Jumatatu, 23 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/25
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Syria

H.  6 Dhu al-Hijjah 1445 Na: 05 / 1445 H
M.  Jumatano, 12 Juni 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Maadui wa Mapinduzi Wanaogopa Vuguvugu la Ummah na Wanaonya kuhusu Kupoteza Udhibiti
(Imetafsiriwa)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, ameonya juu ya kuongezeka kwa taharuki nchini Syria, na kulitaja kuwa eneo jengine hatari linaloonyesha mwelekeo wa kupamba moto. Amefahamisha kuwa kadhia ya Syria inahitaji mkabala wa kina ili kufikia suluhu endelevu. Kauli hii aliitoa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa sita wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Baraza la Ushirikiano wa Ghuba (GCC), uliofanyika jijini Doha mnamo tarehe 9 Juni 2024. Alithibitisha kuunga mkono juhudi za Umoja wa Mataifa na Mjumbe wake Maalum, Geir Pedersen, kufikia suluhu ya kisiasa nchini Syria kwa kuzingatia azimio nambari 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Pia alisifu uamuzi wa Saudi Arabia wa kumteua balozi wa Damascus.

Tangu kuzuka kwa Mapinduzi ya Ash-Sham, serikali ya Uturuki imekuwa ikitekeleza maagizo ya Marekani kukandamiza mapinduzi hayo. Hata hivyo, wametambua kwamba pamoja na njama zao zote, hawajaweza kuwatiisha watu wa Sham (Syria) wala kuleta utulivu wa utawala wa kihalifu. Kinyume chake, wameanza kuonya juu ya mzozo huo wa muda mrefu, wakihofia hatari zisizotarajiwa na zisizohesabika zinazochochewa na ari ya Umma ya mapinduzi na kuyapendelea mapinduzi. Hii ni kweli hasa kwa wimbi jipya la mapinduzi dhidi ya viongozi wanaohusishwa na ujasusi wa Uturuki na wengineo, na juhudi za Ummah za kuregesha mamlaka yake na kufanya maamuzi ili kufikia lengo lake la kusonga mbele kuelekea mji mkuu ili kutwaa taji na kufikia matokeo yanayotarajiwa: kuiangusha serikali na kusimamisha utawala wa Kiislamu.

Kauli ya Fidan inalingana na kukiri kwa Pedersen kwamba kile anachokiita "mgogoro wa Syria" hakiwezekani kutatuliwa, na kwamba hawatajisalimisha kwa sababu kinaweza kuwalipukia tena nyuso mwao, kama alivyosema. Pedersen aliona kuwa ni kosa kubwa kuiacha kadhia ya Syria bila kutatuliwa, pamoja na matatizo yake yanayoongezeka ambayo yanaweza kuzuka wakati wowote, kwa sababu utulivu uliopo sasa ni wa muda tu na hakuna uhakika wa kuendelea kwake.

Ahmet Yıldız, Mwakilishi wa Kudumu wa Uturuki katika Umoja wa Mataifa, alizungumzia ugumu wa kufikia suluhu ya kudumu ya kisiasa nchini Syria kwa sasa, akitoa wito kwa serikali ya Damascus kuanzisha maridhiano ya kweli ya kitaifa. Hapo awali, Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Yaşar Güler alisema kuwa Uturuki inaweza kufikiria kuondoa vikosi vyake kutoka Syria ikiwa mipaka yake itakuwa salama, akimaanisha usalama wa vikosi vya utawala wa kihalifu wa Assad.

Matamshi haya, yanayoashiria hofu, yanaakisi hofu ya maadui kwamba moto katika maeneo yaliyokombolewa ya Idlib na kwengineko utatoka nje ya udhibiti, na kurudisha mamlaka kwa wanamapinduzi wanyoofu. Wanaonya juu ya mlipuko na kupoteza udhibiti wa ala zao katika maeneo yaliyokombolewa, yanayowakilishwa na viongozi wa makundi. Kwa hivyo, wanaharakisha hatua kuelekea suluhisho la kisiasa na maridhiano.

Kwa hivyo, ni sharti kwa wanamapinduzi kuwa makini na wapangaji njama dhidi yao ili kutibua njama zao. Ni lazima waendeleze harakati zao zilizobarikiwa ili kupata tena mamlaka na kufanya maamuzi huku wakizingatia misingi yao. Kisiasa na kijeshi, jambo hilo lazima likabidhiwe wale wenye uwezo wa kutayarisha njia ya kuelekea mji mkuu, kwa lengo la kuipindua serikali ya kihalifu na kusimamisha hukmu ya Kiislamu kwa Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume. Hili si gumu kwa Mwenyezi Mungu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Syria

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Syria
Address & Website
Tel: +8821644446132 Skype: TahrirSyria
www.tahrir-syria.info
E-Mail: media@tahrir-syria.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu