Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari

H.  27 Shawwal 1445 Na:
M.  Jumatatu, 06 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
“Matembezi” Jumla ya Magharibi hadi Asia ya Kati: zamu ya Uingereza
(Imetafsiriwa)

Baada ya tukio la Crocus, kulikuwa na ongezeko la hali ya chuki dhidi ya Uislamu na shinikizo kwa watu wa Asia ya Kati ndani ya Urusi. Baadaye, kuongezeka kwa ziara na mawasiliano kutoka kwa maafisa wa nchi za Magharibi kwenye eneo hilo kulionekana. Inaonekana kana kwamba sera ya uvumilivu ya Urusi, ambayo inatuma ujumbe mwingine wa vitisho kwa serikali za nchi za Asia ya Kati kwa kuzidisha shinikizo kwa wahamiaji kutoka Asia ya Kati, imetazamwa na nchi za Magharibi kama fursa. Katika miezi ya hivi karibuni, utawala wa Urusi na wafuasi wake wamezungumza kwa jeuri na kiburi na pande za Kazakhstan na Uzbekistan, na hata kupendekeza kuziunganisha nchi hizi mbili na Urusi. Sio chuku kusema kwamba tukio la Crocus lilionyesha kuwa tishio la Urusi limefikia kilele chake katika miaka ya hivi karibuni. Kwa hivyo, wakati taharuki hii imeongezeka, uhusiano wa nchi za Magharibi na serikali za Asia ya Kati umeongezeka sana.

Kwa mfano, mwishoni mwa Machi 2024, wajumbe wa maseneta wa Marekani walizuru nchi za Asia ya Kati, hasa Uzbekistan, na kufanya mikutano na Rais wa Uzbekistan na maafisa kadhaa. Katikati ya mwezi wa Aprili, mwaka huu, ujumbe wa NATO ulifika Uzbekistan, na sambamba na hilo, India, ambayo inaungwa mkono na Marekani, pia ilituma ujumbe ulioongozwa na afisa wa ngazi za juu wa kijeshi. Hata hivyo, ujio wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Cameron, ambaye anahesabiwa kuwa mwanasiasa mashuhuri katika siasa za kimataifa, katika nchi za Asia ya Kati ulikuwa ni mfano mashuhuri zaidi wa uvamizi mpya wa Magharibi katika eneo hilo. Kabla ya kuwasili kwake, alisema kuhusu ziara hii aina tatu za umuhimu mkubwa kwa ushirikiano na nchi za Asia ya Kati, ambazo ni mpangilio wa kimataifa, ushirikiano wa kiuchumi, na elimu. Akithibitisha maneno haya, Cameron aliongeza kuwa ufadhili wa masomo wa Chevening, ambao unasaidia masomo ya wageni katika vyuo vikuu vya Uingereza, utaongezeka maradufu. Alionya kwamba Asia ya Kati ndio kiini cha changamoto kubwa zaidi, na akasema kwamba pauni milioni 50 zitatengwa kusaidia "uhuru wake uliopatikana kwa bidii" katika miaka mitatu ijayo.

Ikumbukwe kwamba ziara hii nchini Uzbekistan ni ya kwanza kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza tangu 1997. Wakati wa ziara yake nchini Uzbekistan, Cameron alifanya mikutano na Waziri wa Mambo ya Nje Bakhtiyor Saidov na Mwenyekiti wa Seneti wa Baraza Kuu Tanzila Narbaeva. Kwa mujibu wa taarifa ya Ubalozi wa Uingereza, Uzbekistan na Uingereza zilitia saini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya mawasiliano na miundombinu ya kikanda na kimataifa, ikiwa ni pamoja na Azimio la Ushirikiano Kamili, ambalo linajumuisha kupanua ushirikiano katika maeneo ya kupambana na ugaidi, ulinzi, mabadiliko ya tabianchi na haki za binadamu. Cameron pia alisisitiza wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari kwa kusema, "Ninachosema hapa ni kwamba hatuwaombei kuchagua kati ya washirika hao na nchi kama Uingereza..." Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, wakati wa ziara yake Mongolia, alisema kuwa lengo kuu la ziara yake katika Asia ya Kati lilikuwa ni kwa nchi za eneo hilo kufanya uchaguzi huo. Inaonyesha kikweli jinsi Uingereza ilivyo na unafiki na tamaa kubwa.

Pia, Cameron, ambaye alikutana na marais wote wa kanda hiyo, hakuweza kukutana na Mirziyoyev kibinafsi. Iliripotiwa kwamba Mirziyoyev alikwenda likizo ya kazi siku moja kabla ya kuwasili kwake, Aprili 22. Hii ni hali isiyo ya kawaida, kwani kutokutana na afisa wa ngazi ya juu kutoka nchi kubwa kama Uingereza - kutokana na shakhsiya ya Mirziyoyev yenye tamaa - hakumhusu sana. Inaonekana kwamba kilicho karibu na ukweli ni kwamba hili sio chaguo lake, lakini badala yake ujanja wa kisiasa ili kuepuka kumkasirisha tena "Kaka wa Kirusi", kwa kuwa ziara ya ujumbe wa NATO nchini Uzbekistan ilikasirisha Urusi kabla ya hapo.

Hali nyingine ya kufurahisha ilitokea, kwani ilikuwa wazi kuwa Uzbekistan ilikuwa ni nchi muhimu katika kanda hiyo kwa Uingereza. Baada ya kukamilisha ziara yake nchini Mongolia, Cameron aliregea Uzbekistan mnamo tarehe 27 Aprili na kukutana na Waziri wa Mambo ya Nje. Ingawa hakuna maelezo yaliyotolewa kwa tabia yake, inaweza kuzingatiwa kuwa alilenga kuonyesha kwamba Uzbekistan ilikuwa ya umuhimu maalum kwa Uingereza na kuonyesha tena utayari wake wa kutoa msaada kila wakati kukabiliana na tishio la Urusi.

Ziara ya Cameron inaweza kuonekana kama sehemu ya sera jumla ya nchi zote za Magharibi, zikiongozwa na Marekani, zinazolenga kupunguza ushawishi wa Urusi na China katika Asia ya Kati. Lakini Uingereza pia ina maslahi yake ambayo haitasita kuidunga kisu Marekani au Ufaransa mgongoni ili kufanikisha. Ijapokuwa nchi hizi za kikoloni za makafiri zinaonekana ziko upande mmoja, kiuhalisia wao si marafiki, bali ni maadui. Ni nchi ovu zinazobeba chuki nyoyoni mwao.

Uingereza, haswa, ni moja ya maadui wetu wakubwa, kwani ilisababisha jeraha kubwa nyoyoni mwa Waislamu ambalo bado linavuja damu. Ni Uingereza ndiyo iliyocheza dori kuu katika kuivunja Khilafah Uthmani, mlinzi wa Waislamu na mlinzi wa maisha yao, mali, na hadhi yao. Pia ndiyo iliyoasisi umbile lililolaaniwa la Kiyahudi nchini Palestina.

Ingawa haina nguvu kwa sasa kama ilivyokuwa kabla ya Vita vya Pili vya Dunia, hata hivyo ujanja wake ni ule ule. Pia inaharakisha hatua zake ili kupata sehemu kubwa zaidi inayowezekana na kueneza ushawishi wake katika Asia ya Kati, hasa nchini Uzbekistan. Mwishowe, dola hii ya kilafi ya kibepari ni kimelea ambacho hula miili ya mataifa dhaifu, na huishi kwa kunyonya damu zao. Inaupa mwili sumu tu, na kuufanya kuwa mgonjwa na uchovu. Bila shaka, jambo bora tunaloweza kulifanya ni kujikinga na vimelea hivi vinavyonyonya damu yetu na kutuacha na madhara ya demokrasia, na kuwatupa chini ya miguu na kuwakanyaga. Hata hivyo, kazi hii haitatimia isipokuwa tukisimamisha Khilafah yetu tukufu, ambayo Uingereza ilifanikiwa kuivunja siku moja! Hapo ndipo ujanja wa dola hii ovu, na ya kuchukiza hautakuwa na manufaa yoyote, bali itaonja uchungu wa kushindwa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir in Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu