusu maadui wa Waislamu na Uislamu kwa muda wa mwaka mzima.

Enyi Waislamu wa Pakistan! Ni faradhi kwa majeshi yote ya Waislamu, karibu na Palestina na mbali nayo, kukusanyika. Mwenyezi Mungu (swt) ameamrisha,

[وَاَخۡرِجُوۡهُمۡ مِّنۡ حَيۡثُ اَخۡرَجُوۡكُمۡ‌ وَالۡفِتۡنَةُ اَشَدُّ مِنَ الۡقَتۡلِۚ]

“Na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa.” [Surah Al-Baqarah: 191]. Mwanachuoni mashuhuri wa Hanifi, Ibn Abidin ash-Shami, mwandishi wa kitabu cha Hanifi “Radd al-Muhtar 'ala al-Durr al-Mukhtar” ametangaza katika maelezo (sherh) yake ya Hashiya katika Kitabu cha Jihad, وَفَرْضُ عَيْنٍ إنْ هَجَمُوا عَلَى ثَغْرٍ مِنْ ثُغُورِ الْإِسْلَامِ، فَيَصِيرُ فَرْضَ عَيْنٍ عَلَى مَنْ قَرُبَ مِنْهُمْ... فَأَمَّا مَنْ وَرَاءَهُمْ بِبُعْدٍ مِنْ الْعَدُوِّ فَهُوَ فَرْضُ كِفَايَةٍ عَلَيْهِمْ ، حَتَّى يَسَعُهُمْ تَرْكُهُ إذَا لَمْ يُحْتَجْ إلَيْهِمْ، فَإِنْ اُحْتِيجَ إلَيْهِمْ بِأَنْ عَجَزَ مَنْ كَانَ يَقْرُبُ مِنْ الْعَدُوِّ عَنْ الْمُقَاوَمَةِ مَعَ الْعَدُوِّ أَوْ لَمْ يَعْجِزُوا عَنْهَا لَكِنَّهُمْ تَكَاسَلُوا وَلَمْ يُجَاهِدُوا فَإِنَّهُ يُفْتَرَضُ عَلَى مَنْ يَلِيهِمْ فَرْضَ عَيْنٍ كَالصَّلَاةِ وَالصَّوْمِ ، لَا يَسَعُهُمْ تَرْكُهُ ثُمَّ وَثُمَّ إلَى أَنْ يُفْتَرَضَ عَلَى جَمِيعِ أَهْلِ الْإِسْلَامِ شَرْقًا وَغَرْبًا عَلَى هَذَا التَّدْرِيجِ “Nayo (Jihad) ni faradhi ya lazima (fardh 'ayn) ikiwa watashambulia ardhi ya Uislamu. Kisha inakuwa ni faradhi ya mtu binafsi kwa walio karibu nao... Ama wale walio mbali zaidi na adui, ni faradhi ya jumuiya, ya pamoja (fard kifayah) juu yao, maadamu wanaweza kumudu kuiache, isipokuwa wakihitajika. Ikiwa watahitajika kwa sababu wale walio karibu zaidi na adui hawawezi kumzuia, au ikiwa wanaweza kumzuia lakini wameghafilika na hawakupigana, basi ni wajibu kwa wale walio karibu nao kama faradhi ya mtu binafsi mithili ya swala na Sawm (kufunga). Hawawezi kuipuuza. Hili linaendelea mpaka linakuwa ni faradhi kwa watu Waislamu wote, mashariki na magharibi, kwa namna hii ya utaratibu.” Basi musimwache afisa hata mmoja miongoni mwa jamaa na marafiki zenu, bila ya kumhimiza atimize wajibu wake.

Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Mumeshuhudia kupuuza kwa watawala na makamanda wa kijeshi wa Waislamu kwa mwaka mmoja sasa. Wanakuiteni kwenye utaifa, kiasi kwamba mumepuuza faradhi yenu kwa mwaka mzima. Nyinyi ni Waislamu na Uislamu ni Dini yenu. Wajibu wenu mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) haukufungika kwenye mipaka ya kitaifa. Uislamu haukubali fikra kwamba adui akiishambulia Islamabad, munajibu kwa nguvu, lakini adui akiishambulia Al-Masjid Al-Aqsa, si jukumu lenu kujibu. Uislamu haukubali fikra kwamba adui akiikalia kimabavu Lahore, mutamfukuza adui kwa gharama yoyote ile, lakini adui akiikalia kimabavu Al-Quds, si jukumu lenu kumfukuza. Uislamu haukubali kwamba munawajibika kuilinda ardhi ya Pakistan, lakini sio kuilinda Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina.

Enyi Maafisa wa Jeshi la Pakistan! Fahamu ya utaifa ni ukiukaji wa wazi wa Quran Tukufu na Sunnah ya Mtume. Ummah ni Ummah mmoja na udugu mmoja. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّمَا الْمُؤْمِنُوْنَ إِخْوَۃٌ] “Hakika Waumini ni ndugu.” [Surah Al-Hujurat: 10]. Waumini ni Ummah mmoja mbali na watu wengine wote. Imepokewa na Al-Bayhaqi katika Al-Sunan Al-Kubra kwamba Mtume Muhammad (saw) amesema, «أَنَّهُمْ أُمَّةٌ وَاحِدَةٌ دُونَ النَّاسِ» “Hakika wao ni Ummah mmoja, tofauti na watu wengine wote.” Hairuhusiwi kwa Waislamu kugawanywa katika dola za kitaifa, na Uislamu unawajibisha dola moja na Khalifa mmoja. Ibn Ishaq anasimulia kwamba Abu Bakr as-Siddique (ra) amesema, وَإِنَّهُ لَا يَحِلُّ أَنْ يَكُونَ لِلْمُسْلِمِينَ أَمِيرَانِ “Hakika hairuhusiwi kwa Waislamu kuwa na Amiri wawili.” Uislamu unawajibisha Imarah moja kwa Waislamu wote duniani, na amiri mmoja anayetawala kwa Uislamu. Katika “Sunan” yake, ad-Darimi amepokea kutoka kwa Umar al-Farooq (ra) ambaye amesema,  إِنَّهُ لَا إِسْلَامَ إِلَّا بِجَمَاعَةٍ، وَلَا جَمَاعَةَ إِلَّا بِإِمَارَةٍ، وَلَا إِمَارَةَ إِلَّا بِطَاعَةٍ “Hakuna Uislamu, bila ya umma mmoja, na hakuna umma, bila ya Imarah moja, na hakuna Imarah bila ya utiifu.” Vunjeni sanamu ya utaifa, na mumuondoe mtawala au kamanda yeyote ambaye anakuwa kizuizi kwa faradhi yenu. Ipeni Nusrah yenu Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itakuhamasisheni mara moja kuzikomboa ardhi zilizokaliwa kwa mabavu za Waislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu