Jumatano, 23 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  23 Rabi' I 1442 Na: HTS 1442 / 30
M.  Jumatatu, 09 Novemba 2020

Ualishi wa Kuhudhuria Kongamano Jumuishi la Viongozi wa Makabila, Uongozi Mbali Mbali na Wanachuoni wa Sudan Mashariki
(Imetafsiriwa)

Mbali na fitna ya mizozo ya kikabila mashariki mwa Sudan, na kwa imani yetu kwamba Uislamu mtukufu, na kwa historia yote ya kibinadamu, kuwa ndio pekee utakaounganisha neno, na kuziunganisha safu na kuwayeyusha watu ndani ya chungu kimoja, bali hakika nidhamu za Uislamu ambazo Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume itazitabikisha, ndizo njia pekee kufikia Maisha ya Kiislamu, salama na ya utulivu, ambamo matukufu yatahifadhiwa ndani yake, na nyoyo kuungana ndani yake, ikisadikisha maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

﴿وَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ لَوْ أَنْفَقْتَ مَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مَا أَلَّفْتَ بَيْنَ قُلُوبِهِمْ وَلَكِنَّ اللَّهَ أَلَّفَ بَيْنَهُمْ إِنَّهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ﴾،

"Na akaziunga nyoyo zao. Na lau wewe ungeli toa vyote viliomo duniani usingeli weza kuziunga nyoyo zao, lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliye waunganisha. Hakika Yeye ndiye Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima." [Al-Anfal: 63]

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, inawaalika kuhudhuria kongamano jumuishi la viongozi wa Makabila, uongozi mbali mbali na wanachuoni wa Sudan Mashariki, chini ya kauli mbiu: 

﴿وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعًا وَلاَ تَفَرَّقُوا﴾

"Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane." [Aali-Imran: 103]

Mahali: Mji wa Gadharif - Ukumbi (Wad Al-Barra) mbele ya jengo la manispaa ya Gadharif.

Wakati: Jumamosi 21/11/2020 kuanzia saa 9:30 Asubuhi hadi saa 3:30 Alasiri

Kuhudhuria kwenu ni tofali katika jengo la maisha ya Kiislamu

Ibrahim Uthman (Abu Khalil)

Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu