Jumatano, 22 Rajab 1446 | 2025/01/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  27 Dhu al-Hijjah 1445 Na: 1445 / 16
M.  Jumatano, 03 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Serikali ya Uzbekistan Inataka Kuwafunga Wafungwa 39 Wa Zamani wa Kisiasa kwa Miaka Mingi Zaidi
(Imetafsiriwa)

Tunawatahadharisha Waislamu wetu kwamba mawingu meusi yanakusanyika juu ya vichwa vyetu! Tunawataka wawe macho, tukionya dhidi ya kurudi kwa enzi ya aibu ya uovu inayosifiwa kama “utawala wa takataka”!

Enyi Waislamu wa Uzbekistan!

Je, mnajua kwamba miongoni mwenu kuna vijana wachamungu na wenye ikhlasi ambao wamekaa miaka mingi ya maisha yao katika magereza, katika vyumba vilivyojaa unyevunyevu, katika hali ya kinyama iliyojaa shinikizo la kisaikolojia na kimwili, kwa sababu ya kusema kwao, “Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu”?! Hao ni Mashababu (wanaume) ambao walifungwa kwa miaka mingi kwa mashtaka ya uwongo na walikuwa wahasiriwa wa mashini ukandamizaji ya utawala dhalimu wa Karimov mnamo 1999-2000. Kana kwamba hii haitoshi, miaka hiyo ya kifungo chao ilipoisha, hukumu mpya ziliongezwa kwao kwa visingizio tofauti na vya kubuni. Wakati wa utawala wa Mirziyoyev, ambaye aliingia madarakani baada ya kifo kibaya cha dhalimu Karimov, alianza kuwaachilia wale ambao hukumu zao zilikuwa zimeisha kutoka gerezani mmoja baada ya mwengine. Wakati Mirziyoyev, katika mojawapo ya hotuba zake, alipoukosoa utawala wa Karimov na kuutaja kuwa ni “utawala wa takataka,” kauli yake iliibua mwanga wa matumaini kwa watu wetu. Hata hivyo, inaonekana kwamba tumaini hili limeambulia patupu leo! Mwanzoni mwa mwaka huu, kundi la hawa Mashababu Waislamu waliodhulumiwa walikamatwa, ambao nusura wapoteze afya zao walipokuwa wakitumia ua la ujana wao magerezani. Wakati huu, wakati wa uchunguzi wao, walikabiliwa na mashtaka ya uwongo na mateso, hadi mmoja wao alitishiwa kubakwa mkewe mbele yake, na mwengine kutishiwa kufungwa mwanawe ikiwa hatasaini karatasi ... Wafanyikazi wa Idara ya Usalama waliwatendea kwa ukatili ndugu zetu waliokamatwa mwezi wa kwanza wa mwaka huu. Kesi ya 23 kati ya Mashababu hao ilianza mnamo Mei 9. Hivi majuzi ilifichuliwa kuwa mwendesha mashtaka aliomba wahukumiwe vifungo vya kuanzia miaka 7 hadi 17 jela. Ikumbukwe kuwa hawa Mashababu 23 walikaa gerezani jumla ya miaka 407, na vifungo vipya viliongezwa kwao mara 43! Hata hivyo, serikali ya sasa ya Uzbekistan inaonekana kuamini kwamba hili halitoshi. Inaonekana wataamua kuwafunga tena na kuwahukumu miaka mingi kwa makosa mbalimbali ya uwongo. Vivyo hivyo, wafungwa 16 wa zamani wa kisiasa kutoka maeneo mbalimbali ya nchi yetu waliletwa Tashkent na uchunguzi wao ukaanza. Hakuna hakikisho kwamba kile kilichotokea kwa Mashababu 23 waliopita hakitarudiwa kwao pia. Hali ni hatari sana na inatia wasiwasi!

Dhulma imejitokeza katika jamii yetu, na vitendo kama hivyo vya kinyama vinaelekezwa katika kunyamazisha haki. Lakini cha kustaajabisha zaidi ni kwamba hakuna vyombo vya habari vya ndani na nje, vilivyo na njaa ya porojo, vinavyochapisha habari za kesi hizi zilizotajwa hapo juu wala uchunguzi huu wa kina, ambao unapaswa kuvutia hisia za umma mzima. Inaonekana kwamba serikali inajaribu kuficha kesi ya watu hawa machoni pa watu na kuzitatua kesi hizi haraka kufumba na kufumbua! Labda serikali inajaribu kuwafurahisha “kaka zake wakubwa” kama vile Warusi, na inajaribu kuficha kutoka kwa watu tabia yake ya aibu katika nyayo za serikali ya dhalimu Karimov.

Zingatia kuwa, Mashababu (wanaume) ambao kesi zao zinasikilizwa mahakamani hapo awali walituhumiwa kuwa wanachama wa Hizb ut Tahrir, chama cha kisiasa cha Kiislamu na walifungwa kwa miaka mingi chini ya Ibara ya 159 na 244 ya Sheria ya Jinai ya Jamhuri ya Uzbekistan. Hadi sasa, wengi wao wamesema kwamba wanaichukulia fikra na njia ya Hizb kuwa sahihi. Ni jambo la kimaumbile kwamba kila muumini mwenye ikhlasi anayesikiliza ulinganizi wa Hizb ut Tahrir anakubali na kuunga mkono fikra hizi. Kwa hakika Hizb imekuwa ikitoa ulinganizi kwa Ummah wa Kiislamu kuregesha mfumo kamili wa maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa muda wa miaka 70, na itaendelea kufanya hivyo, Mwenyezi Mungu akipenda... Pia, watu wenye ikhlasi wanaoijua Hizb wanathibitisha kwamba haitumii nguvu kufikia malengo yake, na haina uhusiano wowote na itikadi kali na ugaidi, kama serikali kandamizi zinavyodai. Pia wanajua kwamba njia ya Hizb ni mvutano wa kifikra na mapambano ya kisiasa, na silaha yake pekee ni fikra. Tawala zisizoweza kuhimili mapambano haya ya kifikra na kisiasa hazina budi ila kutumia nguvu kunyamazisha sauti, vifungo, mateso, unyanyasaji na hata kuua.

Kudai kufungwa kwa vijana hawa kwa muda wa kuanzia miaka 7 hadi 17, wanaoweka maslahi ya Ummah juu ya maslahi yao wenyewe, na ambao wamedhamiria kuubeba ujumbe bila ya kusubiri chochote isipokuwa radhi za Mwenyezi Mungu, ni uovu mkubwa na mbaya. Hata hivyo, Mwendesha Mashtaka haitishi adhabu kali kama hiyo kwa wahalifu halisi wanaosababisha madhara makubwa kwa jamii yetu, kama vile wauaji, wabakaji, wafisadi, wapokeaji rushwa, wezi na matapeli. Kila mwenye akili timamu anayesoma shitaka lililoelekezwa dhidi ya hawa Mashababu ishirini na tatu Waislamu atatambua kwamba wao si wahalifu hata kidogo. Kwa kweli, mashtaka hayo ni ushahidi wa wazi kwamba wao hawana hatia na sio wahalifu.

Tunatoa wito kwa watu wetu Waislamu kutochukulia tofauti hatima ya watu hawa wachamungu, Mashababu wapenda mageuzi ambao ni ndugu zenu Waislamu! Waungeni mkono na muwalinde, au angalau muwaombee! Wala msisahau kwamba hakika mtahesabiwa kesho mbele ya Mwenyezi Mungu kwa yale mliyowafanyia watu hawa waliodhulumiwa!

Tunaionya serikali ya Uzbekistan dhidi ya kufuata njia ya aibu ya utawala dhalimu wa Karimov!Vile vile tunaitahadharisha isisibiwe na dua za kina baba, kina mama, watoto, waume na jamaa za vijana hawa wanaodhulumiwa, na dua za Waislamu kwa jumla wanaosimama nyuma yao! Dhulma kamwe haiangazi njia ya dhalimu, bali dhulma ni giza Siku ya Kiyama! Mtume (saw) amesema: «اتَّقُوا الظُّلْمَ فَإِنَّ الظُّلْمَ ظُلُمَاتٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ» “Iogopeni dhulma, kwani dhulma itageuka kuwa giza kupita kiasi Siku ya Kiyama, jihadharini na kughafilika, kwani kughafilika kuliwaangamiza waliokuwa kabla yenu.” Imepokewa na Muslim.

Tunakutahadharisheni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anachelewesha adhabu kali kwa jinai hii kubwa kwa siku ngumu. Kwa ajili ya Siku ya Kiyama. Lakini madhalimu hakika wataona matokeo chungu ya dhulma yao hapa duniani pia katika kuitikiwa dua ya waliodhulumiwa, kwani hakuna pazia baina yake na Mwenyezi Mungu, na adhabu ya Akhera ni kali zaidi na ya aibu zaidi. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

[وَلَا تَحْسَبَنَّ اللهَ غَافِلاً عَمَّا يَعْمَلُ الظَّالِمُونَ إِنَّمَا يُؤَخِّرُهُمْ لِيَوْمٍ تَشْخَصُ فِيهِ الْأَبْصَارُ]

“Wala usidhani Mwenyezi Mungu ameghafilika na wanayo yafanya madhaalimu. Hakika Yeye anawaakhirisha tu mpaka siku yatapo kodoka macho yao.” [Ibrahim 14:42].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu