Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  17 Jumada II 1444 Na: HTS 1444 / 23
M.  Jumanne, 10 Januari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ubalozi wa Marekani waalika Kamati ya Walimu nchini Sudan kwenye Mkutano

Watawala wa Sudan, mko wapi? Mumetuletea Fedheha Gani?!
(Imetafsiriwa)

Imeelezwa katika gazeti la Al-Sudani lililotolewa leo Jumanne tarehe 10/1/2023 na vyombo vyengine vya habari kwamba, Afisi ya Utendaji ya Kamati ya Walimu ya Sudan ilipokea mwaliko kutoka kwa Ubalozi wa Marekani jijini Khartoum kufanya kikao cha pamoja, na Kamati hiyo ilisema katika taarifa yake fupi jana jioni kuwa kikao hicho kinalenga kujadili baadhi ya masuala yanayohusu Elimu, na athari za mgomo wa sasa wa walimu. Kamati hiyo ilisema kuwa Afisi ya Utendaji itakubali mwaliko huo, kisha itatangaza matokeo ya mkutano huo na kuyafanya yapatikane kwa walimu wote.

Tunajua kuwa nchi yetu, Sudan, na nchi nyingine za Kiislamu, hazidhibiti mambo ya utawala na siasa ndani yake, yeyote aliye madarakani. Bali wao ni vibaraka tu wanaotekeleza maagizo ya Magharibi Kafiri wa kikoloni katika nchi yetu, lakini hatukutarajia jambo hilo kuwa ukosefu wa heshima kiasi hicho. Kwa ubalozi wa Marekani kuingilia suala la ndani kikamilifu, na hata kualika baadhi ya raia wa serikali walio na matakwa. Watawala wa Sudan wao ndio wanapaswa kuyajadili na kuyatekeleza, sio kujadiliwa na Ubalozi wa Marekani unaodai kuwa na suluhu nao!

Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan tunakataa uingiliaji huu wa wazi na tunataka yafuatayo:

Kwanza: Balozi wa Marekani lazima afukuzwe, na ubalozi wa nchi yake ufungwe mara moja, kwa sababu Dola ya Kiislamu (Khilafah) hairuhusu kuwepo kwa balozi za nchi za kikoloni katika nchi yetu. Ibara ya 189 ya Rasimu ya Katiba ya Dola ya Khilafah iliyotayarishwa na Hizb ut Tahrir inatamka yafuatayo: “Tatu: Nchi ambazo hatuna mikataba nazo na dola halisi za kikoloni kama vile Uingereza, Marekani na Ufaransa, na dola zinazo mezea mate nchi yetu, kama vile Urusi, zinachukuliwa kuwa ni dola zilizo za kivita kihukmu, kwa hivyo tahadhari zote zinachukuliwa kuzihusu na si sawa kuanzisha uhusiano wowote wa kidiplomasia nazo...”

Pili: Ingefaa zaidi kwenu, ndugu katika Kamati ya Walimu ya Sudan, kukataa mwaliko huu, na kutoukubali, kwa sababu kwa kukubali kukaa na ubalozi wa Marekani, mumesaliti mambo yenu, na kuwasaliti ndugu zenu walimu ambao wametawanyika katika maeneo yote ya Sudan, kwani ni heshima mara elfu zaidi kwenu kubaki mukipambana kwa ajili yao hadi watawala wanyofu watakapoingia madarakani, na kutatua masuala yote, kuliko kumtegemea adui Kafiri kumuomba suluhisho kutoka kwake.

Tatu: Serikali lazima iwe makini katika kutatua masuala ya walimu na mengineyo, na isiwaruhusu kuomba haki, hasa katika masuala ya maisha, kwani Sudan ina rasilimali nyingi. Ikiwa tu kuna mtu anayeweza kutumia rasilimali kwa maslahi ya Ummah, na asiwe msaada kwa Kafiri wa kikoloni katika kufuja mali ya nchi na kuwafukarisha watu, na kuwadhalilisha mpaka kulazimishwa kukaa na adui.

Kwa kumalizia: Tuna hakika kwamba serikali iliyopo madarakani, na hata ile iliyotangulia, na hata ile itakayokuja kupitia muundo mbaya wa makubaliano, haitatatua tatizo kwa wananchi, wala hakutakuwa na maisha ya staha kwao, hivyo kila mtu lazima afanye kazi kwa ajili ya mabadiliko ya kweli ambayo yanatuondoa katika uwezo wa Kafiri wa kikoloni, vibaraka na wasaidizi wake. Na hiyo ni kwa kupitia kufanya kazi kwa bidii na Hizb ut Tahrir, kiongozi asiye wadanganya watu wake, na ambaye anajitahidi kupitia kwenu na pamoja nanyi kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume inayoweka maisha ya heshima na hadhi, na kuukata mkono wa Kafiri wa kikoloni ili Mola Mtukufu (swt) awe radhi nasi.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ)

Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu