Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  23 Shawwal 1444 Na: 1444 / 12
M.  Jumamosi, 13 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Baada ya Kura ya Maoni, ni zamu ya Uchaguzi wa Rais
(Imetafsiriwa)

Kwa mujibu wa amri ya Rais wa Uzbekistan, uchaguzi wa mapema wa rais ulipangwa kufanyika Julai 9, 2023. Amri hiyo inasema: “Kulingana na Ibara ya 110 na 128 ya Katiba ya Jamhuri ya Uzbekistan na Kifungu cha 66 cha Kanuni za Uchaguzi za Jamhuri ya Uzbekistan, uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Uzbekistan umepangwa kufanyika Julai 9, 2023.” Kifungu cha 128 cha katiba mpya iliyopitishwa baada ya kura ya maoni ya Aprili 30 kinasema kwamba "Rais wa Jamhuri ya Uzbekistan ana haki ya kuamua uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Uzbekistan kabla ya wakati." Bila shaka, Mirziyoyev alitarajiwa kutumia fursa hii, lakini mambo hayakutarajiwa kutokea haraka hivyo. Lakini ikiwa tutazingatia hali ngumu ya kiuchumi ya sasa katika nchi yetu na kudhoofika kwa hali ya kimataifa, haishangazi kwake kufanya uamuzi kama huo. Hili linaweza kueleweka kutokana na hotuba ya Mirziyoyev katika mkutano wa baada ya kura ya maoni wa Mei 8, ambapo alieleza kwa nini aliacha muhula wake wa miaka 3.5 kwa hiari yake mwenyewe. Miongoni mwa mambo muhimu ya hotuba yake ni haya yafuatayo: “Nne: Katika hali ya sasa wakati michakato mikali na migumu inatawala duniani na katika eneo letu, suala la dharura zaidi ni kutafuta na kutekeleza njia sahihi na yenye ufanisi ya maendeleo. ” Inaonekana kwamba kipote cha wanasiasa, wakiongozwa na Mirziyoyev, walikuwa na wasiwasi kwamba kwa hali yoyote hatma nzuri haitawangojea mnamo 2026, kwa hivyo ilionekana kuwa bora kuchukua fursa ya hali bora zaidi ya sasa bila kuchukua hatari. Kwa kweli, ni wazi kwamba lengo la vitendo kama hivyo vya kisiasa sio kuwafurahisha watu, kama Mirziyoyev alivyosema, lakini kurefusha uhai wa serikali yake. Hadith hii ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), inawahusu wao:

«إِذَا لَمْ تَسْتَحْيِ فَاصْنَعْ مَا شِئْتَ»!

“Ikiwa huna haya basi fanya unavyotaka!”

Kama tulivyosema kwa muda mrefu, tatizo sio tu kwa katiba mpya au kuongezwa kwa muhula wa Mirziyoyev, lakini mfumo uliolazimishwa na kutekelezwa juu yetu sio wa Kiislamu. Maadamu mfumo huu, ambao ni zao la akili ya mwanadamu, unaendelea kutekelezwa, utabadilishwa kama soksi na wale wanaong'ang'ania mamlaka; Kwa vile lengo lao pekee ni kurefusha uhai wa utawala wao kwa gharama yoyote ile hata kama watalazimika kuwafanya watu wao kuwapigia magoti wakoloni wa makafiri kama Marekani na Urusi na kuwaruhusu kupora mali zetu.

Hivyo basi, kama tulivyowataka Waislamu wote katika nchi yetu wasishiriki katika kura ya maoni na kuisusia, tunawataka pia kukataa kushiriki uchaguzi wa urais; kwa sababu Waislamu hawaruhusiwi kabisa kushiriki katika mambo haya mawili, na kuwalingania watu kushiriki katika mambo hayo. Uislamu unawaamrisha Waislamu kuishi kwa mujibu wa sheria ya Mwenyezi Mungu na kutotii sheria za ukafiri. Lakini kutoshiriki uchaguzi wa urais pekee hakuwezi kubadili maisha yetu ya sasa, ambayo yamejaa udhalilifu na unyimwaji haki. Bali, wokovu wetu pekee upo katika kuachana na katiba isiyo ya Kiislamu ambayo msingi wake ni demokrasia fisidifu na badala yake kuibadilisha kwa katiba ya Kiislamu ambayo imetungwa kwa njia ya ijtihad sahihi inayoegemezwa juu ya Qur’an na Sunnah. Mfumo huo unaweza kutabikishwa tu kwa uwepo wa Dola ya Khilafah. Hivyo basi, enyi Umma mtukufu unaostahiki izza, inusuruni Hizb ut Tahrir na ilinde, kwani ndiyo inayofanya kazi usiku na mchana ili kuiregesha maishani dola hii iliyobarikiwa!

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ ‌تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Muhammad 47:7]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu