Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  25 Jumada I 1445 Na: BN/S 1445 / 10
M.  Jumamosi, 09 Disemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Marekani, iliyotafuta na kufuatiwa na Serikali za Vibaraka Waoga, ndiye Mdhamini wa Mauaji Kabla na Baada ya Kura ya Turufu
(Imetafsiriwa)

Marekani ilitumia nguvu yake ya kura ya turufu mnamo Ijumaa wakati wa upigaji kura katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya azimio lililopendekezwa na Imarati likitaka kusitishwa mara moja kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza. Azimio hilo liliungwa mkono na nchi 13, huku Marekani ikilipigia kura ya turufu. Uingereza ilijiepusha na kupiga kura.

Kura ya turufu ya Marekani juu ya kusitisha mapigano sio jambo jipya bali ni uthibitisho kwamba vitendo vya jinai vya umbile la Kiyahudi ni sehemu ya dhambi na maovu yake. Umwagaji damu isiyo na hatia wa umbile hili la kihalifu hufanywa kwa silaha za Marekani, fedha za Marekani, na pazia la Marekani. Kura ya turufu ni mwendelezo wa uhalifu na mauaji ya halaiki kupitia maazimio ya Marekani. Kwa hivyo, mikono ya Marekani imejaa damu ya Waislamu popote wanapoenda na popote wanapoingilia kati.

Ikiwa Marekani itakaa kimya, kimya chake ni dhulma, na ikiwa itazungumza, kauli yake ni ukafiri. Ikiwa itachukua hatua, huangamiza dunia na watu. Uhalifu uliofanywa na Marekani, iwe moja kwa moja au kupitia washirika wake kama umbile la Kiyahudi, kawaida ni utangulizi wa miradi yake ya uharibifu na maandalizi ya miradi yake miovu. Mipango yake ya kisiasa na harakati za kidiplomasia sio hatari sana kuliko umwagaji damu wake. Yote haya yanatoka kwa chanzo kimoja. Hakuna tofauti kati ya msaada wake kwa umbile la Kiyahudi wa silaha na mabomu, ukataaji wake wa kura ya turufu yu kusitisha mapigano, na uidhinishaji wake wa suluhisho ovu la dola mbili, ambalo linakusudia kumaliza suala la Ardhi Iliyobarikiwa na kulinda umbile la Kiyahudi kama umbo lisilo na silaha na lililo duni chini ya pazia la "Dola ya Palestina."

Hii ni Marekani ambayo watawala wadhalilifu wa Kiarabu na Waislamu wanaipigania na kuitii. Haya ndiyo maumbile ya taasisi zake za kimataifa, kama vile Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa. Ima Marekani inzitumia kumwaga damu kwa kutoa maazimio, kama ilivyokuwa nchini Iraq na Afghanistan, au inazitumia kukaa kimya juu ya umwagaji damu kwa kubatilisha maazimio, kama ilivyo kwa kura ya turufu kwenye kusitisha mapigano. Vyenginevyo, inatoa maamuzi ya kikoloni na miradi ya Kimagharibi, iliyohalalishwa na kupambwa na vibandiko vya sheria za kimataifa na haki, ili kuwahadaa watu wafikirie kuwa hizi ni zana na majukwaa ya kudai haki zao. Kiuhalisia, ni zana za Magharibi kupora na kukiuka haki hizo.

Na huo ndio uhalisia wa makafiri na miungano yao; baadhi yao ni washirika wa kila mmoja wao, na yeyote anayeshirikiana nao anakuwa mmoja wao na pamoja nao. Anakuwa mshirika katika uhalifu wao, iwe kupitia mapuuza yake na kimya au kupitia ushirikiano wake na ulaji njama. Hii inadhihirika katika vitendo vya watawala wa nchi za Kiarabu na Waislamu, ambao husaliti na kukaa kimya, au kushirikiana na kula njama na makafiri. Baadhi yao hata hutafutia soko miradi ya Marekani na hushirikiana nayo, kwani watawala hawa wanapigia suluhisho la dola mbili, kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُ مِنْهُمْ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao. Na miongoni mwenu mwenye kufanya urafiki nao, basi huyo ni katika wao. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.” [Al-Ma’ida:51].

Kukomesha mauaji ya halaiki na kuzuia kumwagwa damu isiyo na hatia hakuhitaji uamuzi uliowasilishwa na watawala vibaraka waoga katika Baraza la Usalama, Baraza la Marekani, kana kwamba wanatafuta msaada kutoka kwa muuaji kumsaidia mwathiriwa. Badala yake, inahitaji uamuzi na hatua kutoka kwa Waislamu, haswa wale walio na njia, kupitia kuzivunja tawala hizo vikaragosi. Kupitia kuziondoa, umbile la Kiyahudi litang’olewa kutoka kwa misingi yake, na ushawishi wa Marekani utakatwa, na kukata mkono wake fisadi ulioenea katika nchi za Waislamu. Bila ya hili, mzunguko wa uhalifu wa Marekani na ukoloni utaendelea, na hali hii itaendelea kuzorota kutoka kuwa mbaya hadi mbaya zaidi.

Kuvunjwa kwa ushawishi wa Marekani na mshirika wake, umbile la Kiyahudi, pamoja na tawala vikaragosi, sio tu inawezekana bali kihakika ni haki.

[وَتِلْكَ الْقُرَى أَهْلَكْنَاهُمْ لَمَّا ظَلَمُوا وَجَعَلْنَا لِمَهْلِكِهِم مَّوْعِداً]

“Na miji hiyo tuliwaangamiza watu wake walipo dhulumu. Na tukawawekea miadi ya maangamizo yao.” [Al-Kahf:59].

Kwa kuongezea, ni wajibu na faradhi juu ya Waislamu pindi Mwenyezi Mungu alipoamuru wawe huru na sio watumwa isipokuwa kwake, Mtukufu. Mwenyezi Mungu amedhamini nusra yake kwao ikiwa watainusuru njia yake.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَنصُرُوا اللهَ يَنصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُم]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad:7] Hakika, matokeo ya mwisho yako mikononi mwa Mwenyezi Mungu pekee.

[وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Yusuf: 21]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu