Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  25 Rabi' I 1444 Na: 06 / 1444 H
M.  Ijumaa, 21 Oktoba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuunganisha Wito na Safu ni Miito ya Haki Inayokusudiwa Kutumiwa kwa ajili ya Batili  
(Imetafsiriwa)

Chini ya uelekezi wa viongozi wa mfumo unganishi wa makundi, kumekuwa na miito mingi kwa pande zote mbili za yale yanayoitwa maeneo yaliyokombolewa katika siku za hivi karibuni kuungana chini ya uongozi mmoja unaowaleta pamoja.

Enyi Waislamu katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Ash-Sham:

Miaka 12 imepita tangu yalipoanza mapinduzi yaliyobarikiwa ya ash-Sham, ambapo watu wa Ash-Sham walionja aina zote za mateso, yakiwemo mauaji, dhulma, ukandamizaji, uhamisho, kunyimwa, kukamatwa na mauaji ya halaiki. Miaka yote hii na mateso yote haya hayakujumuisha dhamira ya umoja kati ya viongozi wa mfumo  unganishi wa makundi, na kila kundi liliendelea kupigana peke yake, au ndani ya kile kinachoitwa "vyumba vya operesheni", hadi hali ya mapinduzi ilipofikia ile ilivyo sasa. Si hayo tu, bali pia mapigano ya makundi yalizuka kati ya vipengele vya mfumo huo wa makundi, ambayo yalisababisha kuvunjika kwa makundi mengi na kuhama kutoka katika mandhari, na yote haya yalitokana na sera za zile nchi zinazoitwa zenye kutoa msaada kwa kuegemea kanuni ya "gawanya utawale", ambayo ilikuwa na ingali inawalisha viongozi wa mfumo unganishi wa makundi sumu ya pesa chafu za kisiasa, kwa hivyo kila kiongozi wa kundi unganishi alikuwa makini juu ya uhuru wa kundi lake kwa kupenda pesa na udhibiti.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, nyumba ya Uislamu:

Bila shaka umoja wa safu na wito wake ni wajibu wa Kisheria, hitaji la watu wengi, na ni jambo la dharura mno, ikiwa umoja huu utaegemezwa kwenye kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu Peke Yake, na wale wanaousimamia watatafuta kupata radhi zake (Mwenyezi Mungu) kwa kuipindua serikali na kusimamisha utawala wa Uislamu. Walakini, ikiwa umoja huu utaegemezwa juu ya maagizo ya ujasusi wa zile zinazoitwa nchi zenye kutoa msaada, ambayo juu yake ni ujasusi wa serikali ya Kituruki, na wale wanaoisimamia kutaka kuiridhisha Magharibi kafiri kwa kutekeleza maridhiano na dhalimu wa Sham, au lile linaloitwa suluhisho la kisiasa, basi bila shaka ni miito isiyokusudiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, bali inakusudiwa kwa ajili ya batili.

Enyi Waislamu katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Ash-Sham:

Hapana shaka kwamba kuhitimisha maridhiano na dhalimu wa ash-Sham kunahitaji chama kimoja kitakachowakilisha kile kinachoitwa “upinzani,” kwani ni moja ya sharti la amani, sawa na ilivyotokea ilipoundwa kile kinachoitwa Kamati ya Majadiliano, ambayo ilizingatiwa kuwa chama pekee cha kujadiliana na dhalimu wa ash-Sham, na ilipewa uhalali wa kirongo katika Kongamano la Riyadh ambapo wawakilishi wa vipengele vingi vya mfumo unganishi wa makundi walialikwa. Kwa hivyo, ni lazima kutambua kwamba lengo la wito wa umoja sio kupindua utawala wa kihalifu, lakini kinyume chake, lengo ni kupatana nayo na kuizalisha upya, na hatua za kwanza za kivitendo kwa hilo ni kufungua vivuko vya kuhalalisha kwayo, na kwamba lengo la wito wa umoja sio kutabikisha Shariah ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuzingatia Maagizo yake, lakini kinyume chake kabisa, lengo lake ni kutekeleza mfumo wa kisekula na kuzingatia maamrisho ya wafuasi, na kwamba lengo la kufanya maandamano ya kutaka umoja ni kuwatumia watu kama kiota chenye kutoa kifiniko halali cha uhalifu kutendwa, kuanzia uhalifu wa mapigano ya makundi, na sio kuishia na uhalifu wa amani na dhalimu wa Ash-Sham.

Enyi Waislamu katika Ash-Sham, nyumba ya Uislamu:

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّهِ جَمِيعاً وَلَا تَفَرَّقُوا]

“Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane.” [Aali-Imran:103]. Mwenyezi Mungu Mtukufu amebainisha kushikamana na kamba yake na sio kamba za ujasusi za zile zinazoitwa zenye kutoa msaada, kisha akasema:

[جَمِيعاً]

“Nyote pamoja” yaani, kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Utukufu, lazima kufanyike kwa pamoja, na sio kwa kila mtu kushikamana kivyake. Kisha akakataza mafarakano. Hii ni kwa sababu matendo ya pamoja ya watu wengi ni matendo yenye tija na madhubuti ambayo yanapelekea kurekebisha mwenendo wa mapinduzi na kufikia lengo linalotarajiwa wakati yanapokuwa na uongozi wa kisiasa wenye ufahamu na wa dhati unaokubali mradi wa kisiasa ulio wazi unaotokana na imani ya watu wa Ash- Sham.

Na ndugu zenu katika Hizb ut Tahrir, kiongozi asiye wadanganya watu wake kama mlivyoizoea, inakuleteeni mradi wa kisiasa ulio dhahiri na wa wazi unaotokana na itikadi ya Kiislamu, basi weka mikono yako katika mkono, ili sote tutembee, tukiwa tumeshikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, tukizikata kamba za mashetani watu na majini wanaotaka kuyazika mapinduzi ya Ash-Sham na kupoteza mihanga ya watu wake, kwani ndani yake yamo maisha ya izza, tamkini na ushindi.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[يا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal:24].

Ahmad Abdul Wahhab
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu