Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  22 Muharram 1446 Na: HTS 1446 / 04
M.  Jumapili, 28 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wale Ambao Hawakufa kwa Risasi za Vita Walikufa ndani ya Makaazi ya Serikali!
(Imetafsiriwa)

Sudan Tribune iliripoti jana, Jumamosi, Julai 27, 2024, ikinukuu taarifa iliyotolewa na Kamati ya Maandalizi ya Umoja wa Madaktari wa Sudan, iliyosema: “Kamati ya Maandalizi ya Umoja wa Madaktari ilisema katika taarifa iliyopokelewa na Sudan Tribune kwamba watu waliokimbia makaazi yao mjini Kassala wanaishi kwenye mahema yaliyochakaa na kuzungukwa na maji kila upande, na watoto wao wanalia kwa njaa. Iliongeza kuwa hali imekuwa mbaya zaidi, kwani watoto wawili walikufa kwa shoti ya umeme, na kuna vifo kutokana na kuumwa na nyoka na kesi zingine zisizojulikana.”

Kinachofichuliwa na watu waliohama kutokana na vita katika majimbo hayo yanayoitwa salama ni jambo la kuogofya, wamekuwa kama mtu anayetafuta kimbilio kutoka kwenye kikaango na kuingia ndani ya moto! Wale ambao hawakufa kwa risasi za vita walikufa ndani ya makaazi ya serikali ambayo yanakosa mahitaji ya kimsingi ya maisha, ambapo watu waliohamishwa kila wakati huwekwa katika maeneo ambayo hayafai kwa makaazi ya wanadamu! Kinachotokea Kassala ni mfano tosha wa unyanyasaji wa kinyama waliyokuwa wakifanyiwa watu waliohamishwa, ambapo waliwekwa kwenye mahema chakavu kama ilivyoelezwa katika taarifa hiyo, na baya zaidi ni kwamba makaazi hayo ni sehemu ya chini ambayo maji ya mvua yanakusanyika, ambapo baadaye husababisha magonjwa na mikurupuko. Watu waliokimbia makaazi yao tayari wanakabiliwa na uhaba wa chakula, na magonjwa yanaenea kutokana na kuzorota kwa hali ya afya, na sasa tuko mwanzoni mwa msimu wa vuli na mvua ndiyo inaanza, hivyo ikiwa serikali haitasonga kutafuta makaazi mbadala yanayofaa kwa watu waliohamishwa, jambo hilo litakuwa janga kwa kila maana ya neno hili.

Sisi katika Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan tunaiwajibisha serikali ya shirikisho na serikali ya Jimbo la Kassala kikamilifu kwa kile kilichotokea na kinachotokea kwa watu waliohamishwa katika maeneo ya makaazi huko Kassala na tunataka wachukue hatua za haraka kurekebisha hali hiyo, kwani huu ni wajibu wa kidini juu yao na wala sio ihsani kutoka kwao. Mtawala katika Uislamu ni mchungaji na anawajibika kwa raia wake, kama ilivyoelezwa katika Hadith Sahihi: «...وَالْإِمَامُ الَّذِي عَلَى النَّاسِ رَاعٍ وَهُوَ مَسْؤُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “... na mtawala aliye juu ya watu ni mchungaji na ataulizwa juu ya raia wake” Kinachotokea katika nchi yetu kwa kukosa utunzaji ni kutokana na kutokuwepo Uislamu chini ya dola yake. Lau tungekuwa na dola yenye msingi wa Uislamu, maafa kama haya yasingetokea kwa watu, kwa sababu Khalifa angetoa makaazi ya staha kwa waliokimbia makaazi yao, chakula, dawa, na mavazi. Kwa kweli, vita hivyo vilivyolaaniwa mwanzo hata visingetokea.

Enyi watu wa Sudan popote pale, hasa wale waliohamishwa na maangamizi ya vita: Hamna wokovu kwenu ila kwa kushirikiana na wale wanaofanya kazi ya kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu duniani kwa kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Ni Khilafah peke yake ndiyo itakayosimamia mambo yenu na kukupeni maisha yenye heshima, salama, na yenye dhamana. Zaidi ya yote, ni wajibu wa Mola wenu Mlezi (swt) ambaye amekufaradhishieni kuhukumu kwa Kitabu Chake na Sunnah za Mtume Wake (saw).

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal 8:24]

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu