Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  17 Rajab 1445 Na: 1445/22
M.  Jumatatu, 29 Januari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mamlaka nchini Tunisia Inakiuka Matukufu na Kuwashambulia Wanawake!
(Imetafsiriwa)

Ijumaa jioni, Januari 26, 2024, katika mji wa Hammamet, kikosi kikubwa cha usalama kilivamia nyumba ya mwanamke mmoja miongoni mwa Shabab wa Hizb ut Tahrir, na kuingia kwa nguvu bila ruhusa. Polisi walijaribu kuwakamata wanawake na kuwapeleka katika eneo la usalama kwa uchunguzi, lakini wanawake hao walikataa na walipendelea kwenda kwenye vituo vya usalama kwa njia zao wenyewe. Walihojiwa kwa muda mrefu, kisha wakaachiliwa huru ili kufika mbele ya mahakama mnamo Jumatatu, Januari 29, 2024.

- Mamlaka hii, ambayo kiongozi wake anadai kufuata nyayo za Umar ibn al-Khattab, haijafikia viwango vya maadili vya Abu Jahl! Uwepo mkubwa wa askari polisi waliofika katika nyumba hiyo hawakuwa na maadili na heshima, wakijiruhusu kuwashambulia wanawake na kuvamia bila aibu nyumba ambayo mmiliki wake alikuwa alikuwa mwenyeji wa dada zake. Je, huu sio uhalifu au angalau tuhuma inayostahili kuchunguzwa na kuhukumiwa?!

- Sababu pekee ya uvamizi huo wa polisi ni kwamba inahusu Hizb ut Tahrir. Je, kuwa mwanacha wa Hizb na kufanya kazi ndani ya safu zake ni uhalifu unaostahili kuvamiwa na kuwatia hofu wanawake na watoto?!

- Je, mamlaka iliyonyimwa uhalali inapata madhara gani ikiwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir wataendelea kueneza dawah yao?! Na nini kinawatia hofu kwa wanawake wachache kukaa majumbani mwao wakisoma Quran?!

- Au ni mbinu mpya ya zamani dhidi ya Hizb? Tukio hili halikuwa la kwanza na halitakuwa la mwisho, kuthibitisha kwamba mamlaka hii imekatwa kutoka kitambaa kile kile kama watangulizi wake kutoka kwa serikali za taabu na uharibifu tangu Bourguiba, Ben Ali, na Essebsi. Wasiwasi wao ni kuwafuatilia wabebaji dawah ya Kiislamu, kuwakagua na kuwavamia wakati wowote, na kuwatisha wao na familia zao.

- Tukio hili sio kitendo cha mtu binafsi au mpango wa usalama wa ghafla; bali, ni hatua ya makusudi na sera iliyoamriwa na dola za kikoloni kutoka ng'ambo na kutekelezwa na mamlaka ya Tunisia dhidi ya Hizb ut Tahrir ili kuzuia shughuli zake. Kwa hiyo, tunaiambia mamlaka hii duni:

- Hamna kitu chochote kwani tunajua kuwa upinzani wenu kwa Hizb ni katika kuwatumikia mabwana zenu wa Kimagharibi tu, ambao ndio pekee wenye nia ya kuuondoa Uislamu maishani na kuzuia kurudi kwa Khilafah. Dola inayowaunganisha Waislamu na kuwakusanya dhidi ya maadui zao.

- Tunaiambia mamlaka hii haramu ijue mahali pake na isidanganywe na kimya cha muda mfupi cha watu kwake. Tunaiambia kwamba ikiwa uhalali wake unapatikana kupitia udanganyifu na ukwepaji, basi uhalali wetu unatoka kwa Mola wa walimwengu. Katika Hizb ut Tahrir, tumetoa kiapo kwa Mwenyezi Mungu kufanya kazi ya kusimamisha Shariah ya Mwenyezi Mungu na kung'oa kabisa ukoloni na vibaraka wake katika ardhi zetu. Jueni kwamba kukaza kwenu mshiko kwa Hizb na shughuli zake hakutazuia Mashababu wake kulingania kwenye haki, kwenye Dini ya Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu, na kutekeleza sheria Zake. Ukandamizaji wa polisi hautawazuia kufanya kazi na Ummah kuikomboa Tunisia na ardhi zote za Kiislamu kutoka kwa utawala wa makafiri wa Magharibi wanaokutumieni.

Na mamlaka hii ya aibu ijue kwamba mizizi ya Hizb ut Tahrir imeenea kwa kina katika ulimwengu wa Kiislamu, na ulinganizi wa Khilafah umekita mizizi. Hakuna dhalimu atakayeweza kuizuia kufikia lengo lake, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu