Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  23 Safar 1442 Na: 04 / 1442 H
M.  Jumamosi, 10 Oktoba 2020

 

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Urasilimali Unafeli kwa Kila Kipimo: Ni Wakati Sasa wa Uchumi Mpya

Masikini wanazidi kuwa masikini wakati matajiri wanazidi kutajirika. Hii ni licha ya nyakati za machafuko tunayoishi ndani yake, ambapo uchumi wa ulimwengu umesababisha na bado unasababisha kushuka kwa uchumi na unyogovu.

Watetezi wa mfumo wa Kirasilimali wanatafuta njia za kuzungumzia juu ya uchumi, huku wakikadiria mateso ya watu. Hatua yao kuu ni pato la taifa (GDP), wakati watu wa kawaida wana ukosefu wa ajira, njaa, na taabu za kukabiliano nazo. Mtu angefikiria kuwa janga la maambukizi ya virusi vya korona lingekuwa ni wakati wa kuungana pamoja sio unyonyaji; lakini wakati maadili ya kisekula ya Urasilimali yanapoenziwa kwa heshima kubwa, kama ilivyo ulimwenguni leo, kubakia hai kwa wanaostahiki ndio zingatio pekee. Kwa kweli, wakati huo huo huku umasikini na uchochole vikiongezeka tena, mabilionea matajiri zaidi ulimwenguni wanauona utajiri wao ukiongezeka kwa angalau asilimia 25. Serikali zimethibitisha kwa mara nyengine tena kwamba hakuna "ujanja-chini" wa sera zao za kifedha, ambazo zimeundwa kimsingi kutunza kilabu cha kipote chao cha wafadhili matajiri.

Urasilimali ni mfumo unaowapendelea matajiri kuliko masikini, kwani unawapa wale walio na njia haki ya kutunga sheria kwa niaba yao, huku wakikana uwajibikaji wowote wa kweli kwa kila mtu mwingine. Sio bahati mbaya kwamba mabilionea hawalipi kodi, kwani wana nguvu ya kuuchezesha mfumo, kwa faida yao. Wale ambao hawawezi kumudu kucheza mchezo huu, ambao ni kila mtu mwingine, hubeba bili ya malipo.

Sasa kuna mazungumzo kati ya wanauchumi kuhusu kurekebisha mfumo wa kodi na kuufanya Urasilimali kuwa wenye ubinadamu zaidi, ambapo sio kweli. Kuongeza kodi ya utajiri kwa mzigo mzito wa kodi ambao tayari uko kunaweza kuwa maarufu kwa muda mfupi tu, lakini hakutashughulikia kimsingi tatizo hilo, ambalo ni ukosefu wa utulivu unaotokana na mfumo wa wizi ulioundwa na kipote cha wachache ambao hawana nia ya kurudisha nguvu halisi kwa watu. Uwajibikaji katika demokrasia ni ahadi tupu.

Urasilimali uko katika mgogoro na tabaka la warasilimali wachache wanajua hili. Kuwanyima watu wengi wa kawaida nguvu yoyote halisi, ambayo bila shaka itawaleta wafisadi kwenye haki na kumaliza udhibiti wao, itabakia kuwa ulinzi wao wa pekee; kwani hakuna njia ya kuutetea kifikra mfumo wa kisekula na nidhamu yake ya Kirasilimali. Maumbile ya kimabavu ya majibu ya serikali kwa janga la maambukizi ya virusi vya korona hayajafanyiwa uchunguzi wowote halisi, kwa njia ile ile ambayo pia mpango wa baada ya Brexit nchini Uingereza haujafanyiwa. Kwa kipote cha wafisadi wachache huu ni wakati wa kufanya mabadiliko kwenye mfumo ambao wanatumai utalinda msimamo wao katika siku zijazo zisizo na uhakika.

Kwa kila mtu mwingine, na haswa kwa Waislamu, huu ni wakati wa kuhoji kufaa kwa mfumo wa kisekula na muundo wake mbaya wa kiuchumi. Nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu ni nidhamu adilifu inayotanguliza mahitaji ya watu wote, sio anasa za matajiri. Kuhakikisha mzunguko wa utajiri ndio lengo msingi la uchumi wa Kiislamu, tofauti na Urasilimali. Lengo sio kukusanya utajiri mwingi, wala kukua kila wakati. Mahitaji ya kimsingi ya watu lazima yatimizwe kabla ya yote.

Tunawaalika kujisajili na kujiunga na Hizb ut Tahrir / Uingereza katika kongamano lake la kimataifa mtandaoni: Kurudi kwa Mfumo wa Kiulimwengu wa Kiislamu.

Wazungumzaji watahutubu mada zifuatazo:

Kutoka kwa Janga la Maambukizi hadi BLM: Wanadamu Wanatafuta Badali kwa Hamu

Uchumi Mpya, Usiotumikia Asilia Mia Moja

Nidhamu ya Khilafah, Utunzaji wa Watu

Kuasisi Uongozi wa Uislamu Duniani na Wajibu wetu

Jumamosi, 31 Octoba Saa Nane Mchana GMT

Jisajili katika

Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu