Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  22 Sha'aban 1437 Na: 1437 / 02
M.  Jumapili, 29 Mei 2016

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Mabunge ya Kidemokrasia ni Taasisi za Kijambazi

Serikali ya Tanzania imemfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga kwa madai ya kufika Bungeni huku akiwa mlevi ambapo ilimfanya kushindwa kujibu vyema maswali ya Wabunge wakati wa kikao cha bajeti.

Sababu iliyo nyuma ya kufutwa kazi Kitwanga yaweza kusemwa kuwa ni kituko na kupuuziliwa mbali na kila aliye mchunguzi makini. Kadhia ya ulevi yaweza kuchukuliwa kama baraka iliyofichika kwani anadaiwa kuhusishwa na Kashfa ya Kampuni ya Lugumi ya Tsh 37 bilioni. Kampuni iliyopewa zabuni ili kuweka mashini 108 za kunakili alama za vidole kielektroniki katika vituo vya Polisi.  

Licha ya asilimia 99 ya malipo tayari kuwa yamefanywa, ni vituo vichache pekee ambavyo vimewekwa mashini hizo.

Lakini, lengo lolote litakalo kuwa nyuma ya kufutwa kazi Waziri huyu, ukweli ungali uko wazi kwa kila mmoja, kuwa Bunge la kidemokrasia licha ya kupewa hadhi ya juu kama taasisi takatifu ya utungaji sheria, kuhesabu watawala, kupitisha mikataba, nk. Mabunge haya si chochote isipokuwa ni magenge ya wafisadi.

Tumeshuhudia mifano mingi ya kijambazi katika Mabunge kama vile Wabunge kupigana wao kwa wao, kuzuliana urongo, kutoa taarifa za ubaguzi, hata wengine kwenda zaidi na kulingania kuhalalishwa kwa bangi, ukahaba na machafu mengineyo. Ilhali hilo ni tabaka la wasiogusika, lenye mishahara mizuri zaidi na kufurahia hifadhi kamili ya kisheria. Kwa tukio la kufutwa kazi huku, Spika wa Bunge Job Ndugai aliweka wazi kuwa wabunge wengi wanajihusisha na ulevi na madawa ya kulevya kupindukia ikiwemo bangi, ambapo alipendekeza mpango wa kuanzishwa kwa uchunguzi wa lazima wa matumizi ya pombe na madawa ya kulevya kwa Wabunge wote.

Misingi ya tabia hizi za kijambazi za Wabunge na ufisadi wote katika mujtama wowote wa kirasilimali inatokana na fikra ya usekula na 'uhuru'. 'Usekula' kama fikra msingi ya urasilimali inamtenga Mwenyezi Mungu kutokana na siasa na mambo ya dola, badala yake imemuachia dori yake ndani ya nyumba za ibada pekee. Huku, 'uhuru' kama nguzo ya demokrasia ukiwasukuma na kuwashajiisha watu kutenda chochote kinacho kuja akilini mwao kwa kuitikia kufurahia ule unaoitwa uhuru. Matokeo ya fikra zote hizi mbili hususan (usekula) Mwenyezi Mungu kutengwa na kuzuiwa kutokana na mambo ya dola, ni kuacha mwanya unao jazwa kwa matamanio, nidhamu za kutungwa na wanadamu, sheria na watu kuzungukwa na matamanio yao wenyewe katika vitendo vyao.

Kutokana na haya na kutokana na umbile la demokrasia, kamwe si ajabu kwa Wabunge kujihusisha na vitendo viovu, kwani Mabunge yao yanatabanni mfumo wa Urasilimali ambao umeweza kutekeleza uhalifu mkubwa zaidi wa kutotekeleza Sheria za Muumba katika maisha ya wanadamu. Sasa tunatarajia nini kwa wafuasi wa urasilimali?

Kwa ufupi, Urasilimali pamoja na fikra yake msingi ya usekula, pamoja na nguzo zake za uhuru umewatia wanadamu katika ghasia na kuwapotosha kupitia kuwageuza kuwa watumwa wa matamanio yao wenyewe. Uislamu pekee ndio unaoleta ukombozi wa kweli kwa wanadamu kupitia kuregesha wadhifa wao asili kama watumwa wa Mwenyezi Mungu na kutekeleza Sheria Zake katika mambo yote ya maisha.

 (أَرَأَيْتَ مَنْ اتَّخَذَ إِلَهَهُ هَوَاهُ)

“Je! Umemwona aliye yafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake?” [25:43]

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu