Jumatatu, 27 Rajab 1446 | 2025/01/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  15 Muharram 1444 Na: HTY- 1444 / 01
M.  Jumamosi, 13 Agosti 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Umwagaji damu ya Watu wa Shabwa, Jukumu lake liko juu ya Waliotoa Maagizo ya Kuimwaga
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumatano, 10/8/2022, Rais wa Baraza la Uongozi wa Rais, Dkt. Rashad Al-Alimi alitoa taarifa ya ufafanuzi kuhusu matukio ya jimbo la Shabwa. Taarifa ya ufafanuzi iliyochapishwa na shirika la habari la Yemen, Saba, ilieleza kuwa hatua kadhaa zilichukuliwa, ikiwemo kufutwa kazi kwa baadhi ya viongozi katika jimbo hilo. Mbali na kuundwa kwa kamati iliyoongozwa na Waziri wa Ulinzi na uanachama wa Waziri wa Mambo ya Ndani na wajumbe watano wa Kamati ya Pamoja ya Usalama wa Kijeshi kuchunguza ukweli na kujua sababu zilizopelekea watu kupoteza maisha. Na kuripoti matokeo kwa Baraza la Uongozi wa Rais ili kuchukua hatua stahiki za kisheria.

Kauli hii ya rais inajiri baada ya vita vikali vilivyodumu kwa siku tatu, na kusababisha makumi ya watu kuuawa na kujeruhiwa, na kukiuka utukufu wa kumwaga damu za watu hao hao; wa imani moja na nchi moja, na wanalijua vyema hili kama Mwenyezi Mungu (swt) anavyosema:

[وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِناً مُّتَعَمِّداً فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِداً فِيهَا وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَاباً عَظِيماً]

“Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa” [An-Nisa: 93]. Mtume wetu mtukufu (saw) amesema, katika riwaya ya Al-Bara’ Bin A’zib:

«لَزَوَالُ الدُّنْيَا أَهْوَنُ عَلَى اللَّهِ مِنْ قَتْلِ مُؤْمِنٍ بِغَيْرِ حَقٍّ»

Kuangamia dunia hii, ni sahali mbele ya Mwenye Mungu (swt) kuliko kumuua muumini pasi na haki.”

Vita hivyo vinatokana na kuzorota kwa huduma katika maeneo yaliyo chini ya Baraza la Amri ya Rais, ikiwemo la Shabwa, ambayo inakabiliwa na huduma mbovu katika masuala ya afya, uchumi, umeme, maji na mambo mengine kutokana na serikali kufungamanishwa na mfumo wa kirasilimali, ambayo haijali kuchunga mambo ya watu kwa mujibu wa hukmu za Uislamu. Bali inajali kutozwa kodi na ushuru kwa wananchi ili kuwafukarisha zaidi, na kujaza mifuko ya watawala hao fedha za mali ya umma na mali ya dola. Kauli hii pia inajiri kutokana na mgawanyiko wa wazi uliopo kati ya wajumbe wa Baraza la Uongozi wa Rais, wafuasi na wapinzani, kwa mujibu wa maelekezo ya vyama vinavyowaunga mkono, hususan nafasi ya Mwakilishi Abdullah Al-Alimi, pamoja na ukweli kwamba Baraza hilo lilikutana bila kuwepo Wawakilishi Tariq Salih, Al-Bahsani na Al-Arada.

Mwenye kutafakari yaliyotokea Shabwa anatambua kuwa huo ni ubadilishanaji dori kati ya mawakala wasioheshimu ahadi au udugu na watu wa imani na nchi yao. Hamu yao pekee ni kukaa muda mrefu wawezavyo kwenye viti vyao vibovu (viti vya utawala) vilivyotengenezwa kutokana na kuusaliti Umma wao na imani yao, na utiifu wao kwa mfumo wa kikafiri na watu wake. Imepokewa kutoka kwa Ma’qal bin Yasar kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), akisema:

«مَا مِنْ عَبْدٍ يَسْتَرْعِيهِ اللَّهُ رَعِيَّةً يَمُوتُ يَوْمَ يَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لِرَعِيَّتِهِ إِلَّا حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ»

Hakuna mja yeyote ambaye Mwenyezi Mungu atamtawalishia raia kisha akafa siku ya kufa na hali ni mdanganyifu kwa raia wake isipokuwa Mwenyezi Mungu amemuharamishia Pepo.”

Enyi watu wa Yemen, mpaka lini mtaendelea kuwa chachu ya vita ambavyo hamkuhusika navyo?! Watawala hawa vibaraka wameutenga Uislamu na utawala, wameuharibu uchungaji wa watu, na hawakuishia hapo, bali wamemwaga damu yenu. Je, sio wajibu juu yenu kwamba damu iliyomwagwa, na nafsi zilizochukuliwa, ziwe katika njia ya Mwenyezi Mungu kama jihad ya kuubeba Uislamu duniani ili kupata radhi za Mwenyezi Mungu (swt)?! Hilo litatokea tu chini ya Dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume pekee, ambayo Hizb ut Tahrir inaifanyia kazi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aharakishe kusimama kwake.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu