Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Urusi

H.  1 Shawwal 1441 Na: 1441/ 02
M.  Jumamosi, 23 Mei 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pongezi za Idd ul Fitr za Mwaka wa 1441 H
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir nchini Urusi inawapongeza Umma wa Kiislamu katika sikukuu ya Idd ul Fitr, twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awakubalie Waislamu funga zao, swala na ibada zote katika mwezi huu mtukufu, na kuwasamehe dhambi zao. Mtume (saw) amesema:

«مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَاناً وَاحْتِسَاباً غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ»

“Yeyote aliyefunga mwezi wa Ramadhan kwa Imani ya dhati na kutarajia thawabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu, husamewa dhambi zake zilizo tangulia.”[Imesimuliwa na Ahmad]

Ramadhan Mwaka huu imekuja katika mazingira ya kuenea kwa virusi vya Korona, ambavyo bado vinaua watu katika nchi za ulimwengu. Imeathiri Waislamu wengi nchini Urusi, lakini maambukizi mengi yalikuwa miongoni mwa watu wa Caucasus ya Kaskazini. Hospitali zilijaa, kulikuwa na upungufu wa vifaa vya kinga kwa wafanyikazi wa matibabu, na kutokuwa na utashi wa serikali kukubali uwepo wa janga, yote haya yalisababisha janga la halisi la Covid-19 huko Dagestan.

Ramadhan ilikuja bila ya ruhusa kutoka kote ulimwenguni, Waislamu wenyewe walikimbilia kufunga misikiti yao kwa swala za jamaa, hadi watetezi wengine wa Uislamu walijaribu kushawishi watu juu ya umuhimu wa kutofunga mwezi huu, ili mwili upambane vyema na virusi!

Vilevile, Waislamu wanaendelea kuteseka kutokana na maovu ya makafiri huko Ash-Sham na ulimwenguni kote. Lakini tunaona nyuma ya mawingu haya meusi mambo ambayo yanatufanya tufurahi, ambayo ni kwamba bila kujali shida zote zinazo wakabili Waislamu, bado wangali wanalinda kila kitu kinacho husiana na Dini. Waislamu ni Ummah mmoja; wanafunga na kuswali swala za usiku katika usiku wa Ramadhan, na wanajitahidi ili Mwenyezi Mungu (swt) awasamehe dhambi zao na awaridhie wao.

Pia tunaona jinsi maisha yanavyo geuka haraka, kama yale yaliyotokea kwa serikali za Kifirauni, ambapo zimesumbuliwa na virusi vidogo visivyo onekana kwa jicho la kawaida la uumbaji wa Mwenyezi Mungu, na Urasilimali ulifichuliwa, na wengine walilingania haja ya kumuomba Mwenyezi Mungu na kuwataka raia wao kuanza maombi ili liondolewe janga hilo.

Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu (swt) anawaonyesha tena wanadamu udhaifu na nguvu zao. Tunaamini kuwa Mwenyezi Mungu (swt) atalirudia jambo hili tena, wakati atakapoupa ushindi Ummah wa Kiislamu katika kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, ili Waislamu wawe na ngao ambayo watapigana nyuma yake tena. Itakuwa sababu nyingine ya majanga kwa serikali za Kifirauni, na suala la Khilafah litajadiliwa katika kila nyumba kama janga hili la sasa linavyo jadiliwa na tofauti ni kwamba watu wataona mabadiliko bora.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atusamehe dhambi zetu katika Ramadhan na kufanya sahali na kusaidia njia ya Ummah wa Kiislamu kuregesha Khilafah juu ya njia ya Utume. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aongeze mara dufu thawabu za wafanyikazi kwenye njia hii, na kwamba wanadamu waweze kuona utunzaji wa kweli wa watu kutoka kwa watawala wa Khilafah Rashida. Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu na mnamuamini Mwenyezi mungu” [Al-i-Imran: 110]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Urusi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Urusi
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-russia.info
E-Mail: mediaoffice.htr@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu