Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  3 Jumada I 1446 Na: HTS 1446 / 21
M.  Jumanne, 05 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mjumbe wa Marekani Anajihusisha na Udanganyifu na Uongo, Ikifichua Ukweli wa Vita kama Pambano lake na Uingereza
(Imetafsiriwa)

Katika mahojiano na gazeti la ‘Sudan Tribune’ jijini Kampala, Uganda, mnamo Jumatatu, 4 Novemba, 2024, mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan, Tom Perriello, alionya kuhusu kutiririka kwa silaha na wapiganaji wa kigeni nchini Sudan. Pia alizungumza kuhusu ukiukwaji wa kutisha unaotokea kutokana na vita, akisema kuwa nyaraka na uhakiki unaendelea ili kuwawajibisha wanaohusika. Perriello alisisitiza kuwa kuingia kwa silaha kutakuwa na matokeo mabaya na ya gharama kubwa kwa hali nchini humu.

Perriello alisema kuwa Marekani inafanya kazi kwa karibu na Troika na ndani ya muktadha wa dori ya sasa ya Uingereza kwenye Baraza la Usalama. Aliongeza, “Sizungumzi kwa niaba ya Uingereza, lakini naamini wamekuwa wazi sana kuhusu Sudan kuwa kipaumbele cha serikali hii mpya, na wana hamu ya kushinikiza kuwepo kwa uongozi mkubwa zaidi wa Umoja wa Mataifa.”

Sisi katika Hizb utTahrir / Wilayah Sudan, tumesisitiza mara kwa mara kwamba mzozo wa Sudan ni mapambano ya ushawishi kati ya Marekani na Uingereza. Tumeangazia dori ya Amerika katika kuchochea vita nchini Sudan na dori yake kuu ya kuvirefusha kupitia vibaraka wake wanaoongoza Vikosi vya Msaada wa Haraka, pamoja na viongozi fulani wa jeshi. Hii ni kutokana na kutokuwa na uwezo wa kuwaondoa vibaraka wa kiraia wa Uingereza ndani ya Majeshi ya Uhuru na Mabadiliko (ambayo kwa sasa yanawakilishwa na Uratibu wa Maendeleo).

Hadi leo, Marekani inasimamia vita hivi, inaanzisha jukwaa la mazungumzo, na kuzuia nchi nyingine kuingilia Sudan, kama Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesema mara kwa mara.

Ama kuhusu mazungumzo kuhusu silaha na maonyo dhidi ya uingiliaji kati wa kigeni, huu ni unafiki wa Marekani, udanganyifu, na taarifa potofu. Umoja wa Mataifa ni nguvu ya kigeni inayoingilia na hatari zaidi inayohusika na masuala ya Sudan na hatari zaidi kwa watu wake; hutoa silaha kupitia vibaraka wake ili kuchochea vita. Ripoti zinaonyesha kuwa silaha za Kimarekani zimefika Al-Fashir, na kwamba kivuko cha Adré kilifunguliwa baada ya Makubaliano ya Geneva kufanya kama njia uhai ya kuvisambazia Vikosi vya Msaada wa Haraka mahitaji, vifaa, na silaha chini ya kivuli cha misaada ya kibinadamu. Matamshi ya Perriello kuhusu Uingereza na Sudan kuwa kipaumbele kwa serikali yake mpya yanathibitisha kile tulichosema kuhusu mapambano ya kikoloni kati ya Marekani na Uingereza kuhusu Sudan, na huyu hapa Perriello akifichua kwa ujanja.

Hebu Amerika, wajumbe wake, na vibaraka wake na wajue kwamba watu wa Sudan si wajinga; bali, wanatawaliwa na viongozi duni, wasaliti wanaotekeleza ajenda za makafiri wa kikoloni. Hii ndiyo sababu ya ukosefu wa usalama na haki. Kutoka kwa Abu Hurairah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «سَيَأْتِي عَلَى النَّاسِ سَنَوَاتٌ خَدَّاعَاتٌ يُصَدَّقُ فِيهَا الْكَاذِبُ وَيُكَذَّبُ فِيهَا الصَّادِقُ وَيُؤْتَمَنُ فِيهَا الْخَائِنُ وَيُخَوَّنُ فِيهَا الأَمِينُ وَيَنْطِقُ فِيهَا الرُّوَيْبِضَةُ» قِيلَ: وَمَا الرُّوَيْبِضَةُ؟ قَالَ: «الرَّجُلُ التَّافِهُ فِي أَمْرِ الْعَامَّةِ»‏   “Itawajia watu miaka ya khiyana, ambapo muongo atasadikiwa, na mkweli atakadhibishwa; msaliti ataaminiwa, na mwaminifu atachukuliwa kuwa msaliti; na Ruwaibidha ndio watakaoamua mambo.” Ikasemwa: ‘Ni akina nani hao Ruwaibidah?’ Akasema: “Watu waovu na wanyonge wanaotawala mambo ya watu.” (Imepokewa na Ibn Majah na Ahmad).

Udhalimu wa Marekani na jinai zake dhidi ya Sudan, na dhidi ya ardhi zote za Waislamu, hautakoma—kama vile inavyowapa Mayahudi silaha ili kuiangamiza Gaza na kuwaangamiza watu wake huku ikizungumzia amani na kusimamisha vita. Ukandamizaji huu utasitishwa tu na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, inayoongozwa na Khalifa mwadilifu anayeisimamisha Dini, kutekeleza Sharia, na kuwatetea waumini na wanaodhulumiwa. Kutoka kwa Abu Hurairah kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «الإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Kiongozi (wa Waislamu) ni ngao yao. Wanapigana nyuma yake na wanalindwa na (yeye kutokana na madhalimu na wavamizi).” (Imepokewa na Bukhari na Muslim).

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu