Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 16 Jumada II 1446 | Na: 1446 / 21 |
M. Jumatano, 18 Disemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mapinduzi katika Ulimwengu wa Kiislamu Yatapelekea kwenye Mabadiliko ya Kweli Pale tu Watu wenye Nguvu Watakapotimiza Wajibu wao wa Shariah kwa Kuwaondoa Madhalimu na kuupa Nusra Ummah
(Imetafsiriwa)
Baada ya mabadiliko makubwa katika utawala wa Syria, baada ya mabadiliko ya utawala nchini Bangladesh na Afghanistan, pamoja na mabadiliko ya utawala yaliyokuja kabla ya haya, makundi tawala yanaendeleza simulizi ya zamani kwamba mapambano yaliyopangwa ya watu dhidi ya watawala yanazua “machafuko, ufisadi na ukosefu wa utulivu.” Iwe ni mkuu wa Jeshi la Pakistan, Jenerali Asim Munir, au watawala wengine, wote wanadai kwamba hawataruhusu nchi zao kuwa “Libya, Syria, Iraq au Sudan” nyengine. Ili kuzungumzia simulizi hii, tunawasilisha nukta tatu zifuatazo:
Kwanza: Kiasili, kwa maumbile yake, dola ni dhihirisho la fikra, hisia na matamanio ya watu. Dola, kimaumbile iliyo tulivu hupanga mambo ya watu kupitia hukmu, maadili na mfumo ambayo watu wanayaamini. Kwa hiyo, Umma na dola yake lazima iwe juu ya msingi huo huo. Dola lazima iwe na msingi wa Shariah ya Kiislamu, iliyokombolewa kutoka kwa ushawishi na utawala wa mifumo, vibaraka na hadhara ya mkoloni kafiri Magharibi. Dola yoyote isiyokuwa hii itachukuliwa kuwa isiyo ya kimaumbile, ya muda, isiyo na utulivu na utawala wa dhulma. Kwa hakika, hakuna hata moja ya dola zaidi ya hamsini za Waislamu ambayo ni dola ya kimaumbile, tulivu. Ndiyo maana, kwa kuongezeka mwamko wa Kiislamu, pengo kati ya dola na raia limefikia kiwango ambacho hakiwezekani kuzibwa. Ndiyo maana, punde au baadaye, mapinduzi hayaepukiki, ambayo hakuna Mubarak, Ben Ali, Hasina, Bashar, Bin Salman au jenerali anayeweza kuyazuia!
Pili: Kumhisabu (muhaasabah) mtawala ni faradhi ya Shariah na hatajio la wakati kwa Ummah. Hivyo basi, kupaza sauti zao dhidi ya dhulma, watawala dhalimu na sera za kikoloni zinazotekelezwa na watawala vibaraka si “machafuko na ufisadi,” wala hakuna sababu ya kufasiri hili kuwa ni “kutokuwa na utulivu.” Hata hivyo, muhaasabah huu lazima uegemezwe tu juu ya msingi wa maamrisho (awaamir) na makatazo (nawaahi) ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw). Inasababisha kuondolewa kwa mfumo na watawala wa sasa, na kurudi kwa Khilafah Rashida mahali pao. Ni kundi tawala ambalo linahakikisha utumwa wa mfumo wa kimataifa kwa kugeuza chuki ya raia kwa mfumo wa sasa kuelekea mtu binafsi, kama vile Musharraf, Zardari, Nawaz, Mubarak, Bashar, Gaddafi au Ben Ali. Kwa hiyo, kwa kubadilisha sura ya mtawala, makundi yanayotawala yanajaribu kutuliza hasira za Ummah. Mabadiliko ya nyuso hufanyika chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa mabwana wa Kimagharibi. Matokeo yake, watu wanainuka dhidi ya watawala wapya baada ya muda mchache, na kuendeleza mzunguko huo mbaya.
Tatu: Iwe ni Libya, Sudan, Yemen au Iraq, sababu ya machafuko yanayoendelea katika Ulimwengu wa Kiislamu ni kufeli kwa watu wenye nguvu, na sio raia. Badala ya kuegemea upande wa Umma katika kuangusha muundo wa dola ya kitaifa wa kikoloni, mfumo wa kiliberali wa Kimagharibi na watawala vibaraka, ili kuhakikisha uchungaji wa mambo ya Ummah kwa mujibu wa Qur'an Tukufu na Sunnah za Mtume (saw). watu wenye nguvu wanachukua upande wa watawala madhalimu, au wamakaa kimya. Kutokuchukua hatua huku kumewapa watawala vibaraka uhuru wa kuwakandamiza watu, kuwanyonga. Kutokuchukua hatua huku ndiko kulikosababisha machafuko. Lau majeshi yangeegemea upande wa Umma, badala ya kuwaunga mkono madhalimu, kuwang'oa watawala na kuurudisha Uislamu kwenye utawala, kusingetokea machafuko yoyote. Kupitia nguvu huja majukumu. Jukumu lililoambatanishwa na nguvu ya Nusrah ni kuitumia kwa ajili ya Uislamu na Waislamu. Hata hivyo, Ummah umeendelea kutoa kafara kila kitu, ukitoa maisha yao, mali zao, huku wanajeshi wakitazama tu tamasha hilo, wakikwepa jukumu lao, na kusukuma simulizi ya watawala. Ummah daima umekuwa tayari kwa ajili ya kujitolea. Ni udhaifu wa watu wenye nguvu ambao umesababisha kuuawa shahidi kwa mamilioni ya Waislamu.
Kwa hivyo, yeyote miongoni mwa vikosi vya jeshi anayetaka kuziokoa nchi za Waislamu kutokana na machafuko na kuleta mabadiliko ya kweli lazima atoe Nusrah kwa Hizb ut Tahrir. Ndiyo njia pekee ya mabadiliko ya kina yanayoweza kuletwa bila machafuko yoyote, umwagaji damu, na ugomvi, kama vile uazishwaji wa dola mjini Madina. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ» “Kisha utakuwepo utawala wa kutenza nguvu, na utakuwepo muda anaotaka Mwenyezi Mungu uwepo, kisha Mwenyezi Mungu atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwa Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha (saw) akanyamaza.” (Musnad Ahmad)
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: +(92)333-561-3813 http://www.hizb-pakistan.com/ |
Fax: +(92)21-520-6479 E-Mail: htmediapak@gmail.com |