Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  11 Rabi' II 1442 Na: 1442/20
M.  Alhamisi, 26 Novemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mgogoro Huu Umeundwa na Serikali Iliyopo ... Tunawezaje Basi Kutarajia kuwa Suluhisho Litatoka Kwake?!

(Imetafsiriwa)

Maeneo mingi katika mikoa yote ya kusini mashariki na kusini magharibi mwa Tunisia, hadi mkoa wa Sfax, yanashuhudia uhaba wa chupa za gesi ya nyumbani, ambayo inasababisha madhara makubwa kwa watu, haswa katika hali hizi za baridi, hadi tumefikia kusikia mwaka 2020 kurudi kupika chakula kwa kutumia kuni!!

Katika kila mgogoro ambao serikali ya Tunisia unashuhudia, sababu zake zinachangiwa na kukaa kwa vijana wanaodai haki za kimsingi za maisha na kupinga sera za kutengwa kwa utaratibu, umaskini na utunzaji duni. Ambapo, hatua ambayo ilifanyika katika kiwango cha eneo la viwanda la Gabes - eneo linaohusika na uzalishaji karibu asilimia 40 ya mahitaji ya nchi ya gesi ya nyumbani - ilianza mara tu baada ya hotuba ambayo Waziri Mkuu Hisham El Mechichi alitangaza matokeo ya suluhisho la kukaa kwa El Kamour, ingawa serikali hii na serikali zilizotangulia wao wanatia saini makubaliano haya na vijana wa El Kamour, Gabes, Redeyef, Sbikha na maeneo mingine na kutoa ahadi za uwongo na wanachukulia haya kuwa ni mafanikio!!

Serikali yenyewe ndiyo ya kwanza kukanyaga maamuzi na ahadi za hapo awali, na ndio inayosababisha mvutano na ghadhabu nchini kwa marefu na mapana.

Ikiwa hivi ndivyo ilivyo, ni kipi kimesalia kwa serikali hii isipokuwa kitengo chake cha usalama ambacho kinashughulikia kulinda kampuni zinazopora utajiri pekee? Je! Kamwe Serikali inawezaje kuhalalisha uwepo wake kwa watu wa Tunisia?!

Na ikiwa serikali hawapi watu gesi na petroli, na inakata kutoka kwa mishahara ya maskini kusaidia bajeti yake, na inathibitisha hili kwa kuhamasisha vijana bila ya kupanga kutoa mahitaji ya kimsingi ya maisha bora, basi ni kwa uso gani waziri mkuu pamoja na aliyeleta katika mamlaka wanazungumza juu ya "mpango wa utawala" na "mradi wa serikali za mitaa" na kadhalika miongoni mwa orodha ya maneno matupu?! Bali baya zaidi, ni jinsi gani watu hawa wanadharau akili za watu na wanazungumza juu ya kukamilisha njia ya kidemokrasia iliyofilisika, na juu ya ushuhuda wa Benki ya Dunia na vitengo  vya kigeni kwao kwa hilo?

Ikiwa umasikini, ukosefu wa ajira, uhaba wa rasilimali, na kukazwa kwa visu kwa wafanyabiashara na ushuru mkubwa ndio ukuaji wa kiuchumi ambao serikali inautaka, tabaka duni la kisiasa linalouunga mkono na miradi ambayo wameahidi kwayo watu wa kawaida, basi maangamivu yawe kwao, miradi yao bandia, na ukuaji wao wa kiuchumi wa kirongo.

Hakika ukweli uko wazi hauna vumbi juu yake, na hakika imedhihirika wazi kwa watu wa Tunisia kwamba kundi la watawala ndio walengwa tu wa kufaidika, wafanyabiashara, na wawekezaji, ambao hawajali isipokuwa tu maslahi yao, na wala hawajali maswala ya watu, nchi yao iliyotekwa nyara, utajiri wao ulioporwa, au mateso yao ya kila siku, hakika serikali hii umekuwa mzigo kwa watu wa Tunisia na inamlinda adui yao, na huwaibia kheri zao, na wala haletea chochote isipokuwa misiba, majanga na maafa.

Basi Enyi Watu wa Mapinduzi wa Tunisia:

Mgogoro huu umeundwa na serikali iliopo, tunawezaje basi kutarajia kuwa suluhisho litatoka kwake?!

Rasilimali katika Uislamu ni mali ya umma, na hii ndio asili, kwa hivyo mfumo wa kirasilimali uliopo utakubali hili? Bila shaka hapana.

Vitendo vya watawala nchini Tunisia vinathibitisha ukweli wa mwenendo wao kuwa ni abiria wa wakoloni, kumuasi Mwenyezi Mungu na kuachana na hukmu zake za kisheria. Hakika hilo halitawarithisha watu wake isipokuwa maisha ya dhiki na hasara duniani kabla ya Akhera.

Hakika jukumu la dola ni kuwatunza watu kwa dhati na rasilimali na utajiri ulio chini ya udhibiti wao, ambayo ni haki ya kimsingi kwao, na lazima pia iwapatie utajiri huu kwa umbile la kihakika, sio kupoteza mali na vyanzo vyake na kuitunuku Magharibi, kisha kukusanya kutoka kwa watu matumizi yake na mzigo wa madeni yake, kisha kuwakumbusha ukarimu wao wa kile wanachopokea kutoka kwa makombo ya mezani na mafanikio ya uwongo ambayo hawayahisi kihakika, mpaka ikawa kati ya watu wa Tunisia wanakula majalalani! Mtume (saw) amesema:

«اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَاشْقُقْ عَلَيْهِ، وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَرَفَقَ بِهِمْ فَارْفُقْ بِهِ»

 “Ee Mwenyezi Mungu, yeyote anayewajibika chochote katika amri ya umma wangu, na akawa mkali kwao, basi kuwa mkali kwake, na yeyote anayewajibika chochote katika amri ya umma wangu, na akawa mpole kwao basi kuwa mpole kwake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu