Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uingereza

H.  20 Safar 1444 Na: 1444 H / 01
M.  Ijumaa, 16 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
[فلا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ]
Basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi mkiwa nyinyi ni Waumini.” [Quran 3:175]

(Imetafsiriwa)

Waislamu na wasiokuwa Waislamu kwa pamoja walisusia ombi la kutapatapa la kukubaliwa lililoonyeshwa katika msikiti wa katikati mwa London wiki hii. Vyombo vya habari vilialikwa kutazama watoto wa Kiislamu wakilazimishwa kuimba wimbo wa taifa wa Uingereza, ingawa ni maombi ya kumuombe mfalme na ahifadhiwe, atutawale na kuwa washindi juu yetu.

Misukosuko ya Uingereza inafichuliwa kwa mara nyingine tena, huku nchi hiyo ikiwa katika mgawanyiko baada ya kifo cha Malkia Elizabeth II, na kukwea mamlaka kwa mtoto wake Mfalme Charles III. Wanasiasa na mashirika yenye kejeli wamejaribu kukaa sambamba na hisia ya hasara ya kibinafsi inayohisiwa na watu wengi wa kawaida, huku wakati huo huo uhalali wa ufalme, historia yake wa ukoloni na mustakabali wake yakiwa kwenye ndimi za wengine wengi. Wimbi la kihisia linalolikumba taifa hili limesababisha majibu yasiyo na shaka kutoka kwa wale wanaohisi kwamba Ufalme wa Uingereza haupaswi kujadiliwa kwa wakati huu, na pia kutoka kwa wale wanaohisi kuwa familia ya kifalme haipaswi kupata pasi ya bure.

Waliobanwa katikati ni jamii ya Waislamu, ambao kimsingi wanatoka katika wahanga wa ghasia na unyonyaji wa ubeberu wa Uingereza, alhali wanachukuliwa kama raia wa daraja la pili na wanaishi chini ya uangalizi wa mara kwa mara kwa dalili zozote za kutokuwa waaminifu kwa Uingereza au maadili yake.

Sera ya muda mrefu ya Uingereza ya kuwakandamiza Waislamu, kulazimishwa kuiga na kutekeleza unafiki haki yake iliyojitangazia ya uhuru wa kujieleza, ilimaanisha kwamba wachache katika jamii ya Kiislamu wamejaribu kuichumbia serikali na vyombo vya habari, mara nyingi wakipindisha maadili na kanuni za Kiislamu ili kukabiliana na propaganda hasi dhidi ya Uislamu. Majaribio kama hayo ya kuliwaza bila shaka yatabadilisha maadili matukufu ya Kiislamu kwa matamanio ya watu masekula. Shakhsiya ya adhimu ya Kiislamu hatimaye  itakoma kuwepo, baada ya kubadilishwa na mchanganyiko wa maadili ya kiliberali ya kimagharibi yaliyo kanganyikiwa na kuongana na baadhi ya matagaa ya Uislamu.

Vyombo vya habari na mashini ya Uhusiano Mwema wa umma ya ikulu iliweza kufanikiwa kusimamia sura ya marehemu malkia, kiasi kwamba Waingereza wengi walimwona sawa na bibi mwema wa taifa hilo. Walifanikiwa kidogo kuhusiana na wanawe, hata hivyo, ambao tabia zao za kashfa mara kwa mara zilijipenyeza kwenye macho ya umma, na kusababisha chuki kwa utawala wa kifalme na nafasi yake ya upendeleo.

Kushindwa kukubwa kwa mfumo wa kisekula na kielelezo chake cha kidemokrasia ni kwamba hauna kanuni na maadili madhubuti. Kila kitu kiko katika hali ya kubadilika badilika, ukiyumba pamoja na mihemko ya umma, ambayo taasisi za kirasilimali, wanasiasa na mashirika hujaribu sana kughilibu na kudhibiti.

Uislamu, kwa upande mwingine, haujakosa kanuni. Haki na batili haziamuliwi na umaarufu wake wakati wowote. Qur’an na mafundisho ya Mtume Muhammad (saw) yanatoa muongozo ulio wazi juu ya lipi ni zuri na baya.

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِن تَتَّقُوا۟ ٱللَّهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًۭا وَيُكَفِّرْ عَنكُمْ سَيِّـَٔاتِكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ﴿

Enyi mlio amini! Mkimcha Mwenyezi Mungu atakupeni kipambanuo, na atakufutieni makosa, na atakusameheni, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kubwa.” [8:29].

Mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu ndio mfumo pekee iliojengwa juu ya akili, wenye uthibitisho wa kiakili kwa imani yake msingi, na kanuni zilizo wazi za kisheria kwa hukmu zake za sharia. Kuwafurahisha masekula kwa maadili yao ya kiliberali ya kimatamanio kutaishia tu katika taabu, katika maisha haya na yajayo. Uislamu hauhitaji mabadiliko yoyote au marekebisho ili kuendana na ulimwengu wa kisasa unaobadilika kila mara. Licha ya shinikizo juu ya jamii ya Kiislamu kuingia ndani yake kimya kimya, Waislamu wa Uingereza wanahitaji kusimama ili kuelezea usahihi wa Uislamu na upotovu wa mfumo wa maisha wa kisekula iwe wa kijamhuri au ufalme wa kikatiba.

[وَلَا تَلْبِسُوا۟ ٱلْحَقَّ بِٱلْبَـٰطِلِ وَتَكْتُمُوا۟ ٱلْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ]

Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua.” [2:42]

Yahya Nisbet

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uingereza
Address & Website
Tel: +44 (0) 7074 192400
www.hizb.org.uk
E-Mail: media@hizb-ut-tahrir.info / press@hizb.org.uk

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu