Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  16 Muharram 1442 Na: 1442 H / 02
M.  Ijumaa, 04 Septemba 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ni Nani Atakayeihami Heshima ya Muhammad (saw)?
Masekula wenye chuki wanaendelea kupatiliza fursa ya kuwepo na ombwe la uongozi wa kisiasa wa Kiislamu ulimwenguni leo

Kila mara watetezi wa chuki ya usekula hudai haki yao ya kuwatusi Waislamu kupitia uchomaji nakala zilizo chapishwa za Qur'an na kuchapisha vikaragosi vinavyomkejeli Mtume Muhammad (saw). Umbo halisi kwa wale wanaoshikamana na batili, wakijua fika kwamba kamwe hawana uwezo wa kifikra wa kupambana na imani ya Kiislamu, achilia mbali kuhami mfumo wao wenyewe batili. Katika historia yote tumeshuhudia majaribio yasiyo na idadi ya wafisadi hao, ambao riziki zao zinategemea ufisadi na unyanyasaji na mateso ya wengine, kuichafua sifa ya Mitume wa Mwenyezi Mungu (AS), kwa matarajio ovyo kwamba wataweza kuepuka kufichuliwa kwa ufisadi wao mbele ya watu wa kawaida. Mitume walisema kweli kwa watu wao, wakiwalingania katika haki na maisha mazuri, huku kipote cha wafisadi wakiwapinga, kuwatusi na kuwachafulia majina kwa uongo wao muovu.

Mtume wetu Muhammad (saw), ambaye ni heshima yetu, ndiye Nabii wa mwisho kabisa kwa wanadamu wote. Ujumbe wake wa Uislamu una kipimo cha haki kwa vitendo vyote leo, iwe vya kibinafsi, kijamii, kiuchumi, kimahakama, au kisiasa. Masekula leo hawana uthibitisho wa imani yao batili, kwa hivyo wanaushambulia Uislamu na kujaribu kuukashifu. Lakini kwa kufanya hivyo, wanafichua tu kutokuwa na tumaini kwao katika kupambana na dalili za kiakili za Uislamu, na kutukana jamii ya Waislamu kote ulimwenguni.

Hili linaonekana kuwa lengo la kimakusudi, kwani ni sehemu tu ya mwendelezo wa sera za vyombo vikuu vya habari na serikali. Wanaongoza njia kwa ajenda zao zinazoongozwa na chuki kwa kutoa dhana kwamba Waislamu hawana chochote cha kutoa kwa ulimwengu isipokuwa ufisadi; haswa kwa sababu mfumo wao wa kirasilimali wa kiulimwengu ndio chimbuko la taabu na ufisadi wote ulimwenguni leo, na wanataka kupotoa umakini wa watu mbali na ukweli huo. Watetezi duni kisha wanafuata nyayo, ima kwa kumwaga hasira zao mitaani, mtandaoni au kwa kuchapisha, au hata kuchukua silaha dhidi ya waabudu wasio na hatia misikitini. Ajenda ni moja na hiyo hiyo.

Lakini sisi hawa hapa tena, bado hatuna uongozi wa dhati wa kisiasa ambao unatekeleza Shariah ya Kiislamu na kuulingania ulimwengu kwa haki na mwongozo wa Muhammad (saw). Badala yake, viongozi wote katika ulimwengu wa Kiislamu kwa uoga wanakubali tamaduni za kimataifa kama zinavyoagizwa na Magharibi, hawawezi kutoa upinzani hata dhaifu kutetea heshima na hadhi ya Waislamu na Nabii wao. Hawako hata tayari kutetea maisha ya wanawake na watoto ambao wanachinjwa jirani yao, kwa hivyo kuna matumaini gani kwamba wanaweza kupata ujasiri wa kutoa changamoto kali kwa wale ambao wanathubutu kumdhihaki Nabii Muhammad (saw). La kusikitisha, watu wengine huanguka katika mitego ya Magharibi, bila kujua ukubwa na mizizi halisi ya tatizo, kwa hivyo huyachukua mambo mikononi mwao, na daima huharibu zaidi kuliko kutengeza.

Mwenyezi Mungu hakuwaacha wanadamu bila mwongozo kwa maana hiyo alimtuma Muhammad (saw) kutuongoza. Yeye hakutuacha tusahau ujumbe Wake wa mwisho kwa wanadamu wote, kwani Alituma wabebaji wa Dawah kuubeba kote ulimwenguni. Yeye hakutuacha bila ya dola kuonyesha uadilifu wa Uislamu, kututetea sisi na heshima yetu, kwani Yeye alituma Makhalifa (khulafaa) wema kwa mfano mzuri wa kuigwa.

Kinachokosekana leo ni matakwa ya viongozi kusimama kwa umoja ili kupambana na wale wanaovuka mipaka. Kwa hali hiyo, na hadi sisi kama Ummah tutakapokusanyika pamoja kuregesha Khilafah kwa njia ya Utume, basi kipote cha warasilimali na wenye chuki ambao hufanya zabuni zao wataendelea kutumia udhaifu wetu; kwa usalama kwa kujua kwamba hakutakuwa na majibu madhubuti.

Tunawalingania Waislamu kufanya kazi kwa ajili ya Uislamu, kufanya kazi kwa ajili ya Khilafah, na kuwakomboa wanadamu.

Mnamo 2014, wakati ambapo kuwatusi Waislamu ilikuwa ni fesheni ya mwisho, wakati huo tulichapisha Taarifa kwa Vyombo vya Habari kulaani, kama ambavyo inapaswa kulaaniwa leo. Tafadhali isome

http://www.hizb.org.uk/media/press-releases/hizb-ut-tahrir-britain-denounces-the-republication-of-cartoons-insulting-prophet-muhammad/

Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu