Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  6 Jumada I 1360 Na: HTY- 1442 / 12
M.  Jumatatu, 21 Disemba 2020

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

            Ewe Muhammad Al-Imad: Khilafah Itasimamishwa, kwa Idhini ya Mwenyezi Mungu

Na Ndio Nidhamu ya Utawala katika Uislamu, Aridhike Mwenye Kuridhika na Akasirike Mwenye Kukasirika
(Imetafsiriwa)

Kurudi kwa Uislamu kama umbile la kisiasa; Dola ya Khilafah, ingali inawatia tumbo joto mno nchi za Magharibi, kwani kurudi kwake kunamaanisha kuondolewa kwa ushawishi wao uliodumu karibu miaka mia moja, na kutofaulu vibaya kwa serikali za kifalme na za kijamhuri ambazo waliziasisi katika nchi za Waislamu, baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia. Katika wasiwasi huu, nchi za Magharibi zinashirikiana na miongoni mwa watoto wa Kiislamu ambao wamepagawishwa na thaqafa ya Magharibi, waliofuata njia yake na kuongozwa na mwongozo wake na kukiunga mkono kile kilichotolewa na yeye, na kuufanya Uislamu utengane na maisha.

Wimbi la chuki na shambulizi kwa Khilafah linaenea kote katika nchi za Kiislamu, na wakati huu linaonekana nchini Yemen, haswa kutoka kwa chaneli ya Al-Hawiyyah inayofungamana na harakati ya Houthi, ambayo mkurugenzi wake, Muhammad Ali Al-Imad, alisema hewani: kwamba yeye ni "msekula." Kwa hivyo, anafuata nyayo za Mustafa Kamal, mvunjaji wa Khilafah, na Fahd bin Abdul Aziz, ambaye alitangaza kwamba hatakuwa kama Mustafa Kamal na kuuharibu Uislamu kutoka nje, bali atauharibu kutoka ndani. Hivyo basi haishangazi kwa chaneli yake kuishambulia Khilafah!

Na ikiwa tutawaangalia wengine wanaoishambulia na kuichukia Khilafah; Tutapata mikono yao ikiwa imefungwa na mkono wa Magharibi wa kikoloni, ambao waliahidi kutoiondoa nidhamu ya kijamhuri ya serikali waliyoileta kwao, na kuthibitisha ikhlasi yao kwao. Kwa hivyo, Mahouthi waliialika (Magharibi) iwawekee ruwaza ya dola ya kisasa la Yemen ambayo kwayo itawachorea wao tena utenganishaji wa dini na maisha kwa njia ya kina katika utawala, uchumi, uhusiano wa kimataifa na elimu ... nk.

Huu hapa Umoja wa Mataifa, UNICEF, UNESCO, FAO, OCHA, Mpango wa Chakula Duniani, na mfuriko wa mashirika mengine ya Kiamerika yanayoongoza "kazi ya kibinadamu!" nchini Yemen, na wawakilishi wao, kama vile Martin Griffiths, Lise Grande, Jean-Nicholas Bueze, Philippe Douville, Anna Paolini, Alfredo Impiglia, na wengineo ambao wamepanga njama dhidi ya Uislamu na watu wake mchana na usiku, na bado wangali wanapanga njama.

Uislamu ni ushahidi unaopambana na watu, na watu sio ushahidi unaopambana na Uislamu. Basi yeyote atakayeuchukua Uislamu kwa usafi wake amefaulu, na yeyote atakaye kunywa uchafu basi ni juu yake na alicho kunywa. Mtume (saw) Amesema:

«قَدْ تَرَكْتُكُمْ عَلَى الْبَيْضَاءِ لَيْلُهَا كَنَهَارِهَا لَا يَزِيغُ عَنْهَا بَعْدِي إِلَّا هَالِكٌ»

“Hakika nimewaacheni pahali peupe usiku wake kama mchana wake hapotei yeyote napo baada yangu isipokuwa mpotevu [Imesimuliwa na Ibn Majah kutoka kwa Al-Irbadh Bin Sariyah]. Khilafah inayokuja ni Khilafah ya Waislamu na kwa sababu ni kwa njia ya Utume, itasimama pasi na budi kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyo ahidi katika maneno yake:

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao.” [An-Nur: 55].

Hao ni wale walioichukua njia ya Kisheria kama njia ya kuisimamisha, na hawakupotoka kutoka kwayo hata kidogo,  hali yakuwa wako kwenye njia hiyo mpaka Nusra kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) uwashukie. Amesema Mtume (saw):

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

“… kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume” [Imesimuliwa na Ahmad kutoka kwa Al-Nu’man Bin Basheer].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu