Afisi ya Habari
Ukraine
H. 22 Rabi' I 1441 | Na: 1441/01 |
M. Jumanne, 19 Novemba 2019 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Urusi Yaendeleza Vita vyake dhidi ya Uislamu
Mnamo tarehe 12 Novemba 2019, Mahakama ya Kijeshi ya Urusi Kusini mwa mji wa Rostov-on-Don iliwahukumu Waislamu 6 wa Crimea kwa kile kiitwacho “Kesi ya Yalta Hizb ut Tahrir” kwa kifungo cha miaka 7 hadi 19.
Muslim Aliev (miaka 19), Inver Bekirov (miaka 18), Emit-Useyin Kuku (miaka 12), Vadim Syruk (miaka 12), Refat Alimov (miaka 8) na Arsen Djepparov (miaka 7) walipatikana na hatia katika kupanga na kushiriki katika shughuli za Hizb ut Tahrir.
Kwa miaka 5 iliyopita tangu Urusi ilipoichukua Crimea ni hukumu ya tano kwa kiitwacho “Kesi za Hizb-ut-Tahrir” ambapo Waislamu wanatuhumiwa na harakati za kigaidi. Hizb ut Tahrir ni chama cha kimataifa cha kisiasa cha Kiislamu kinacho lenga kusimamisha tena maisha ya Kiislamu katika nchi za Waislamu kupitia mapambano ya kifikra na kisiasa. Sifa ya Hizb ya kutotumia vurugu inajulikanwa vyema kupitia ulimwengu mzima na imethibitishwa na miaka 60 ya utendajikazi wake katika nchi zaidi ya 40. Majaribio yoyote ya kuituhumu Hizb kwa matendo ya vurugu hayana msingi wowote.
Mahakama za Urusi kwa mara nyingine tena ziliweka wazi mashtaka yake katika ugaidi. Karatasi zote za Mahakama, mashahidi wa tukio na wataalamu wa upande wa mashtaka walithibitisha kukosekana kwa kupanga, kutayarisha au kutambua vitendo vya kigaidi. Hakuna silaha, waliouawa au kujeruhiwa katika kesi hizi. Kesi yote imetegemea uchambuzi na mazungumzo ya hawa ndugu. Kiini cha kesi hizi ni uchunguzi wa shaka wa mazungumzo ya mada za Kiislamu.
Upuuzi wa hukumu hii ni dhahiri, kwa kuwa wanaume hao sita walihukumiwa vifungo ambavyo havipeanwi ndani ya Urusi kwa wauaji, wenye kunajisi watoto na wabakaji. Kesi hii ya mahakama ni uthibitisho mwingine kuwa Urusi imetangaza vita dhidi ya Uislamu, walinganizi wake na udhihirisho wowote wa dini yetu tukufu.
Urusi haijali ugaidi, wahalifu au usalama wa umma. Haya yote ni pazia za moshi tu kuziba ukatili wake wa wazi kwa wanaojitolea, wasafi na wenye maadili ambao ni wachamungu na mfano wa kudumu sio tu kwa Waislamu lakini pia watu wote.
Hofu juu ya fikra ya Uislamu inazilazimisha mamlaka za Urusi za kisasa kuwatambua kuwa ni wahalifu; na kuwahukumu wabebaji ulinganizi wa dini hii tukufu ambao hawajadhihirikiwa hata kwa makosa madogo kwa kifungo kisichoingia akilini.
Hii pia ni mbinu inayoelekezewa waislamu nchini Urusi na si tu nchini Crimea. Mambo ambayo yaonekaniwa na waislamu wa Crimea ni sehemu ya sera ya uhalifu ya Urusi dhidi ya Uislamu ndani ya nchi kama tuonavyo
Kaskazini mwa Caucasus na eneo la Volga na nje ya nchi kama tuonavyo huko Syria.
Mwenyezi Mungu aliyetukuka atueleza sisi kuhusu madhalimu kama hao katika Qur’an Tukufu:
(وَمَا نَقَمُوا مِنْهُمْ إِلَّا أَنْ يُؤْمِنُوا بِاللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ)
“Nao hawakuona baya lolote kwao, ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Msifiwa!” [85:8]
Tunawaambia Waislamu wa Crimea kama ifuatavyo:
Sio mara ya kwanza katika historia ya Crimea, wakati Urusi inafanya mashambulizi dhidi ya Waislamu wa Crimea Matatar. Hivi leo viongozi wahalifu Wakirusi kwa mara nyingine tena wanawakandamiza Waislamu wa Crimea bila ya sababu zozote.
Sera hii ya kikatili imetekelezwa tangu Urusi ya Czar na ukafiri Ukomunisti, ambapo Shirikisho la Urusi la kisasa ni mrithi wao wa kisheria katika sera hii ya jinai dhidi ya mataifa yote ya Kiislamu kwa ujumla na hususan Waislamu wa Crimea.
Na lau mwaka wa 1944 watu wote Matatar wa Crimea walitambuliwa kuwa wasaliti na katika miaka ya 90, walilaumiwa kwa misimamo mikali, leo wawakilishi wake bora wanashtakiwa kwa kuhusika katika shughuli za kigaidi.
Enyi Waislamu wa Crimea!
Madhalimu kama Catherine II na Stalin ambao walifanya uhalifu mkubwa zaidi dhidi yenu na wakajaribu sio tu kuifuta Crimea kutokamana na madhihirisho yoyote ya Kiislamu lakini pia walijaribu kufuta uwepo wenu wa kiwiliwili katika ardhi hii iliyobarakiwa, walikufa na kuzikwa makaburini. Wakati huo huo, licha ya majaribio yote haya, mulivumilia na siku hadi siku, mumeimarika na na kurudi kwenye Ufahamu wa zamani wa Uislamu na utekelezaji wake. Karibuni ni siku ambayo “magaidi” wakisasa watapotea kama wale waliopotea na serikali zao wale waliowashtaki nyinyi kwa usaliti na msimamo mikali hapo zamani, na mutafurahia katika ardhi zenu zilizohifadhiwa na utabikishaji wa Uislamu katika maisha yenu ya kila siku.
(وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ)
“Na siku hiyo Waumini watafurahi, Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu, humnusuru amtakaye, Naye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.” [30:4-5].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Ukraine |
Address & Website Tel: |