Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  13 Jumada II 1446 Na: 1446 / 20
M.  Jumapili, 15 Disemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir Inalingania Ukombozi wa Ardhi za Waislamu kutokana na Ukoloni

(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir imekuwa mada ya mjadala wa kijamii ndani ya duara zenye ushawishi za Pakistan. Mjadala huo unajumuisha kama tiba za Shariah kwa matatizo ambayo Hizb ut Tahrir inayawasilisha zinapaswa kutekelezwa ili kuepuka matatizo mengi ambayo Pakistan inakabiliana nayo. Kuna mjadala mkali kuhusu Hizb ut Tahrir yenyewe, ikiwemo kupigwa marufuku kwake nchini Pakistan na msimamo mkali dhidi yake katika suala la mateso, unyanyasaji na kifungo. Kwa maslahi ya mjadala wenye tija, mambo yafuatayo ni ya kuzingatiwa na wenye ushawishi kwa jumla na watunga sera, waandishi wa habari, mashirika ya haki za binadamu na ndugu wanasheria hasa.

Kwanza: Hizb ut Tahrir (Chama cha Ukombozi) kinalingania ukombozi (tahrir) wa ardhi za Waislamu kutokana na ukoloni. Neno ‘tahrir’ kwa Kiarabu linamaanisha ukombozi au ukombozi kutoka kwa utumwa. Hizb ut Tahrir inalingania kukombolewa (tahrir) kwa Ardhi za Waislamu kutoka kwa fikra, mifumo na hukmu za wakoloni, na pia kukombolewa kutoka kwa utawala na ushawishi wa dola za kikoloni.

Hizb inafanya kazi kwa ajili ya ukombozi na mwamko wa Waislamu ni kwa kupitia kuwainua Waislamu kifikra. Hii ni kwa kuzalisha fikra na fahamu sahihi za Uislamu ndani ya Waislamu. Kwa hivyo, Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa, ambacho mfumo wake ni Uislamu. Hizb ut Tahrir ilianzishwa kwa kuitikia aya ifuatayo ya Quran Tukufu,

[وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ]

“Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa.” [Surah Aali Imran 3:104]. Basi kwa nini Hizb ut Tahrir isiruhusiwe kulingania kukombolewa ardhi za Waislamu kutokana na ukoloni?

Pili, Hizb ut Tahrir inapinga ukoloni wa kiuchumi wa ardhi za Waislamu. Hizb inasisitiza kuwa njia ya kuchukua mikopo ya nje kwa ajili ya ufadhili ni hatari kwa nchi yoyote. Hapo awali, mikopo ilikuwa njia ya ukoloni wa moja kwa moja kwa nchi. Leo, mikopo ni njia kuu ya kupanua ushawishi na utawala juu ya nchi. Mikopo hii ni ya riba, yenye kuiingiza nchi katika mtego mkubwa wa madeni. Kisha taasisi za kifedha za kikoloni, kama vile Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, zinaweka masharti ambayo yanazidisha hali ya uchumi kuwa mbaya. Masharti yanaruhusu makampuni ya kigeni kunyonya malighafi na kutawala masoko ya ndani na bidhaa zao za thamani kubwa. Masharti hayo yanazuia viwanda kuzalisha bidhaa zenye thamani ya chini kwa masoko ya nje. Masharti hayo yanalazimisha ubinafsishaji wa viwanda vya serikali na mali ya umma kama mafuta na umeme, na kuinyima hazina ya dola fedha.

Mashirika kama vile Mfuko wa Fedha wa Kimataifa ni zana mikononi mwa dola kubwa, hasa Marekani, ambazo zinawanyonya ili kufikia maslahi yao binafsi. Wao ni njia ya kuzalisha ushawishi wa wakoloni juu ya Waislamu na ardhi zao. Hili haliruhusiwi kwa mujibu wa Shariah, kwa sababu kanuni ya Shariah inasema الوَسِيْلَةُ إِلَى الحَرَامِ مُحَرَّمَةٌ “njia ya kupelekea kwenye kilichoharamishwa ni haramu.” Hizb ut Tahrir inalingania kutabikishwa hukmu za Shariah ya Kiislamu kuhusu uchumi ili kukomesha ukoloni wa kiuchumi. Basi kwa nini Hizb ut Tahrir isiruhusiwe kulingania kukomesha ukoloni wa kiuchumi katika ardhi za Waislamu?

Tatu, Hizb ut Tahrir inapinga ukoloni wa kijeshi wa ardhi za Waislamu. Hizb inasisitiza kwamba hairuhusiwi kufanya makubaliano ya kijeshi na nchi za kikoloni, kama vile makubaliano ya ulinzi wa pande zote, makubaliano ya usalama wa pande zote, na uwezeshaji wowote wa kijeshi unaohusiana na hilo, kama vile kukodisha kambi za kijeshi, viwanja vya ndege, au bandari. Pia hairuhusiwi kuomba msaada (isti’aanah) kutoka kwa dola za kikoloni, na majeshi yao.

Hizb ut Tahrir inapinga kisiasa ukoloni wa kijeshi kwa msingi wa Uislamu. Mtume (saw) amewakataza Waislamu kutafuta msaada (isti ́aanah) kutoka kwa dola za kikafiri, kwa kuwa amekataza kutafuta nuru kutoka kwenye moto wa washirikina, kama alivyosema, «لاَ تَسْـتَضِـيئُوا بـِنَارِ الْمُشْرِكِينَ» “Musitafute nuru kutoka kwa moto wa washirikina.” [Imepokewa na Ahmad]. Moto ni kinaya cha vita. Mtume (saw) pia amesema:

«فَإِنَّا لاَ نَسْـتَعِينُ بـِمُـشْـرِكٍ»

“Sisi hatuombi msaada kutoka kwa mshirikina.” [Sahih Ibn Hibban]. Basi kwa nini Hizb ut Tahrir isiruhusiwe kulingania kukomesha ukoloni wa kijeshi katika ardhi za Waislamu?

Nne, Hizb ut Tahrir inapinga ukoloni wa kisiasa wa ardhi za Waislamu. Baada ya kuvunjwa Khilafah mikononi mwa dola za kikoloni, ardhi za Waislamu ziligawanywa katika dola ndogo zaidi ya hamsini, kama sehemu ya sera ya kugawanya na kutawala. Hizb inasisitiza kuwa Waislamu ni Ummah mmoja tofauti na watu wengine. Ni faradhi kwamba Waislamu wawe kama kitengo kimoja, katika dola moja, kama umbo moja. Ni faradhi kwamba kazi ifanywe kwa ajili ya kuziunganisha ardhi zote za Waislamu ndani ya dola moja chini ya dola ya Khilafah.

Hizb ut Tahrir inalingania muungano wa kisiasa wa ardhi za Waislamu kwa msingi wa Uislamu. Imeelezwa katika Quran Tukufu,

[وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا]

“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Surah Aali Imran 3: 103]. Mtume (saw) amesema,

«يَا أَيُّها النَّاسُ أَلا إِنَّ رَبَّكُمْ وَاحِدٌ، وَإِنَّ أَباكُمْ وَاحِدٌ، أَلا لا فَضْلَ لِعَرَبِيٍّ على عَجَمِيٍّ، وَلا لِعَجَمِيٍّ عَلَى عَرَبِيٍّ، وَلَا أَحْمَرَ عَلَى أَسْوَدَ، ولا أَسْوَدَ على أَحْمَرَ، إِلَّا بِالتَّقْوَى»

“Enyi watu, hakika Mola wenu ni Mmoja, na baba yenu wa mwanzo ni mmoja. Hakika Mwarabu hakuna ubora kwa Mwarabu juu ya asiyekuwa Mwarabu, wala asiye Mwarabu juu ya Mwarabu, wala mweupe juu ya mweusi, wala mweusi juu ya mweupe, isipokuwa kwa uchamungu.” [Ahmad]. Basi kwa nini Hizb ut-Tahrir isiruhusiwe kulingania muungano wa kisiasa wa ardhi za Waislamu?

Tano, Hizb ut Tahrir inapinga ukoloni wa kithaqafa wa ardhi za Waislamu. Baada ya kuvunjwa Khilafah, wakoloni walitengeneza mitaala na silabasi za elimu kwa mtazamo wa mfumo wao, urasilimali. Ni mfumo wa kutenganisha dini na dola, na kutenganisha dini na maisha, kama ilivyoandikwa “Mpeni Kaisari kilicho cha Kaisari, na Mungu kilicho cha Mungu.” Kwa kuzingatia hilo, mwanadamu ndiye anayejiwekea mfumo wake wa maisha.

Kupinga kwa Hizb ut Tahrir ukoloni wa kithaqafa wa ardhi za Waislamu kunatokana na mtazamo wa Uislamu. Katika Uislamu, Mwenyezi Mungu (swt) ndiye Mtungaji Sheria na Yeye pekee ndiye aliyeweka mfumo kwa ajili ya wanadamu, na akaifanya dola kuwa sehemu ya hukmu za Shariah za Uislamu. Katika Shariah, Muislamu anatakiwa kufanya vitendo vyote kwa mujibu wa hukmu za Shariah. Quran Tukufu inasema,

[فَلاَ وَرَبِّكَ لاَ يُؤْمِنُونَ حَتَّى يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ]

“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana.” [Surah An-Nisaa 4:65]. Basi kwa nini Hizb ut-Tahrir isiruhusiwe kulingania kukomesha ukoloni wa kithaqafa katika ardhi za Waislamu?

Kwa kumalizia, Hizb ut Tahrir ni chama cha kisiasa ambacho mfumo wake ni Uislamu. Inaifunga kazi yake kwenye matendo ya kisiasa na kifikra, kwa kuzingatia njia ambayo Mtume (saw) alibeba Dawah mjini Makka. Misimamo yake yote ya kisiasa na kifikra iko juu ya msingi wa Uislamu. Inafanya kazi ya kukomesha aina zote za ukoloni katika ardhi za Waislamu. Inafanya kazi kwa ajili ya kuunganisha ardhi za Waislamu chini ya mfumo wa utawala wa Kiislamu, Khilafah. Kwa maslahi ya mjadala wenye ikhlasi na wenye natija, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan inatoa mwaliko wa dhati kwa yeyote ambaye angependa taarifa zaidi kuhusu Hizb ut Tahrir.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu