Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  1 Jumada II 1443 Na: 1443 / 07
M.  Jumanne, 04 Januari 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ni Chini ya Uislamu Pekee ndipo Hadhi ya Wanadamu Hupatikana!
(Imetafsiriwa)

Katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa watu wa Uzbekistan, Rais Shavkat Mirziyoyev alipendekeza kutangaza 2022 kuwa mwaka wa "Kuhakikisha Maslahi ya Binadamu na Maendeleo ya Mahalla".

Hili liliripotiwa na huduma ya habari ya raia wa nchi. Mirziyoyev alisema: "Ili kutoa kuupa jina Mwaka huu Mpya, tumetafiti maoni ya umma na kwa msingi wa mapendekezo haya ninapendekeza kutangaza 2022 katika nchi yetu mwaka wa "Kuhakikisha Maslahi ya Binadamu na Maendeleo ya Mahalla". Kuheshimu utu humaanisha kudhamini haki, uhuru na maslahi halali ya kila mtu anayeishi katika nchi yetu. Na Mahalla (kitongoji) ambacho huunda msingi wa jamii yetu hucheza dori kubwa katika suala hili. Endapo Mahalla ina amani, kutakuwa na amani nchini…”

Inajulikana kuwa moja ya njia hatari zaidi za uvamizi zinazotumiwa na wakoloni ni njia ya upotoshaji. Mfano wa hayo ni kauli mbiu zinazovutia kwa udanganyifu kama vile "mageuzi", "mabadiliko" na "maendeleo". Mirziyoyev, ambaye alichukua nafasi ya dhalimu Karimov baada ya kifo chake, anaendelea kutumia mbinu hii. Yeye pia, mwanzoni mwa kila mwaka mpya, huupa jina mwaka na kutoa ahadi kwa magunia (ahadi tupu). Aliuita mwaka wa 2022, mwaka wa "Kuhakikisha Maslahi ya Binadamu na Maendeleo ya Mahalla." Kwa hivyo, je, kauli mbiu hii changamfu inalingana na maisha halisi nchini Uzbekistan?

Ni dhahiri, kwa mtu yeyote mwenye akili timamu aliye na uwezo wa kuona angejibu "Hapana." Kwa sababu inajulikana vyema utu uko katika kiwango gani sasa chini ya hali za mfumo wa kikafiri, chini ya hali za urasilimali nchini Uzbekistan. Mfano rahisi wa hili ni ukweli kwamba watu wanaganda baridi kwa sababu ya ukosefu wa gesi na umeme! Endapo watu watapinga dhulma hii, wanatishiwa na vikosi vya usalama. Kuna mifano mingine mingi inayoonyesha kwamba utu hauna thamani hata senti moja chini ya mfumo huu wa kikafiri. Na bado Mirziyoyev hakuona aibu kusema: "Tutahamasisha nguvu zetu zote na uwezo wetu ili maisha ya watu wetu yawe na mafanikio zaidi na yenye maana!" Kana kwamba watu wa Uzbekistan wamewahi kuishi maisha ya mafanikio!!

Kwa hakika, si tu kwamba hadhi ya Muislamu itatukuzwa, bali hadhi ya mwanadamu yeyote pia itatukuzwa chini ya Uislamu, ambao ni rehema kwa walimwengu. Tukiitazama historia ya Uislamu, tutashuhudia kwamba heshima ya madhimmi, Mayahudi na Manaswara, ililindwa na dola sawa na Waislamu. Katika siku ambazo Waislamu walishikamana na Uislamu, walikuwa taifa bora kabisa lililotolewa kwa wanadamu. Khalifa Omar (ra) aliyeongoka amesema: “Sisi ni watu ambao Mwenyezi Mungu amewatukuza kwa Uislamu, tukitafuta utukufu usiokuwa huo, Mwenyezi Mungu atatudhalilisha. Mazingira magumu ya Waislamu, wakiwemo watu wa Uzbekistan, yanathibitisha ukweli wa maneno ya bwana wetu Omar (ra).

Kwa hiyo, isipokuwa serikali hii ya kikafiri iliowekwa na makafiri wa kikoloni na watawala vibaraka wao, watumishi wao, ipinduliwe, na isipokuwa mfumo wa Uislamu unaotabikishwa na Dola ya Khilafah Rashida usimamishwe, mwanadamu hatakuwa na hadhi, na udhalilifu huu utaendelea. Hivyo basi, ikiwa Waislamu wanataka kuishi kwa utu, wasidanganywe na hila za watawala, wala wasicheze na firimbi za watawala madhalimu, wala wasipigane na ndugu zao Waislamu. Bali wawanyoshee mkono wana wao na ndugu zao katika Hizb ut Tahrir ili kusimamisha dola ya Khilafah Rashida, ili waregee kama taifa bora lililotolewa kwa wanadamu! Ni hapo tu ndipo wanadamu wataheshimiwa kikweli.

 [ولِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَٰكِنَّ الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na Waumini. Lakini wanaafiki hawajui.” [Al-Munafiqn: 8].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu