Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  12 Jumada I 1444 Na: HTS 1444 / 16
M.  Jumanne, 06 Disemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wanajeshi na Raia Watia Saini Khiyana kwa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waumini
(Imetafsiriwa)

Wanajeshi na baadhi ya vikosi duni vya kiraia wakiongozwa na Vikosi vya Uhuru na Mabadiliko walitia saini rasimu ya makubaliano ya kisiasa ambayo yanafungua njia ya kuanzishwa kwa serikali ya kiraia kwa kipindi cha mpito. Makubaliano hayo yalishuhudiwa na mashahidi wa uongo kutoka kwa pande tatu; Volcker na washirika wake, Quartet; Marekani na Uingereza, na wafuasi wao Saudi Arabia na Imarati, na mwakilishi wa Muungano wa Ulaya.

Dibaji ya mradi huo chini ya kichwa cha Kanuni Jumla ilisema yafuatayo: [2- Sudan ni nchi yenye tamaduni nyingi, makabila, dini na lugha nyingi ambayo kitambulisho chake kinategemea vipengele vyake vya kihistoria na kisasa, vipimo vyake vya kijografia na urithi wake wa kitamaduni wa kipekee unaoenea kwa miaka elfu saba, yameunda anuwai yake na chanzo cha utajiri wake. 3- Sudan ni dola ya kiraia, ya kidemokrasia, ya kifederali, ya kibunge, ambayo ubwana wake uko mikononi mwa watu, ambao ndio chimbuko la mamlaka, na utawala wa sheria na uhamishaji wa madaraka kwa amani unatawala kupitia chaguzi huru na za haki ugavi wa haki wa mali na rasilimali].

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, na pamoja nasi watu wa Sudan wanaomuamini Mwenyezi Mungu, tunakataa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu chukizo hili kubwa na la wazi, na tunathibitisha yafuatayo:

Kwanza: Zaidi ya 98% ya watu wa Sudan ni Waislamu, na hawana thaqafa yoyote zaidi ya thaqafa ya Kiislamu, ambayo imani ya Kiislamu iliunda msingi wake. Ama watu hawa miongoni mwa watoto wa Kiislamu wa Sudan ambao wamepachikwa thaqafa ya Kimagharibi, wanajiwakilisha wao wenyewe na mabwana zao pekee ambao, bila kughafilika, waliwatawala juu ya Ummah.

Pili: Kuna uhusiano gani wa makabila na lugha na mifumo ya maisha, au ni kupotosha na kurusha jivu machoni ili kuufukuza Uislamu na hukmu zake, na kulazimisha mifumo ya kikafiri ya kikoloni ya Magharibi ambayo haina uhusiano wowote na makabila ya watu wa Sudan au lugha zao?!

Tatu: Kusema kwamba Sudan ni dola ya kiraia na ya kidemokrasia ni tamko la wazi juu ya usekula wa dola, na Sudan ni nchi ya Kiislamu ambayo dola yake lazima iwe juu ya msingi wa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na sio juu ya itikadi ya kutenganisha dini na maisha, na hivyo kuitenganisha na siasa na dola, ambayo ni Itikadi ya dola ya kiraia ya kidemokrasia.

Nne: Masharti ya dola ya kifederali ni utabikishaji wa mipango ya muuwaji wa Kiyahudi wa Kiamerika wa Mashariki ya Kati, Bernard Lewis, ambaye alipendekeza kuraruliwa kwa nchi zilizogawanyika za Kiislamu kwa misingi ya kikabila, kikanda na kimadhehebu. Dola katika Uislamu ni dola moja kwa Waislamu wote, sio dola ya kifederali. Mtume (saw) asema: «مَنْ أَتَاكُمْ وَأَمْرُكُمْ جَمِيعٌ عَلَى رَجُلٍ وَاحِدٍ يُرِيدُ أَنْ يَشُقَّ عَصَاكُمْ أَوْ يُفَرِّقَ جَمَاعَتَكُمْ فَاقْتُلُوهُ»  “Anapowajieni mtu wakati ambapo mumeungana chini ya mtu mmoja akataka kuwatenganisha, au kuugawanya umoja (jamaa) wenu, muuweni.”

Tano: Ubwana katika dola ya Kiislamu ni kwa Shariah na si kwa watu kama ilivyoelezwa katika mapatano ya kisiasa, Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:

[فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّى يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنْفُسِهِمْ حَرَجاً مِمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيماً]

“La! Naapa kwa Mola wako Mlezi! Hawataamini mpaka wakufanye wewe ndiye muamuzi katika yale wanayo khitalifiana, kisha wasione uzito katika nyoyo zao juu ya hukumu utayo toa, na wanyenykee kabisa.” [An-Nisa 4:65].

Kwa kumalizia: Wajibu wa kisheria kwa watu wa Sudan wa kukataa makubaliano haya si kwa sababu ni ya pande mbili kati ya uhuru, mabadiliko na jeshi, bali ni kwa sababu ni kinyume na Uislamu katika msingi na matawi yake na kufanya kazi kubwa ya kusimamisha Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida, kwa njia ya Utume, ndiyo dola pekee ya Kiislamu inayotakiwa na Sharia, ili Mwenyezi Mungu awe radhi nasi, na tuishi kwa ukarimu na furaha hapa duniani na Akhera.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal 8:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu