Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Sweden

H.  8 Safar 1445 Na: 1445 / 02
M.  Alhamisi, 24 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Utendaji Mbaya wa Serikali Unaonyesha Sura Halisi ya Chuki kwa Uislamu ya Dola la Uswidi

(Imetafsiriwa)

Hadi leo, Quran bado inachomwa moto mara kwa mara katika mitaa ya Uswidi. Serikali yatangaza kwamba vitisho dhidi ya Uswidi vimeongezeka, na polisi wa usalama wamepandisha kiwango cha vitisho vya ugaidi kutoka 3 hadi 4. Serikali inajaribu kudhibiti hali hiyo kwa kuwaalika wawakilishi wa Waislamu, kufanya mazungumzo na dola zengine na kutuma jumbe kwa Waislamu wa nchi hiyo. Waziri Mkuu alishiriki katika programu ya Ajenda ya SVT mwishoni mwa juma ili kutoa maoni yake juu ya kiwango cha tishio kufuatia kuchomwa moto kwa Quran na akatangaza kwamba mtu yeyote ambaye hakubali "ukosoaji wa Uislamu" yuko katika nchi isiyofaa. Naibu Waziri Mkuu pia alizungumzia hali hiyo katika hotuba yake ya msimu wa kiangazi ambapo alisema kuwa tafsiri ya Uislamu ambayo haikubali kuchomwa moto kwa Qur'an haina nafasi nchini Uswidi na ambapo pia aliwataka Waislamu "kugeuza shavu la pili".

Dola ya Uswidi chini ya serikali mbalimbali, imejaribu kuwasambaratisha Waislamu kwa matumaini ya kuwaoanisha na kutokomeza kitambulisho chao cha Kiislamu. Kila kitu kuanzia kuwateka nyara watoto, kuzifungia shule za Kiislamu, kupiga marufuku uvaaji wa hijab na ukandamizaji wa heshima hadi uchomaji moto wa Quran ni sura mbalimbali za haya.

Serikali inasisitiza kuwa ni halali kuchoma Quran lakini wakati huo huo inajaribu kutuma ujumbe kwa ulimwengu wa nje kwamba Uswidi sio nchi inayochukia Uislamu. Hii ndiyo serikali ile ile inayoshirikiana na Wanademokrasia wa Sweden, ambao mara kwa mara wanachochea dhidi ya Uislamu, Mtume, Quran na Waislamu. Waziri Mkuu, Ulf Kristersson, aliliita shambulizi la kuchukiza la Richard Jomshof dhidi ya Mtume Mohammad (saw), ambapo anamwita mtume kuwa ni jambazi, mbabe wa kivita na muuaji wa halaiki, "ukosoaji wa Uislamu" katika Agenda mnamo Jumapili jioni. Katika sehemu hiyo hiyo, alikuwa na ujumbe kwa Waislamu: "wale ambao hawawezi kulikubali hilo wanaishi katika nchi isiyo sahihi".

Naibu Waziri Mkuu Ebba Busch pia alikuwa na ujumbe kama huo kwa Waislamu katika hotuba yake ya msimu wa joto, akiwataka Waislamu kugeuza shavu la pili na kwamba toleo la Uislamu ambalo haliwezi kukubali kuchomwa moto kwa Quran halina nafasi nchini Uswidi.

Ujumbe wao uko wazi; Uislamu wa kisekula unakaribishwa nchini Uswidi na Waislamu wanaokana maadili yao ya Kiislamu wanakaribishwa huku wale wanaochagua kushikamana na Uislamu ni "Waislamu wenye msimamo mikali" ambao hawana nafasi nchini Uswidi. Ni wazi kwamba kuruhusu kuchomwa moto kwa Qur'an ni kuwasawazisha na kuwalazimisha Waislamu kukubali kejeli ya imani yao na kuwalazimisha kushikamana na uhuru wa kuzungumza juu ya Uislamu. Serikali ya Uswidi bila shaka ni serikali inayochukia Uislamu na inafuata sera ya chuki dhidi ya Uislamu.

Jambo ambalo Serikali ikiongozwa na Waziri Mkuu na manaibu wake inashindwa kuelewa ni kwamba maadili yetu hayauzwi kama yao. Waislamu hawajawahi na kamwe hawatayatelekeza maadili ya Kiislamu kama wanasiasa wa Magharibi wanavyofanya ambapo wanahujumu kanuni zao wenyewe za kidemokrasia katika vita dhidi ya Uislamu. Serikali za Magharibi, wabebaji viwango vya uhuru, ikiwemo Uswidi, zinajihusisha na udhalimu wa kimaoni ambao unalenga kuharamisha maoni fulani ambayo yanapotoka nje ya muundo wa usekula. Si katika maumbile ya Waislamu kupiga magoti au kugeuza shavu jengine mbele ya matatizo. Kwa zaidi ya karne moja, Waislamu wamekuwa wakikabiliwa na kila aina ya ukandamizaji na mpaka leo Waislamu wanasimama wima na kuheshimu kila maelezo ya Uislamu. Uislamu, tofauti na Ukristo na Uyahudi, umekataa kugeuza shavu la pili mbele ya makabiliano ya ghasia ya usekula ili kuuondoa siasa na kuufanya kuwa wa kisekula. Hii ndiyo sababu halisi ya vita dhidi ya Uislamu.

Katika muktadha huu, Carl B. Hamilton, Mbunge wa zamani kutoka katika chama cha third governing party, alisema kwamba mpaka ungechorwa lau kama mashambulizi hayo yangekuwa dhidi ya Mayahudi.

Vita dhidi ya Uislamu vinataka kuuondosha kabisa Uislamu lakini wanajua kuwa wao ni dhaifu sana kufanikiwa. Hivyo basi, badala yake wanajaribu kuutia usekula Uislamu na kufuta chembe zake za kisiasa kama vile Khilafah, Jihad na Sharia.

Jaribio lisilo na matumaini la serikali kutangaza sura ya kirafiki kwa Uislamu kwa ulimwengu litafeli kwa sababu Waislamu wanaweza kuona moja kwa moja unafiki wao. Wawakilishi wa Waislamu wanaokubali mwaliko kutoka kwa serikali wanafanya tu matakwa ya serikali. Serikali haiwaaliki wawakilishi wa Waislamu ili kusikia maoni yao au kutatua tatizo, wanafanya hivyo tu kuwatumia ili kuuhadaa ulimwengu kwamba hawana tatizo na Waislamu tatizo lao tu ni Waislamu wenye misimamo mikali. Majaribio hayo yasiyo na matumaini hayamdanganyi yeyote, na Waislamu wanaweza kuona yaliyo ndani yake. Siri iliyo nyuma ya subira na ukakamavu wa Waislamu ni imani yetu thabiti katika maadili yasiyo tingishika ya Uislamu na fauka ya hayo imani thabiti kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kwamba Yeye huwapa ushindi waja wake waumini, ushindi huo pasi na shaka uko karibu hasa hivi sasa kwamba mfumo wa kirasilimali umeshajichimbia kaburi lake wenyewe.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uswidi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Sweden
Address & Website
Tel: 
https://hizb-ut-tahrir.se/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu