Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  15 Dhu al-Hijjah 1444 Na: BN/S 1444 / 17
M.  Jumatatu, 03 Julai 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Bila ya Mlinzi au Msaidizi... Umbile la Kiyahudi Linaifanyia Ukatili Jenin kwa Kuua na Uharibifu
(Imetafsiriwa)

Tangu jana usiku, umbile la Kiyahudi limefanya mashambulizi makubwa dhidi ya Jenin na kambi yake, kwa kutumia droni, vifaru vya kivita na magari makubwa ya kijeshi. Pia limetuma mamia ya wanajeshi hadi Jenin katika uadui wake unaoendelea hadi sasa, ambao umeacha idadi ya mashahidi na makumi ya majeruhi, na matokeo yake kwa kuzingatia uadui huu wa kinyama unaongezeka na kuongezeka. Hili lilimfanya mkurugenzi wa Hospitali ya Al-Razi mjini Jenin azingatie idadi na uzito wa majeraha yanayoingia katika hospitali hiyo kuwa mbaya zaidi katika kipindi cha zaidi ya miaka 21.

Uadui huu muovu na unaoendelea unajiri kwa kuzingatia kimya cha watawala, mithili ya kimya cha watu wa makaburini, na kwa kuzingatia njama za Mamlaka ya Palestina ambayo haikusita jana usiku kuwakamata Mujahidina katika mji wa Jaba, katika wilaya ya Jenin na kwengineko, na chini ya ulinzi wa Marekani, kwani umbile la Kiyahudi lilitangaza kwamba lilikuwa limeijulisha Ikulu ya White House kuhusu operesheni yake huko Jenin.

Jinai za Mayahudi hazijakoma, bali zinaongezeka siku baada ya siku, na lau wangejua wao ni viumbe waoga zaidi wa Mwenyezi Mungu, na kwamba nyuma ya watu wa Jenin lau kungekuwa na mtawala atakayewapiga kwa pigo kubwa zaidi, waoga hawa wasingesubutu kugusa hata unywele wa mtoto kutoka kwa watu wa Palestina. Bali, uwepo wao katika Ardhi hii Iliyobarikiwa ungekuwa umeshafutwa. Tumeshuhudia uoga wao na wasiwasi wao uliokithiri wa maisha, na tumeona kuanguka kwao mbele ya ushujaa wa mtu binafsi, kama katika tukio la askari shujaa wa Misri, Mohamed Salah na katika ushujaa wa mujahidina huko Jenin, Nablus, Ukanda wa Gaza, na kwengineko. Hawa ni watu ambao hawana nguvu za kupigana wala kusubutu kufanya hivyo. Mkweli, Aliyetakasika amesema:

[لَا يُقَٰاتِلُونَكُمْ جَمِيعاً إِلَّا فِى قُرًى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَاءِ جُدُرٍ بَأْسُهُم بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعاً وَقُلُوبُهُمْ شَتَّى ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ]

“Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipo kuwa katika vijiji vilivyo zatitiwa kwa ngome, au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili.” [Al-Hashr 59:14].

Na ikiwa hii ndio hali, basi kuna udhuru gani kwa wale wenye vyeo na medali ambao wamezembea katika kutowanusuru watu wa Jenin?! Ni udhuru wa jeshi la Wamisri ni upi, ambao, endapo watahamasika, wangetikisa ardhi chini ya miguu ya wavamizi, na Vita vya Oktoba ni mfano mdogo tu wa hili, licha ya njama na usaliti?! Je, udhuru wa jeshi la Jordan ni upi kwamba kama lingetaka, na makamanda wake wa jeshi wanajua hili, wangeswali alasiri Al-Aqsa?! Je, udhuru wa jeshi la Uturuki ni upi inayohalalisha mahusiano na mnyakuzi huyu na kudai kusimama na watu wa Palestina? Uko wapi ulinzi wa Wauthmani?! Uko wapi ulinzi wa watu wa dini (Ahl ul-Din)?! Je, Waislamu wanauawa huku jeshi la Uturuki likiwa na mapigo ya moyo?! Jeshi la Pakistan liko wapi?! Viko wapi vipenzi vya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)?! Je, Masrah yake (saw) inanajisiwa na huku mnatazama? Muna shida gani?! Je, kauli mbiu yenu sio imani, taqwa, na jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu?! Kwani taqwa inakuiteni kuwahami Waislamu katika Ardhi iliyobarikiwa na kuilinda Masrah ya Mtume wenu, basi ikiwa hiyo sio jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, jihad ni ipi kwa maoni yenu?!

Palestina itabakia kuwa ni jeraha linalovuja damu maadamu Mayahudi wana umbile ndani yake, na suluhisho pekee lisiloepukika ni kuikomboa na kuling'oa umbile la Kiyahudi na masuluhisho mengine ni udanganyifu na upotoshaji, na hili litakuwa tu kupitia majeshi ya Ummah pekee, na kila upotokaji kutokana na dira kutoka kwa majeshi ni upaji nguvu Mayahudi juu ya shingo za watu wa Palestina ili kuongeza uhalifu, mauaji na uharibifu wao.

Jinai za Mayahudi na damu tukufu inayomwagwa leo kwenye ardhi ya Jenin na Palestina yote ni kilio kwa majeshi ya Ummah, kilio kwa wale ambao nyoyoni mwao bado wana chembe ya imani miongoni mwa makamanda wa wanajeshi. Kukuteni vumbi la udhalilifu kutoka mabegani mwenu na mgeuze meza juu ya vichwa vya watawala vibaraka na vunjeni viti vyao vya enzi na mwende Palestina, na muingie humo, kama wakombozi mkishangilia kwa takbira na tahlili, na mkiingia mtakuwa washindi, na kuweni na tawakul kwa Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi ni Waumini, na msipofanya hivyo, basi muko katika hatari kubwa.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache. Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Tawbah 9:38-39]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu