Ijumaa, 24 Rajab 1446 | 2025/01/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Tunisia

H.  29 Jumada I 1443 Na: 1443/15
M.  Jumapili, 02 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Sheria ya Fedha ya Rais Inachipuza Kutoka katika Chanzo Kile kile cha Utawala wa Zamani
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumanne, 28/12/2021, Waziri wa Fedha, Siham Boughediri Namsiyah alitangaza wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu bajeti ya serikali ya mwaka wa 2022, ambayo ilitolewa na amri ya rais iliyojumuisha sura za Sheria ya Fedha ya mwaka wa 2022, alikadiria nakisi kuwa dinari bilioni 8.548. Alisema, "Dola ya Tunisia itahitaji mikopo ya ziada yenye thamani ya dinari bilioni 19.9, ikijumuisha dinari bilioni 12.6 kutoka nje ya nchi na dinari bilioni 7.3 kutoka ndani ya nchi." Ili kuhalalisha Tunisia kuuendea Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kwa mara nyingine tena, badala yake, kutangaza furaha yake kwamba Tunisia itaingia katika mazungumzo na IMF hivi karibuni!

1- Kukabiliana na kuendelea kuichezea Tunisia na uwezo wake, sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia tunataka kufafanua kwa rai jumla yafuatayo:

Amri hii inakanusha madai ya rais kwamba kuna awamu mpya na fikra mapya. Serikali ya rais huyu iliyo na sheria hii ya fedha inafuata njia ile ile ambayo serikali mtawalia zimefuata nchini Tunisia tangu ilipokuwa chini ya Mamlaka ya Tume ya Fedha, ambayo dola hii haijaondoka kutokana nayo hadi leo. Fikra yake mpya iko wapi basi? Na "matakwa ya watu ..." yako wapi? Au ni kujificha tu na udanganyifu.

2- Sheria ya Rais ya Fedha si chochote ila ni orodha ndefu ya kodi zisizo za haki na kandamizi, kwani mapato ya kodi yamechukua sehemu kubwa zaidi ya mapato yanayotarajiwa katika bajeti ya 2022, ambayo yamefikia takriban dinari bilioni 38.618, na thamani inayokadiriwa ya dinari bilioni 35.091, akibainisha kuwa kiasi cha deni kilipanda hadi kiwango kipya cha rekodi kikifikia dinari bilioni 100 (dolari bilioni 30.3), kikiwakilisha asilimia 90 ya Pato la Taifa. Hii ni bajeti nyingine, ambayo inalenga kuwaadhibu mamilioni ya wananchi wa Tunisia kwa kuchimba mifukoni mwao, hivyo kubaki - kama kawaida - chanzo kikubwa cha mapato ya serikali, huku wakiteseka kutokana na mfumko wa bei na bei za juu za bidhaa msingi! Yako wapi madai ya rais ya kurudisha pesa za wananchi kutoka kwa wezi?!

3- Marekebisho yaliyopigiwa debe na Rais na serikali yake ni ishara ya mapenzi kwa Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, adui wa watu, na kimsingi yamejengwa juu ya masharti yake ya kidhulma: kushuka kwa thamani ya dinari dhidi ya fedha za kigeni, kuondoa ruzuku, kuuza taasisi za umma, na kuwafungia watu mishahara.

Kushuka kwa thamani ya dinari kutaongeza kuchochea bei nyingi za vifaa vilivyohamishwa, na kuinua ruzuku ya mafuta kutasababisha kuongezeka kushuka kwa uchumi, huku wazalishaji wakiondoka kutoka kwa mzunguko wa uzalishaji pindi gharama ya uzalishaji inapoongezeka, pamoja na ukweli kwamba kufunga mlango wa mgawo katika afisi ya umma kutawanyima mamia ya watu wanaoota ndoto walio na digrii za juu haki yao ya kufanya kazi. Na hakutakuwa na suluhisho kwa serikali isipokuwa kuuza taasisi za umma au kuomba milangoni mwa afisi za balozi kwa matumaini kwamba itapata mkopo wa riba ambayo itaongeza zaidi majanga yake.

Enyi watu wetu waheshimiwa nchini Tunisia,

Munaadhibiwa kwa ajili ya mapinduzi yenu, na wakati huu adhabu inakujieni kutoka kwa rais aliyevalia kama wanamapinduzi wacha Mungu, na kudai kuwa anapigana na wezi ili kuregesha pesa zenu zilizoporwa, lakini akapitisha sheria ya fedha ya 2022 ambayo inalenga tu mifuko yenu kuikamua kile kilichobaki ndani yake kwa faida ya duara za waporaji wa kigeni, na katika utabikishaji wa sera zao haribifu kwa uchumi wa nchi hii.

Moja ya mambo hatari zaidi tunayokabiliana nayo leo nchini Tunisia ni uharibifu na utumwa unaoletwa na bajeti hii, na kuongezeka zaidi kwa kiwango cha deni la riba, huku Rais Kais Saied akiipotosha rai jumla juu ya mabadiliko, na kutuongoza kukubali masharti ya duara za kikoloni. IMF na matagaa yake, na huku akihubiri kuhusu ubwana wa nchi, anatia saini kifungo chetu cha utumwa, na huku wezi wanaokaa katika Bunge la Bardo wakitoa vitisho, yuko kimya kuhusu wezi wakubwa walioiba na wanaoiba mali zetu kila siku.

Enyi watu wetu waheshimiwa katika Zaytouna nchini Tunisia,

Je, sisi si Waislamu kutoka katika Ummah wa Muhammad (saw)? Je, Mwenyezi Mungu (swt) hakutuletea Dini ili kutukirimu? Kwa nini tunadhalilishwa kwa kuwaomba na kuwasihi maadui zetu?! Je, katika sheria za Uislamu wetu mtukufu hakuna suluhisho la matatizo yetu? Sheria zao duni zilizotungwa na wanadamu zina umuhimu gani kwetu?!

Wakati umewadia sasa kwetu tukabiliane na upuuzi huu wa kirasilimali wa kisekula, usiotimizi ahadi zake nasi, na kuelekea katika utabikishaji wa hukmu zilizoteremshwa na Mwenyezi Mungu za Kiislamu ambazo zina tiba ya matatizo yetu yote. Hakuna maisha bila ya Uislamu, hakuna hadhi bila ya Uislamu, na hakuna heshima isipokuwa kwa Uislamu na hukmu zake zinazotabikishwa na dola ya halisi, ambayo ni dola inayomrithi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), katika kusimamia mambo ya watu kwa Uislamu, utunzaji ambao utawapa utu na utukufu, sio kudhalilishwa, kuchukiwa na kushambuliwa na mataifa.

 (وَلِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ)

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanaafiki hawajui.” [Al-Munafiqun: 8].

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tunisia
Address & Website
Tel: 
http://www.ht-tunisia.info/ar/

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu