Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  1 Rajab 1445 Na: 1445/19
M.  Jumamosi, 13 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Umbile la Kiyahudi ni Kivuli cha Tawala za Kiarabu. Kitu Kinapotoweka, Kivuli Chake pia Hutoweka
(Imetafsiriwa)

Kama kawaida ya kila Ijumaa, mnamo Ijumaa tarehe 12/1/2024 Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia iliandaa matembezi ya kuinusuru Gaza. Yalianza mbele ya Msikiti wa Al-Fatah kuelekea ukumbi wa michezo wa manispaa katika mji mkuu. Kauli mbiu ya Matembezi ya Ijumaa hii ilikuwa “Umbile la Kiyahudi ni Kivuli cha tawala za Kiarabu. Kitu Kinapotoweka, Kivuli Chake pia Hutoweka Lakini inaonekana kana kwamba jina anwani hii haikuwa ya kupendezwa na mamlaka nchini Tunisia, na kwa hivyo vikosi vyake vya usalama vilishambulia Matembezi hayo na kuliondoa bango lililoonyesha anwani hiyo. Kwa nini?!

1- Tawala hizi za Kiarabu ndizo zilizosimama na kutazama, na bado zinaendelea kutazama jinsi magenge ya Kiyahudi yanavyowaua watu wa Palestina. Wanaunga mkono hata magenge ya Kiyahudi katika kuwaua. Vyenginevyo, ina maana gani kwamba siku 100 za mauaji zimepita na tawala hizi hazikufanya lolote?! Badala yake, baadhi yao wanasubiri ruhusa kutoka kwa Marekani, Uingereza, au umbile la Kiyahudi ili kufungua vivuko au kupitisha makombo ya misaada!

2- Tawala hizi za Kiarabu, zikiwemo mamlaka za Tunisia, ni vijidola vilivyoundwa na Wafaransa na Waingereza katika Makubaliano maovu ya Sykes-Picot baada ya kuvunjwa dola ya Waislamu, Dola ya Khilafah 1924 M.

3- Tawala hizi za Waarabu ni ndugu pacha wa magenge ya Kiyahudi; zote mbili ziliundwa na duara za kikoloni za Uingereza na Ufaransa.

4- Tawala hizi za Kiarabu na umbile la Kiyahudi, zote mbili zilizuka ili kuusambaratisha umoja wa Waislamu, na zote mbili zilizuka ili kuwatesa Waislamu na kuwafanya watumwa na watiifu kwa wakoloni wa Magharibi.

5- Tawala hizi za Waarabu ndizo ambazo kihistoria zimelilinda umbile la Kiyahudi. Vita vya 1948, 1956, 1967, na 1973 vilikuwa tu kwa ajili ya kuliimarisha zaidi umbile la Kiyahudi na kuwagawanya Waislamu.

Huu ni baadhi ya ukweli ambao kila mtu anaujua kuhusu tawala za Waarabu, ikiwemo Tunisia, ambayo inasimama pembeni na kutazama Marekani na Uingereza zikizunguka anga za nchi za Kiislamu, zikimshambulia kwa mabomu wamtakaye, kumuangamiza yeyote wanayemtaka, na kumchinja yeyote wamtakaye miongoni mwa Waislamu nchini Palestina.

Je ukweli unakukereni kiasi hiki?! Je ukweli wenu ni mchungu sana?! Je, sio wakati sasa wa nyinyi kuamka na kutambua kwamba tawala hizi, ukiwemo utawala wa Tunisia, si chochote ila ni pacha wa umbile la Kiyahudi? Je, mtaendelea kuwalinda?!

Je, haujafika wakati sasa wa nyinyi kusimama upande wa haki, upande wa Ummah wenu, Dini yenu, na nchi yenu?! Je, sio wakati sasa wa nyinyi kuvunja vikwazo na mipaka?!

Enyi Majeshi: Hatukwambiini muwaokoe watu wa Gaza, kwani wao wako katika heshima isiyo na kifani. Badala yake, tunakuambieni kuiokoa heshima yenu, kuokoa uanaume wenu, ambao umechezewa na vibaraka wa kikoloni. Je! hakuna mtu miongoni mwenu mwenye akili?!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu