Jumamosi, 04 Rajab 1446 | 2025/01/04
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  12 Rajab 1445 Na: 1445 / 11
M.  Jumatano, 24 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Urithi, Utamaduni, na Utambulisho Wetu Umekita Mizizi ndani ya Uislamu, Sio katika Desturi na Mila za Ustaarabu wa Kipagani Uliopitwa na Wakati!
(Imetafsiriwa)

Mwanamke mmoja mdogo kutoka Sudan alishiriki katika mashindano yanayojulikana kama ‘Miss World’, ushiriki uliosherehekewa na Yaser Arman, kiongozi katika Baraza Kuu la Uhuru na Mabadiliko akitoa maoni yake kwa ujanja, licha ya athari kubwa ya utamaduni wa uokoaji dhidi ya ubunifu, urembo, na wanawake, Tibah Diab, mshiriki kijana, alionyesha ujasiri na ufahamu, akisubutu kushiriki katika mashindano ya urembo na kujaribu kuakisi sehemu ya turathi, utamaduni, na utambulisho wetu. (Tovuti ya Sudan Pulse)

Mkusanyo wa kimakusudi fikra baina ya dini ya watu wa Sudan ambayo imeweka mfumo makhsusi wa maisha kwa wanawake, na utawala wa kisekula na utamaduni wake, utawala ambao haukushikamana na Uislamu, si chochote ila ni uwongo mtupu na hadaa. Kila mwenye ujuzi anajua kwamba katika mfumo wa uokoaji uliopitwa na wakati, hakuna chochote cha Kiislamu katika katiba yake isipokuwa tu neno Bismillah Al-Rahman Al-Rahim. Msemo huu ulipingwa na wanasiasa wa kisekula kama Arman, ambao wanalenga kutumia mkusanyiko wao wa kimakusudi kama nyenzo ya kuwatenganisha Waislamu wa Sudan na Uislamu kwa kuuhusisha na utawala wa uokoaji, utawala ambao haukuwa na uhusiano wowote na Uislamu na, kwa kweli, ni mfumo wa kikafiri.

Mwenyezi Mungu, Mtukufu, ameweka ubunifu na urembo wa kweli katika kuheshimu wanadamu na akili ya mwanadamu - mahali pa kuwajibika. Kupitia kwayo, kuwepo kwa Muumba kunathibitishwa, na kwa kuifahamu, watu huinua tabia zao, kurekebisha maisha yao ya kidunia na Akhera.

Uislamu umeufanya ujumbe wake kuwa wa mwisho na sheria yake tukufu kwa wanadamu. Mwanaume wala mwanamke siye kitovu cha mazungumzo na jukumu. Wanawake wanaheshimiwa na kuhifadhiwa, wakiwekwa mbali na fahamu za kisekula zinazoigeuza miila yao kuwa ni bidhaa, hivyo kusherehekea dhati ya uumbaji.

Urithi, utamaduni, na utambulisho wa watu wa Sudan umekita mizizi katika Uislamu mtukufu. Wale wanaoshikamana nao wanaokolewa kutoka kwenye shimo la maangamizi ya makafiri, shimo ambalo wanasiasa wa kisekula wametafuta kwa muda mrefu kuuingiza Ummah, wakiuza bidhaa zilizochanganyika na ukafiri, wakijisongeza karibu na mabwana zao wanaowafadhili na kujaza hazina zao pamoja nao!

Tunajitahidi kusafisha urithi wetu, kama Waislamu wa Sudan, kutokana na mila na desturi, kama vile uchi, uchezaji densi, na kuimba katika hadharani.

Bila shaka, Muislamu yeyote mwenye ufahamu wa kimsingi wa hukmu za Kiislamu anajua kwamba uchi katika mashindano kama hayo ni umeharamishwa kidini, unakubaliwa tu na wale waliopotoka kimaadili pekee!

Utambulisho wa watu wa Sudan ni Uislamu mtukufu, na Mwenyezi Mungu (swt) bila shaka ataupa ushindi Ummah huu, na kuurudishia hadhi yake na hadhi yake kama Mwenyezi Mungu alivyokusudia uwe—Umma bora ulioletwa kwa ajili ya wanadamu, wenye kushikamana na Sharia, kuifikisha kwa walimwengu, kuchunga kushikamana huku kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Khilafah hii itawaneemesha watu wa Sudan na kila Muislamu kwa dini ya Mwenyezi Mungu, kuwatangaza kuwa ni watumwa wa Mwenyezi Mungu peke yake, kwa kutekeleza sheria za Mwenyezi Mungu, na kukata njia za waru masekula.

Msemaji Rasmi wa Kike wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu