Afisi ya Habari
Tanzania
H. 7 Jumada II 1440 | Na: 1440/04 |
M. Jumanne, 12 Februari 2019 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Pamoja na Kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Dhidi ya Ukatili wa Uchina kwa Waislamu Eneo la Mashariki Turkestan
Uchina kama taifa la kirasilimali haijihusishi tu kuzitumia kilafi rasilimali za kiasili za mataifa yanayo endelea hususan bara la Afrika na kulazimisha juu yao mzigo wa mikopo usio himilika, pia inatekeleza kampeni ya ghasia, vurugu na ukatili dhidi ya Uislamu na Waislamu wa Turkestan Mashariki, eneo ambalo lilivamiwa kinguvu na kutekwa na Uchina.
Ukatili wa Uchina kwa Waislamu ulio shawishiwa kupitia historia ya chimbuko lake kutoka kwa Himaya ya Manchu, ulitokea wakati wa enzi ya Ukomunisti na kwa sasa unatiliwa nguvu na vita vya kimataifa dhidi ya Uislamu na Waislamu ukitekelezwa na mataifa ya Kimagharibi hususan Marekani. Uchina kwa jumla ilishindwa kuuondoa na kuumaliza Uislamu kutoka katika ardhi yake wakati wa enzi ya Ukomunisti licha ya kampeni kali na katili ambayo hatimaye iliwapa nguvu Waislamu wa Uyghur kuulinda na kuuhifadhi Uislamu hata katika wakati mgumu.
Lakini, Uchina haijamaliza kiu yake ya damu ya Waislamu kutoka katika mauaji yaliyo tangulia, uvunjaji wa taasisi za Kiislamu ikiwemo Misikiti kwa maelfu, kuwauwa wanachuoni wa Kiislamu na mengi zaidi. Kwa sasa inatumia mbinu kadha wa kadha kufanya yayo hayo, kama kuwaritadisha kwa lazima, kuwadhalilisha kimwili na kiakili, kuwauwa, kuwatesa kwa kisingizio cha ugaidi na zaidi ya hayo kuwafungia katika kambi katili maalumu za wafungwa ikiwalazimisha kuachana na kitambulisho chao cha Kiislamu.
Mkakati wa Uchina wa kuanzisha kambi ili kuwafungia Waislamu ni jaribio la kuondoa fungamano la Waislamu binafsi pamoja na jamii yao na kuwaweka mbali na athari zao za kithaqafa, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu (swt) kamwe hawatafaulu. Licha ya ripoti ya Kamati ya Umoja wa Mataifa mnamo Agosti 2018, katika Jimbo la Xinjiang, kuna takriban kambi milioni moja za Waislamu za ugeuzaji dini (bbc). Lakini, kwa mujibu wa taarifa ya Muungano wa Kimataifa wa Vyuo Vikuu vya Kiislamu, idadi ya Waislamu katika kambi hizi iko katika mamilioni. (Yenisafak)
Ukandamizaji huu wa Uchina kwa Waislamu wa Uyghur unafanyika huku kukiwa hakuna uingiliajikati wowote wa maana wa kimataifa, ingawa kuna baadhi ya shutuma, lakini kiuhalisia ni taarifa tupu, za kuhadaa tu kilio cha kimataifa hususan Waislamu pasi na hatua zozote za kivitendo.
Mataifa ya Kimagharibi yakiongozwa na Marekani licha ya kuonekana kama yalio safu ya mbele katika kulinda 'haki za binadamu', lakini, uhalisia waashiria kuwa ulinzi sio kadhia inapokuwa ni mateso ya Waislamu. Tumeshuhudia mifano mingi ya mateso ya Waislamu kama vile nchini Afrika ya Kati, Myanmar, Kashmir, Ardhi ya Baraka – Palestina na kwingineko; hakuna hatua imara zinazo chukuliwa kuzuia hali hiyo. Ama watawala wa ardhi za Waislamu ambao walitarajiwa kuchangamka kwa njia ya kivitendo katika kuzuia na kukomesha uhalifu huu hatari mno, wamenyamaza kimya au hata kushirikiana na muuwaji (Uchina) wakitenda kwa njia za kijinga kwa kuwa haiwahusu.
Hizb ut Tahrir / Tanzania inashutumu unyama wa Uchina kwa Waislamu wa Uyghur na udhaifu wa watawala katika ardhi za Waislamu katika kukabiliana na uhalifu huu.
Kwa upande mmoja, tunasimama pamoja na kampeni ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir iliyo kwa anwani, "Vita vya Uchina Dhidi ya Uislamu eneo la Turkestan Mashariki Vitasitishwa na Khilafah Rashidah pekee" ili kufichua vitendo vya kinyama vya serikali ya Uchina na kimya cha ulimwengu wa Waislamu.
Tunawaombea ndugu na dada zetu wa Waslamu wa Uyghur nchini Uchina wadumu katika subra wakati huu wa ukatili. Tunawakumbusha Waislamu wote kuwa udhaifu wa watawala katika ardhi za Waislamu ni ishara ya kushindwa kwao kusimamia mambo au kuulinda Ummah wa Kiislamu, tunawasihi kama kaka zetu na dada zetu wa Waislamu kufanya kazi na Hizb ut Tahrir / Tanzania ili kusimamisha tena dola ya Khilafah ili kuwakomboa Waislamu wa Turkestan Mashariki na kwingine kila mahali. Tunawaomba Waislamu wote na wote walio na utu nchini Tanzania na kwingineko kushiriki katika kampeni hii tukufu ili kufichua unyama wa Uchina dhidi ya Waislamu wa Uyghur eneo la Turkestan Mashariki.
Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Tanzania |
Address & Website Tel: +255778 870609 |
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz |