Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  1 Rajab 1442 Na: 09 / 1442 H
M.  Jumamosi, 13 Februari 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Miaka Mia Moja Bila ya Khilafah! Isimamisheni, Enyi Waislamu

(Imetafsiriwa)

Mwaka huu katika mwezi mzima wa Rajab, Hizb ut Tahrir ameandaa kampeni ya kiulimwengu kutanabahisha karne moja ya kuvunjwa kwa Dola ya mwisho ya Kiislamu, Khilafah mikononi mwa wakoloni. Mnamo tarehe 28 Rajab 1342 Hijria, kibaraka wa Uingereza Mustafa Kemal alifutilia mbali Khilafah baada ya kuwa kiongozi wa dola ya kisekula ya Kituruki.

Tangu siku hiyo Umma wa Kiislamu ulipoteza uongozi wake na kugawanyika mgawanyiko ambao haujawahi kuonekana; Ndugu na dada walilazimishwa kuishi katika dola tofauti za kitaifa ambazo wavamizi wa kikoloni na vibaraka wao walizibuni kwa haraka. Tangu wakati huo mfululizo wa marais, mawaziri wakuu na wafalme wameteuliwa kuwalazimisha watu kusalimisha rasilimali zao na ubwana wao kwa matakwa ya dola za kikoloni ng'ambo.

Khilafah ilikuwa ni dola inayoongoza ulimwenguni kabla ya kuanguka kwake na kuangamia kusiko tarajiwa. Ilikuwa na uwezo wa kubeba ulinganizi wa Kiislamu ulimwenguni, kuhami raia wake dhidi ya maadui zao, na kusimamisha utawala adilifu wa Uislamu Ardhini. Kisha tukapewa utaifa, usekula, ujamaa na urasilimali. Tangu wakati huo tumepitia udikteta, ufalme, uimla na demokrasia. Tangu wakati huo Umma umeteseka katika hali ambayo haijapatapo kuonekana.

Kwa miaka mia moja wakoloni wafisadi wamekuwa na utawala huru wa kuangamiza ulimwengu na watu wake. Maadui wa haki wameufanya ulimwengu mzima kuwa mahali penye mateso kuishi. Rushwa, uongo, utumwa, unyonyaji na mauaji yote yamehalalishwa katika mfumo wa kisekula ambao unatawala maisha yetu leo. Ingawa inaonekana kutowafaa karibu watu wote kwenye sayari hii, lakini hakuna mahali pengine pa wanyonge kugeukia kwa ajili ya hifadhi, mwongozo na usaidizi.

Pindi Khilafah itakaporudi kwa njia ya Utume, ulimwengu utakuwa na mwokozi wake. Wafisadi watakutana na adhabu yao, na madhalimu watahisabiwa.

Hili ndilo ambalo sisi katika  Hizb ut Tahrir tunalifanyia kazi mchana na usiku.  Tunaitaka, Khilafah kwa njia ya Utume. Tunasema miaka mia bila ya dola, bila ya Khilafah imetosha. Tunawaambia Waislamu; isimamisheni! Kuweni pamoja na wale wanaofanya kazi kwa ajili ya kuirudisha.

 [يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfaal 8:24]

#أقيموا_الخلافة

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#خلافت_كو_قائم_كرو

Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu