Afisi ya Habari
Tanzania
H. 21 Jumada I 1441 | Na: 1441 / 01 |
M. Alhamisi, 16 Januari 2020 |
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
KUKAMILIKA KWA KAMPENI YA “UKOMBOZI WA KONSTANTINOPOLI”
Hizb ut Tahrir / Tanzania imekamilisha kampeni ya Ufunguzi wa Konstantinopoli iliyo zinduliwa mwanzoni mwa mwezi huu na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, kama kampeni pana ya kiulimwengu kuadhimisha tukio adhimu la Hijria la Ukombozi wa Konstantinopoli (mji wa Heraclius) ambao ulizingirwa kuanzia 26 Rabii' al-Awwal hadi 20 Jumada al-Awwal 857 H sawia na 5 Aprili hadi 29 Mei 1453 M.
Kampeni hii ambayo iliendeshwa chini ya uongozi wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, (Mwenyezi Mungu amuhifadhi) kwa kauli mbiu “Bishara Njema Ikatimia… inafuatiwa na Bishara Njema Nyingine!” Kimsingi ilimakinika katika kufafanua yafuatayo:
1. Ukombozi huo unaonyesha utukufu wa Uislamu na Waislamu pindi Uislamu unapotekelezwa kivitendo, ukafiri utatoweka.
2. Kuwahakikishia Ummah wa Waislamu juu ya kutimia kwa bishara nyinginezo tatu za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kama ilivyo patikana ya mwanzo, ambazo ni kukombolewa kwa Roma, na nyingine mbili: kurudi kwa Khilafah kwa njia ya Utume, na kupigana na Mayahudi na kuwashinda kwa nguvu.
3. Kuwakumbusha Waislamu wajibu wa kufanya kazi kusimamisha tena Khilafah Rashidah, huku wakizingatia kuwa makafiri Wamagharibi, pamoja na makhaini waliweza kuivunja Khilafah mnamo 1342 H – 1924 M na wangali wanatia juhudi kubwa ili kuzuia kurudi kwa Khilafah wakitumia kila njia na mbinu.
Kampeni hii ilifanyika katika sehemu kadha wa kadha nchini Tanzania kama vile miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Zanzibar, Mtwara (Eneo la Kusini), Tanga (Eneo la Kaskazini Mashariki) nk., kwa kutumia njia na mbinu kadha wa kadha kama vile ugawanyaji hotuba ya Amiri kwa umma: darasa maalumu misikitini na nje ya misikiti, mihadhara, bayan, khutba za Ijumaa, kanda za video, mitandao ya kijamii pamoja na baadhi ya wanachama wa Hizb kuelezea maalumati ya kampeni hii katika vituo vya runinga na redio, kama vile Island TV, na Chuchu FM (Zanzibar).
Huku tukitoa shukrani zetu za dhati kwa wote walioshiriki au kuchangia kwa njia moja au nyingine katika kufanikisha kampeni hii, tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) tawfiq (mafanikio) yake tukufu na malipo makubwa.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |