Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  25 Muharram 1444 Na: HTS 1444 / 04
M.  Jumanne, 23 Agosti 2022

Majibu kwa Vyombo vya Habari
(Imetafsiriwa)

Dada Ustadha Um Wadhaah

Assalam Alaikum wa Rahamatullahi wa Barakatuh,

Jibu la swali lako mwishoni mwa hotuba yako (neno mpendwa) katika safu yako ya usomaji (neno la heshima) katika Gazeti la Akhbar Al-Youm, lililochapishwa leo, Jumanne, Muharram 25, 1444 H, sawia na 08/23/2022 M, Toleo Na. 10770, ambapo ilikuja katika hotuba ya kupendeza zaidi: (Jana, kaka mmoja aliniuliza swali muhimu na akaniuliza nitafute jibu na yaliyomo ndani ya swali hilo ni: Je! Ipi sababu ya kufeli kwa jamii ya Sudan katika kuunda uongozi ulioongoka unaochangia kuitoa Sudan katika giza na kuiingiza kwenye nuru tangu uhuru hadi sasa?? Yeyote mwenye jibu atupe, kupitia neno la Mwenyezi Mungu), mimi nasema: Kinaufanya uongozi kuwa wa hekima ni fikra ya kisiasa inayotokana na imani sahihi inayojumuisha mifumo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na mengineyo inayoweza kutatua masuala yote ibuka na kushughulikia mambo ya watu kwa uadilifu na usawa. Yeyote anayetazama makundi nchini Sudan anaona kwamba hayakuegemezwa kwenye fikra ya wazi ya kisiasa na hayakuwa na mipango ya wazi ya kisiasa, kiuchumi au kijamii. Bali, yameegemezwa juu ya urithi wa mkoloni kisiasa, kiuchumi na mwengineo, urithi unaopingana na imani yetu ya Kiislamu na kugongana nayo katika msingi na matawi; hiyo basi, tangu kuondoka kwa mkoloni, Sudan imekuwa ikiyumba na itaendelea kuyumba isipokuwa tutoke kwenye sanduku la mkoloni tulimowekwa ndani yake na kutufanya tusifikirie, bali yeye ndiye afikiri kwa ajili yetu kwa siri na dhahiri!

Ama kuhusu suluhu, ni rahisi sana na isiyo na utata iwapo tutaifanya itikadi ya Kiislamu kuwa ndio msingi ambao mifumo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na mengineyo inachipuza humo. Nazo ni hukmu za Shariah zinazotokana na wahyi mtukufu, na kutokana na msingi huu watu wameumbwa, kwani ni ndio uliombadilisha wenye kuabudu mawe kuwa mabwana wa dunia, na wachungaji wa ngamia na kondoo kuwa wachungaji wa mambo ya dunia. ulimwengu, na ndio uliowatengeneza viongozi walioongoka kama vile Abu Bakr Al-Siddiq, Omar bin Al-Khattab, Othman bin Affan, Ali bin Abi Talib na Omar bin Abdulaziz, Harun al-Rashid, Suleiman Mtukufu, na Abdul Hamid II, na wengine wengi ambao walitengenezwa kutokana na njia hii tukufu. Leo hii, njia hii ipo, na kuna chama ambacho kinatafuta pamoja na Ummah na kupitia kwacho kuifanya itikadi ya Kiislamu kuwa ndio msingi na hukmu za Shariah kuwa ndio kipimo. Ni Hizb ut-Tahrir, ndiyo inayotaka kuregea mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, na imejitayarisha kwa ajili hiyo, kwa kuwasilisha kwa Umma rasimu ya katiba yenye ibara 191 iliyovuliwa kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake (saw), na yale yanayoyaongoza kwa ijtihad sahihi, na ina ruwaza ya kina katika vitabu na machapisho kuhusu mfumo wa uchumi, mfumo wa utawala, idara, mfumo wa kijamii, mfumo wa huduma za afya, mfumo wa elimu na mengineyo. Na kukinai kwetu ni kwamba kutoka gizani kuingia kwenye nuru kunaweza kutokea tu kwa Uislamu, na Uislamu peke yake bila ya kuuchanganya na chochote, hata kiwe kidogo kiasi gani. Ni ule ulioutoa ulimwengu uliopotea hapo awali kutoka gizani na kuupeleka kwenye nuru, na ndio utakaowatoa watu leo, watu wote kutoka kwenye ukandamizaji wa urasilimali unaotawala ulimwengu hadi kwenye uadilifu na nuru ya Uislamu. Al-Faruq alikuwa sahihi aliposema: “Sisi ni watu ambao Mwenyezi Mungu amewatukuza kwa Uislamu, kwa hivyo tukitafuta utukufu kwengine kando nao, Mwenyezi Mungu atatudhalilisha.”

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu