Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  26 Jumada I 1442 Na: 1442/25
M.  Jumapili, 10 Januari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Al Mishishi Anafuata Mienendo ya Wale Waliokuwepo Kabla Yake
(Imetafsiriwa)

Baada ya nia ya kufungua mazungumzo na Muungano wa Ulaya juu ya makubaliano ya "ALECA", Waziri Mkuu Hisham Al-Mishishi mnamo Ijumaa 08 Januari 2021 M, alielezea ujumbe wa IMF, kupitia teknolojia ya mawasiliano ya mtandaoni, utayari halisi wa kuanza njia ya mageuzi ya kimuundo. Wakati wa mkutano huo, ambao ulihudhuriwa na Waziri wa Uchumi, Fedha na Msaada wa Uwekezaji, Ali Al-Kali na Mshauri wa Kiuchumi kwa Waziri Mkuu Abdel Salam Al-Abbasi, ilikubaliwa kuanzisha mpango wa mageuzi ya kiuchumi.

Mtu anaweza kuuliza: Je! Mageuzi haya yanayodaiwa ni pamoja na kupatikana kwa utajiri ulioibiwa na kuzinduliwa kwa miradi kabambe kama vile viwanda na kilimo cha kimkakati ambacho kinafikia usalama wa chakula kwa watu wa Tunisia?! Au ni kukamilika kwa programu iliyobaki ya mageuzi ya muundo ambayo ilibuniwa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa na ambayo serikali za baada ya mapinduzi ziliahidi kutekeleza kupitia barua ya kwanza na ya pili ya dhamira mnamo 2013 na 2016 na kusababisha mtaji wa benki za umma, uhuru wa benki kuu, kuvuliwa kwa hali ya mkono wake wa fedha, kuporomoka kwa kiwango cha sarafu, gharama kubwa ya maisha, kuongezeka kwa madeni na upungufu wa mizani ya kibiashara, ukosefu  mkubwa wa ajira, na ukosefu wa maendeleo, pamoja na kuelekea katika kupoteza kile kilichobaki katika uwezo wa watu wa Tunisia chini ya jina la kubinafsisha sekta ya umma?

Je! Tunaweza kusubiri kitu kutoka kwa waziri mkuu ambaye huwa anajadili ili kuimarisha Mkataba wa Uhusiano na Muungano wa Ulaya, ambao ulihitimishwa na Rais wa zamani Ben Ali mnamo 1995 na kusababisha uharibifu wa muundo wa viwanda vya Tunisia, na kutabiri uharibifu wa kilimo na tishio kwa usalama wa chakula wa Tunisia? Je! Mageuzi ya kimuundo anayosema sio utekelezaji wa kile kilichobaki cha maagizo ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, ambao Waziri Mkuu aliusifu uhusiano nao kuwa wa kistratejia?

Hakika migogoro ya kiuchumi ambayo Tunisia inakabiliwa nayo haiwezi kutatuliwa kupitia mageuzi yanayosimamiwa na duara za Kimagharibi na mikono yao ya kifedha, wala haiwezi kutatuliwa na viraka nusu kwa msingi wa na mfumo wa kirasilimali uliosababisha migogoro hiyo.

Suluhisho lazima liwe katika kitovu cha mfumo wa Ummah na mradi wake wa hadhara. Katika Uislamu, nidhamu ya kiuchumi inaweza kutoa maisha adilifu ya kiuchumi bila migogoro chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, na wanasiasa na wanafikra na maoni lazima wazingatie badili hii pekee ya kihadhara ambayo ndio wokovu wao na wokovu wa Ummah wao.

[فَمَنِ اتَّبَعَ هُدَايَ فَلا يَضِلُّ وَلا يَشْقَى وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً]

“basi atakaye ufuata uwongofu wangu, hatapotea wala hatataabika * Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki.” [Ta-Ha: 123-124].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu