Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  16 Dhu al-Hijjah 1443 Na: BN/S 1443 / 20
M.  Ijumaa, 15 Julai 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

            Mamlaka ya Palestina Yavuruga Sheria na Kupoteza Haki na Malalamishi Mahakamani
(Imetafsiriwa)

Chama cha Wanasheria kilitangaza mgomo wake mnamo Jumatano na Alhamisi na kukaa mbele ya Kiwanja cha Mahakama huko Ramallah, kukiwa na uwezekano wa kuongezeka kwa hatua za kukataa kuanzishwa kutumika kwa marekebisho ya kile kinachoitwa "utekelezaji, na msingi wa mashtaka ya kiraia na kibiashara na taratibu za adhabu” sheria zilizotolewa na rais wa Mamlaka ya Palestina kupitia “maamuzi ya sheria” mwezi Machi uliopita. Mamlaka ya Palestina (PA) haikukubali hatua zozote za kuifanyia marekebisho, huku polisi wa Palestina wakifunga eneo la jengo la mahakama mnamo Jumatano, kwa kutarajia kuketi kwa mawakili waliotangaza kwamba watakaa mahali hapo kama sehemu ya kupinga maamuzi hayo.

Kukaa huku kwa wanasheria kunajiri, wao wakiwa ndio kundi linalowakilisha watu katika kesi za haki, malalamishi na migogoro mbele ya mahakama, kama jibu kwa kile PA inachokifanya katika suala la kupitishwa kwa sheria zisizo za haki ambazo zinanyima haki. Na wao ndio waliokuwa wamechukua hatua za kupinga hapo awali kujibu ubabe na uvurugaji katika kipengele cha mahakama, wakati PA ilipotaka - na ingali inataka - kuifanya idara ya mahakama kuwa chombo cha kuwalinda wahalifu wakuu na kifiniko cha uhalifu wao dhidi ya watu wa Palestina, kama vile kuunda Baraza Kuu la Mpito la Idara ya Mahakama, na uteuzi wa rais wake, ambaye alipewa mamlaka ya kurekebisha sheria na kujiteua tena, na vile vile kupitia kile kinachoitwa "maamuzi ya sheria" ambayo sasa yanatolewa na PA au vyama vyao vikuu vyenye ushawishi.

Haya "maamuzi ya sheria" kusema kwa uchache, yalikuja na marekebisho, ambayo yanachanganya na kupoteza haki za watu badala ya kuzidumisha. Wanachochea migogoro kati yao badala ya kusuluhisha, na wamefungua mianya kadhaa ya kuwalinda wahalifu kupitia kile ambacho sheria hizi mpya zinaruhusu kutokana na uwezekano wa kufuta kesi. Walitoa kibali kwa mamlaka kuongeza muda wa kukaa mahabusu bila kufikishwa mahakamani, yaani walitoa kifiniko kwa vyombo vya ulinzi na usalama kumkamata wamtakaye bila kujali sheria inataka nini katika suala la kuwalinda watu binafsi na sio kuwaweka kizuizini isipokuwa kwa uamuzi wa mahakama. Na mambo mengine yanayotajwa na mawakili katika maandamano yao, kama vile kumpa mwendesha mashtaka kazi ya kuleta mashahidi, taarifa za kielektroniki za kesi au kwa njia ya simu. Pamoja na kusimamisha utekelezaji wa malipo ya kifedha kwa hundi na stakabadhi za malipo kwa madai ya ghushi na kumpa mwendesha mashitaka kuthibitisha uhalali wake, na ada kubwa kwa kutumia vibaya hitaji la watu kufungua kesi na hatua za kisheria kwa madhumuni ya kodi na kadhalika.

Sheria mpya zilizotajwa hapo juu zimeanza kutumika na zitawasukuma watu kwenye machafuko na mapigano kwa sababu hawatapata haki na sheria zinazolinda haki zao. Marekebisho haya yatavunja imani kati ya watu katika miamala yao ya kifedha, na yatawasukuma kuamiliana kupitia benki zenye riba, na wanufaika wa marekebisho haya watakuwa sekta ya benki na mabepari wakubwa wasiojali Halali wala Haramu, na matokeo yake yatakuwa ni kuitumbukiza jamii katika lindi la madeni ambayo kwayo watu watavuna tu vita na Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw), na kuweka rehani mali zao kwenye benki.

Kwa hivyo, PA inaendelea kuharibu na kufisidi jamii, na inataka kutumia mahakama kama chombo na kifiniko cha utekelezaji wa uhalifu wake. Walio mbali na walio karibu waunajua ufisadi uliokithiri katika taasisi zake, hasa kwa kuwa vyombo vyake vya usalama ndivyo vinajitokeza zaidi katika kukiuka mahakama na kupuuza maamuzi yake.

Enyi Watu wa Ardhi Iliyobarikiwa:

Mamlaka ya Palestina inatabikisha sera za maadui wa Uislamu zinazolenga kukuangamizeni na kuifanya Ardhi Iliyobarikiwa kuwa windo rahisi kwa umbile la Kiyahudi. Uhalifu wake dhidi yenu hauishii katika kuikabidhi ardhi hii kwa Mayahudi, watu wenye uadui zaidi kwa Waumini, bali umekwenda zaidi ya hapo ili kutoa sababu na masharti yote ambayo yanaliwezesha umbile la Kiyahudi kukaza mshiko wake kwenye Ardhi Iliyobarikiwa, mkubwa zaidi ni uharibifu wa jamii na ubomoaji wa maadili yake. Mlengwa sasa sio ardhi yenu kwa sababu imeshasalimishwa, badala yake, walengwa ni nyinyi, familia zenu na watoto wenu. Shambulizi hili ni pana, lenye kulenga elimu, familia, uchumi, idara mahakama na vyombo vya habari. Na tunaamini kwamba munaona athari zake mbaya kwa familia zenu na maslahi yenu. Kufikia hadi kwamba LGBTQ imetangaza vilabu na mikutano ya hadhara ambamo wananyanyua bendera zao kwa ukaidi wa wazi wa maadili ya kujisitiri na usafi.

Mamlaka ya Palestina, katika dori yake ya aibu ya usalama, sera zake za kiuchumi na kodi, na ufadhili wake wa ufisadi na mporomoko wa maadili, imekuwa ni kisu kinachowachinja watu wa Palestina na fimbo inayowavunja migongo yao, na kuua roho yao ya uasi na uwezo wao wa kustahamili umbile vamizi la Kiyahudi, na inakamilisha mzunguko wa ufisadi kwa ufisadi na dhulma zaidi katika idara ya mahakama na sheria. Msimamo wa watu wa Palestina dhidi ya hujma na ufisadi wa Mamlaka ya Palestina katika nyanja zote za maisha yao, na uungaji mkono wao kwa wale wote wanaopinga ukandamizaji wake na upuuzaji wake wa haki za watu kama wanasheria wanavyofanya hivi sasa, ni sehemu ya kuimarisha uthabiti wao na uwezo wao wa kubakia katika ardhi yao mpaka Mwenyezi Mungu Atakaporuhusu ushindi na ukombozi, na Umma na majeshi yake kuregesha dori yao na kuikomboa Masra (mahali pa Isra) ya Mtume. Iwapo watu watashindwa kufanya hivyo, hawatapoteza tu ardhi na matukufu yao kwa Mayahudi pekee, bali watapoteza pia utu wao, watoto wao, wenza wao, na hasara kubwa zaidi ni kupoteza Dini yao na kujitolea kwao katika sheria ya Mola wao Mlezi, na hiyo ndiyo hasara ya wazi.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَاتَّقُواْ فِتْنَةً لَّا تُصِيبَنَّ الَّذِينَ ظَلَمُواْ مِنكُمْ خَاصَّةً وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللَّهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ]

“Na jikingeni na Fitna ambayo haitowasibu walio dhulumu peke yao kati yenu. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.” [Al-Anfal: 25]. Mtume (saw) asema: «والَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ، لَتَأْمُرُنَّ بالْمَعْرُوفِ، ولَتَنْهَوُنَّ عَنِ المُنْكَرِ، أَوْ لَيُوشِكَنَّ اللَّه أَنْ يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عِقَاباً مِنْهُ، ثُمَّ تَدْعُونَهُ فَلا يُسْتَجابُ لَكُمْ» “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikoboni mwake! Hamtaacha kuamrisha mema, na hamtaacha kukataza maovu, isipokuwa Mwenyezi Mungu atakaribia kuteremsha juu yenu adhabu kutoka kwake, kisha mtamuomba wala hamtajibiwa.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu