Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
H. 29 Rabi' I 1442 | Na: 1442/07 |
M. Jumapili, 15 Novemba 2020 |
Taarifa Kwa Vyombo vya Habari
Mashirika na Misaada ya Kimagharibi Yanaiangamiza Yemen Wala Hayaijengi, Ewe Hamid!
(Imetafsiriwa)
Gazeti la Al-Thawra linalochapishwa nchini Yemen la mnamo tarehe 11/11/2020 lilifuatilia warsha ya kazi iliyoandaliwa na Wizara ya Fedha katika Serikali ya Wokovu, kuanzia tarehe 07 hadi 11/11/2020 M jijini Sana'a chini ya kichwa "Uunganishaji wa fahamu na kuratibu uongozi wa kiakili wa kada ya serikali za mitaa kuelekea mipango ya maendeleo ya kawaida ya mitaa pamoja na sheria na misingi ya kuandaa bajeti," kwa makada wa serikali za mitaa, akiwepo mkurugenzi wa afisi ya Mahdi Al-Mashat, Ahmed Hamed, mkuu wa Baraza la Maswala ya Kibinadamu. Baraza hili lilikuwa limefanya mkutano tarehe 08/11/2020 M, ambapo lilijadili juu ya utaratibu wa mwingiliano uliofuatwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi nchini Yemen. Warsha hii na mkutano wa Baraza la Masuala ya Kibinadamu zilizingatia jinsi ya kuidhinisha miradi na kutoa vibali kupitia baraza hili, baada ya kukosekana kwa usawa ambao uliharibu kazi za mashirika katika kipindi cha miaka mingi.
Ni muhimu kukumbuka kuwa mashirika ya Kimagharibi yamelenga Wizara ya Kilimo kuizuia kupanua kilimo cha nafaka ambazo Mahouthi wanadai kuwa wako kwenye njia ya kujitosheleza kwa nafaka na mipango ya mbegu kwa nia ya kuondoa mbegu za kienyeji kuagiza mbegu kutoka nje, ama shirika la FAO limeangamiza mifugo ya watu katika maeneo tofauti tofauti. Mwisho wake ulikuwa katika tarafa za Jimbo la Taiz, kwa kugawanya kwake mifugo wagonjwa mwanzoni mwa mwaka huu, ambayo ilikufa baada ya kugawanywa, na kusambaza maambukizi kwa mifugo mingine. Mipango ya mashirika pia ililenga upande wa idadi ya watu kupitia Wizara ya Afya na shughuli zingine za kutiliwa shaka katika wizara anuwai, kama ilivyotokea katika Wizara ya Maji, ambayo Waziri Nabil Al-Wazir alihusishwa kwa ufisadi wa mamia ya mamilioni ya riyal.
Kupona kwa Mahouthi walichelewa kutambua kwamba kazi ya mashirika ya Magharibi na misaada wanayotoa chini ya hali zisizo za kawaida, ili kuweza kufikia malengo yaliyotumwa kwa ajili yake, nayo ni kuimarisha uhusiano kati ya Yemen na Magharibi. Mahouthi walifurahi kwa mashirika kutoa pesa za ukarimu na kufanya kazi ya huduma ya jamii, kama vile kutoa mgawo wa chakula, kukarabatisha barabara, kuondoa taka kutoka mitaa ya jiji, kutoa dawa, kulipa sehemu ndogo ya mishahara ya walimu, na kupeana mafuta kwa bei rasmi.
Ewe Hamid! Wewe ni mwendelezo wa serikali iliyopita kwa sababu ya kutegemea misaada ya Kimagharibi, ambayo mnamo 2006 ilifikia dolari milioni 350, ambayo kwayo Amerika ilitaka kumpindua Saleh, na leo inakuungeni mkono kwayo. Hakika umethibitisha utepetevu wenu na kutokuwa na uwezo kwenu wa kuyafukuza mashirika yote, haswa Mpango wa Chakula Duniani, licha ya kujua uovu wake. Hivi sasa limewaletea tena zaidi ya makasha 326 ya chakula kilichoharibika (At-Thawra 12/11/2020). Uko wapi ubwana wa uamuzi wenu wa kisiasa ambao munawadhihaki nao wafuasi wenu?!
Hakika utajiri wa Yemen, ambao Mwenyezi Mungu ameijaalia, unaitosheleza kutokana na kuomba omba na kunyoosha mkono wake kwa Magharibi, lakini chini ya kivuli cha watawala vibaraka, kheri yake na utajiri wake hautaonekana kwa sababu wanatii amri za dola za Magharibi. Hakika utabikishaji wa Uislamu ni utabikishaji wa kimapinduzi ya kikamilifu katika nidhamu zote za maisha; kisiasa, kiuchumi, na kijamii ... nk. Ni faradhi juu ya watu wa Yemen kupitia Dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ambayo Hizb ut-Tahrir inafanya kazi kuisimamisha, kwani ndio mdhamini wa kuikata mipango ya dola za magharibi kutoka Yemen. Mtume (saw) amesema:
«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»
"Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume."
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |